Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

tunataka viongozi wajasiri...nadhani ni zitto peke yake ndani ya uongozi wa chadema mwenye uwezo wa kutoa maoni binafsi ya kumkosoa mzee mtei. Tunaposhauri mkapa astafu siasa kulinda heshima yake nadhani huu ujumbe umuhusu na mzee mtei.huyu mzee amejijengea heshima kubwa sana ndani ya nchi hii ni vema akabaki kama kioo cha mabadiko ya siasa za tanzania.
 
Kitu kizuri pekee naweza kukwambia ni kuwa subiri uje kushurutishwa kufuga midevu ndipo ujue nani mpuuzi kati yako na hii tume!!!
Ina maana wakina Mbowe, Dr Slaa, Mnyika, Lissu na uongozi mzimz wa CDM walioona kauli ya Mzee Mtei ina mushkeri nao hawajaona kama watakuja kushurutishwa kufuga midevu? huwaamini kiasi hicho viongozi wako na unamtetea Mtei?

Halafu inaonekana hujui hata hiyo tume inafanya kazi gani masikini............
 
binafsi sioni ubaya wa kauli ya mzee mtei, kwani ni jambo lisilo pingika kuwa wajumbe wote kutoka zanziba ni waislam, inamaana hakuna wakrisro? wajumbe kutoja bara ni mchanganyiko waislam na wakristo kuonyesha kuwa bara kuna imani tofauti. hivi kama wajumbe kutoka bara wangekuwa wakristo tu, waislam wangekaa kimya? penye ukweli tuongee ukweli, jk ni mdini mkubwa.
 
Nadhani ZITTO kasema ukweli wake, uasisi sidhani kama ni rungu la kuwanyima watu uhuru wa kutoa maoni
Hata Mtei alichoongea ni ukweli mtupu. Just a simple research inaonesha kuwa katika yale majina ya wajumbe wa tume ya katiba waislam ni wengi kuliko wakristo. Zitto kusema mzee Mtei azomewe ni ukosefu wa adabu, ingawa na mzee Mtei kwa hadhi yake hakustahili kuongea kauli kama hizo.
 
mbona wengi wameongea maneno ya hovyo hovyo hawaambiwa wamefilisika mawazo, kama ni kweli Mh.Zito Kabwe kasema maneno hayo basi kuna tatizo ktk jamii, ama sivyo basi ule mradi uliokuwa ukipigiwa chapuo na akina Rejao, FF, Mohamed Said, Topical na radio imani basi utekelezaji wake umeanza.

Yalianza kwa kuita Mfumo kristo baadae wakaona, wanakosa waitikiaji wakaja na mfumo katoliki, still hakuna waitikiaji now wanakuja na katiba. Naomba wajumbe wawe makini kutetea maslahi ya WaTZ na sio kunufaisha kundi fulani ktk jamii
 
Ina maana wakina Mbowe, Dr Slaa, Mnyika, Lissu na uongozi mzimz wa CDM walioona kauli ya Mzee Mtei ina mushkeri nao hawajaona kama watakuja kushurutishwa kufuga midevu? huwaamini kiasi hicho viongozi wako na unamtetea Mtei? Halafu inaonekana hujui hata hiyo tume inafanya kazi gani masikini............
haaa jamani kufuga madevu na tume wapi na wapi?
 
Naanza kuamini maneno ya Tuntemeke kuwa hii tume imeundwa maalum kumsafishia Zitto ndoto yake ya kuwa rais ili aje kulinda maslahi ya swahiba yake Kikwete. Ingawa mimi ni kijana wa umri kama wa Zito nitakuwa mstari wa mbele kupinga kipengele cha umri kushushwa chini ya miaka 40. Kwa malezi na makuzi tunayopitia sisi watanzania ambayo asilimia kubwa ni ya hovyo hovyo sio rahisi kuwa na busara ya kuwa rais before 40. Zitto hata akifika 49 atakuwa hajafikia hiyo busara.
 
chama cha dini ya kikristo........chakosoa waislamu kuwemo kwenye tume......muislamu aliyeko kwenye chama hicho akosoa...! HEADING ILITAKIWA ISOMEKE HIVYO
 
Mzee Mtei aliandika hoja yake kwa niaba yake na sio kwa niaba ya chama. Hata hivyo CHADEMA kimetoa tamko rasmi kuelezea msimamo wako kuhusu uundwaji wa tume. Kama naibu katibu mkuu, kwa nini Zitto anataka atoe kaulu yake pembeni? Hakuridhirika na official statement iliyotolewa na katibu mwenezi wa chama chake - Mnyika?

Pili, Zitto anapata wapi moral authority ya kusema kuwa Mzee Mtei amefilisika kimawazo? kauli za udini zilitumika sana kwenye uchaguzi mkuu 2010, na magogoni waliamua ama kwa makasudi au kutojua matokeoa yake kuwekeza kwenye udini. Na huyu huyu Zitto alijitokeza mbele ya vyombo vya habari akilia udini mara baada ya uchaguzi, na watu walihoji kama kweli jimboni kwake kulikuwa na udini ina maana yeye Zitto alichaguliwa wa waislam tu? wako wangapi watu waliuliza.

Binafsi pamoja na kwamba naona kauli ya Mzee Mtei ni ya utata lakini inatulazimisha kujadili hizi kauli za kichinichini huku mtaani. Kuna radio moja huko Morogoro, Zitto aliwahi kusikia wanaongea nini? Na kama ameisikia ana maoni gani? Ningetaka kuamini kuwa Jambo leo wamemnukuu vibaya Zitto.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Source Jambo Leo ~ Habari Leo. Labda ungesema ama tweet tungekuelewa.
 
Zitto naye kalewa madaraka. Alishindwa nini kusema tu kuwa "hayo ni mawazo ya Mtei binafsi, siyo ya Chama"?
 
Kama kweli Zitto umenena haya pls hama chama.
Toka mapema ili chama kizibe haraka pengo lako.
Mara nataka urais, mara Mzee Mtei kafirisika?
Are you with us kweli wewe?
Ungana na Makamba pls!
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.


hilo gazeti la global pablishaz

zitto ndiyo wa kwanza kulalamikia kasoro za udini kwenye tume yenu ya msikiti, kwenye akaunti yake ya twitter.
 
Zitto hana maadui ndani ya CDM!! Maadui wa Zitto wapo ndani yake mwenyewe Zitto na kutoka kwake kamwe hatakiua chama. Fumbua macho uone wewe.
 
Sioni shida kwa wote wawili,Mzee Mtei kaongea kwa mtazamo wake na Zitto nae kapinga mtazamo wa Mzee Mtei kuhusu kamati na hata mwingine anaweza kutoa maoni yake yakapingwa pia kama yana hisia ambazo hazina tija kwa Taifa.

Binafsi siungi kauli ya Mzee Mtei kwani hatuhitaji wingi wa wakristo na waislamu tunachohitaji ni katiba mpya iliyobeba matarajio ya Watz kuelekea Tz tunayoitaka.
Tubadili mtazamo kuhusu maisha na matarajio yetu na wala sio imani zetu.
 
Jambo Leo is not my reliable source of information!!

I reserve my comments.
 
Unajua watu wanalumbana hapa ndani hata majina ya wajumbe wa hiyo tume hawajayaona, mimi nayaandika haya majina ili unapochangia hoja ujue unachangia nini na wala sio kulaumiana. Nimeandika majina yote ya wanaohusika na tume hii iliyoteuliwa na Mh. Rais.
1. Jaji Joseph Warioba 2. Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani 3. Joseph Butiku 4. Ester Mkwizu 5. Al-Shaymaa Kwegiyir 6. Edmundi Mvungi 7. Profesa Mwesiga Baregu 8. Palamaganda Kabudi 9. Said El-Maamry 10. Riziki Shahari Mngwali 11. Richard Lyimo 12. John Nkolo 13. Jesca Mkuchu 14. Humphrey Polepole 15. Yahya Msulwa 16. Maria Malingumu 17. Mwantumu Malale 18. Dr. Salimu A. Salimu 19. Fatma Said Alli 20. Omar S. Mussa 21. Raya S. Hamad 22.Awadh A. Said 23. Ussi K. Haji 24. Salama Maulid 25.Nassor Hamis 26. Simai M. Said 27. Mohamed Y. Mshamba 28. Kibibi Hassan 29. Suleiman Alli 30. Salama Ahmed 31. Abubakar Alli 32. Ally Saleh 33. Assaa Ahmed 34. Casmir Kyulu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom