Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.
Nioneshe popote niliponukuliwa kusema unavyosema hapa.

Sijawahi kumjibu Mtei moja kwa moja hata siku moja. Kwenye suala hili msimamo wangu niliuweka wazi hat kabla Mtei Hajasema.

Walioandika wameunganisha tu tweets zangu na kauli ya Mtei ambayo siiungi mkono hata kidogo. Mzee was mistaken.

Tume ya Katiba imeteuliwa kwa mujibu wa sheria. Haina Udini. Ina wajumbe ninaowaheshimu sana. Twende tukatoe maoni. Tuache maneno yasiyo na maana yeyote.
 
Hakuna kesi ama ipo, Madaktari wameweka ka loop hole cha kupata rushwa kwenye riport yao, wakipewa tu wanamalizia maelezo yaliyobaki!
 
Mzee mtei kaona mbali subra yavuta heri jana kuna uzi uliwekwa hapa unamuhusu mze mtei na lowasa,waislam wanafurah wanapoona lowasa ukachomolewa hata uhu sina shaka watu watakapo ongezeka na mawazo mbalimbali utafungiwa .lets go
 
Hiki sio kile chama cha magamba ambacho wanaoruhusiwa kuzungumza ni mwenye kaya tu na vibabu waanzilishi wa TANU, huku kwetu kila mtu ana uhuru wa kuzungumza mawazo yake
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Hayo maneno ya mtei angekuwa kaongea sheikh kuhusu wakristo ungesikia hawa wanapenda udini wasubiri wakale ubwabwa kwa vile ni baba mkwe yanakuwa ni mawazo yake binafsi sasa ndio mtajua udini upo au haupo chafya ikija huwezi izuia
 
Mawazo ya Mtei yaheshimiwe kama mawazo ya mtu mwingine, tusimshambulie sana. Mawazo ya Mtei siyo tamko rasmi

Hilo ni tamko rasmi.Hivi matusi ya Lusinde niyake au ya chama? Ufisadi ni wa Mkapa au lowasa na sio CCM?
 
Zitto anaivuruga CDM, au chadema inamvuruga zitto?? Zitto anapanbana na maadui zake ndani ya chadema wasiotaka kuona chama kinatoka minoni mwa wenye malengo maalum!! Mtoeni zitto ili chama chenu kife ili tanzania iendelee kuwa na amani

wewe una mawazo yapi mbona huchangii umesha ambiwa ni mawazo tu ya mzee halafu habari yenyewe ipo kwenye gazeti moja tuuuuuuu jambo la leo hutalisikia kesho limekaa kimipasho zaidi...
mimi napendekeza wakuu wa mikoa na wilaya waondolewe hawana faida kwa watz ni kula kodi zetu tu wala sijui wana kazi gani kila siku zaidi ya kuwakilisha chama yaani wanalipwa ruzuku bado wanapokea mishahara serikalini vyeo kibao kote wakihudhuria wanakula posho
 
Mawazo ya Mtei yaheshimiwe kama mawazo ya mtu mwingine, tusimshambulie sana. Mawazo ya Mtei siyo tamko rasmi

Sasa mlivyokuwa mnalalamika CCM inawatukana kumbe ni Mwigulu na Lusinde yalikuwa mawazo yao binafsi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom