Serikali imeshakamilisha mtego wa kumzima kabisa Dr.Ulimboka. Mtego huo umeratibiwa na Usalama wa Taifa na Polisi kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi. Mtego huo ni upi? Ni hivi:kuna 'Jambazi' la kikenya lililofikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumteka na kumtesa Dr.Ulimboka. Kesi iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Sasa,kuna taarifa kuwa Dr.Ulimboka anaendelea kupata nafuu na ameshaanza kufanya mazoezi mepesi. Ni habari ya kutia moyo. Lakini,Dr.Ulimboka atakaporudi nchini,atatamani akutane na Waandishi wa Habari na kuzungumzia sakata lake. Hilo hatafanikiwa kulifanya.Na akilifanya atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama. Kivipi?
Serikali kupitia Jeshi la Polisi litamuwahi kwa kumwambia kuwa suala analotaka kulizungumzia liko Mahakamani. Dalili za kusimamia mtego huo zimeshaanza kuonekana Bungeni.Ni juzi tu Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Mambo ya Ndani ilizuiwa(baadhi ya kurasa zake) kwa kisingizio hichohicho. Swali litakalobaki ni je,mambo hayo ndio yataishia kwa 'Jambazi' la Kikenya?
Unataka ufafanuzi upi inamaanisha tangu sakata ili lianze huna taarifa na haujui nani alihusika kufanya unyama huo? kama usalama wa Taifa walifanya unyama huo pia ni hao hao watakao taka kufanya hayo yaliyoandikwa na mleta uziVUTA-NKUVUTE Hebu tufafanulie kidogo mkuu, hapo Usalama wa Taifa wanahusika vipi?
Nalo hilo wazo lakini; try as hard as they may, bottom line ni kwamba ukweli utajulikana tu, Newtons 3rd law of motion inasema hivi "to every action there is an equal and opposite reaction" upo hapo, tafakari na kwa kuwa swala hili liko mahakamani tusilijadili hapa kwenye forum maana kadiri unavyojieleza sana ndivyo vivyo hivyo unavyojiachia kupigwa sucker punch" waache waendelee kuandaa mkikakati ya hujuma lakini kaa tulia ukweli wa sakata la Dr. ullimboka litaanikwa siku si nyingi. tul
but action and reaction takes place on different bodies.
Yesu anachukia dhambi, bali anampenda mdhambi.
Jamani hivi kamanda Uli ni mwanachama/mshabiki wa chama gani?
kuna taarifa zisizo rasmi zinasema kwamba amehasiwa kipindi cha kuteswa.sasa kama ameshahasiwa kutakuwa na faida gani ya kuficha ukweli wakati kimsingi ni kama hana tena kitu cha kupoteza.akinyamazishwa tunamuombea dua apasuliwe tena na afe kabisa.mungu azidi kumpa afya ili tuone mwisho wa hii senema.ila tusishangae atakapokuja na kuomba suala lake lisizungumziwe.
bongo fitna nyingi hawachelewi kwenda kumnyamazishia huko huko.
Lakini ninamuombea ujasiri kutoka kwa Mwenyezi Mungu aje afunguke na Wovu wake waaibike.
ukimuona mtu ana tatizo jichoni,puani,sikioni,mdomoni,kichwani,ulimini na popote penye kiungo kinachotawala mfumo wa utambuzi na hisia za binaadamu basi ujue huyo hayuko sawa kwa % zote.sasa kwa maelezo hayo hujaona kasoro yeyote kwenye kiungo chochote cha kova,nawasilisha.Huu ni mtego wa serkali iliyochoka,serikali dhaifu inayoongozwa na Rais dhaifu,chama dhaifu na sera mbovu!
Mhe.Msigwa hivi karibuni wakti akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu alisema,ninanukuu,"Tatizo kubwa tulilo nalo kwa sasa kwenye nchi yetu ni kwamba,TUMERUHUSU AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA!(English:Small/foolish mind to lead intelligent mind!) Huu ni ukweli ulio wazi kabisa.
Kwamba kwa sasa serikali ya majuha(small mind)inaongoza Watanzania wenye akili zao timamu kwa kujaribu kuwarubuni na kuwalaghai kwa mitego ya kipumbavu ambayo hata mtoto wa std 1 anaweza kuing'amua. Watanzania tunajua kabisa kuwa KOVA AKISHIRIKIANA NA UWT WAMEPANGA KUTAFUTA KICHAA MMOJA NA KUMBANDIKA URAIA WA KENYA KWA MADAI KWAMBA YEYE NDIYE AMEHUSIKA NA KUMTEKA,KUMTESA NA KUHATARISHA MAISHA YA DR.ULIMBOKA! MARA TU BAADA YA KOVA KUUTANGAZIA UMMA KUWA WAMEMKAMATA MTUHUMIWA HUYO BASI AKATANGAZA RASMI KUWA MJADALA WA DR.ULIMBOKA UMEFUNGWA MAANA TAYARI SWALA LIKO MAHAKAMANI!
CCM NA SERIKALI YAO BADO WANAFIKIRI WA-TZ WA SASA NI WALE WA MIAKA YA KARNE YA 19! KWAMBA WANAWEZA KUDANGANYWA KWA PROPAGANDA ZA KIHUNI KAMA HIZI!CCM NA SERIKALI YAKE WAMESHAGEUZA KUWA MAHAKAMA NI KICHAKA CHA KUTAKA KUFICHA MADHAMBI YAO.KWAMBA WAKISHAONA JAMBO AMBALO LITWAUMBUA BASI WATAKIMBILIA MAHAKAMANI ILI KUWAZIBA WATU MIDOMO WASIENDELEE KUHOJI MAANA LIKO MAHAKAMANI!!!HUU NI UPUMBAVU NA UJINGA AMBAO LAZIMA UKOMESHWE MARA MOJA! OK,HATA KAMA NI KWELI KUWA SWALA LILILOKO MAHAKAMANI HALILITAKIWI KUJADILIWA,BASI IWE NI KWELI LIMEFUATA HATUA ZOTE ZA KISHERIA,KIUPELELEZI NA KUTIWA HATIANI KWA MTUHUMIWA/WATUHUMIWA. TUNACHOKIONA KWA SWALA LA DR. ULIMBOKA NI MCHEZO WA KUIGIZA! HAIWEZEKANI UKAMATE KICHAA/MWENDAWAZIMU HUKU UKIWAACHA WATUHUMIWA MUHIMU(SUSPECT NO.1)WALIOTAJWA NA DR.ULIMBOKA KUWA WALITOKEA IKULU.WA-TZ TUNAHOJI WAKO WAPI HAWA AFANDE KOVA???ARE THEY STILL AT LARGE????MTU ANAYEFANYA KAZI IKULU ATAKIMBILIA WAPI KAMA SIYO LONGOLONGO TU??
TUNASEMA HATUTAKI UONGO HUU WA MCHANA KWEUPE,MAYBE YOU NEED TO CHANGE YOUR TECHNIQUE CAUSE THIS ONE HAVE PROVED A TOTAL FAILURE!
Mkuu, mbona hii picha iko peupe mno, ni nini unachoshindwa kuelewa ??
Unashindwa kuelewa kuwa "Mkenya feki yupo mahakamani" ??? au
Unashindwa kuelewa kuwa serikali ina mkono wake kwa Dr. Ulimboka ??
au Unashindwa kuelewa kuwa Dr. ulimboka kama mtu aliyetaka kuthuriwa atakuwa shahidi muhimu katika kesi hii ya kichina????
Swali la msingi; Serikali kupitia kwa Polisi na Tiss ndio watuhumiwa wa kwanza, Je ndo watakoahusika pia kumhoji Dr. Ulimboka????
Waandishi wa habari wamfuate huko huko ,kama wale waandishi wa Kimataifa wanaweza kuifanya kazi hiyo ,au hata madaktari wanaweza kumfanyia mazungumzo na kuhusisha masuali mazito kwake ,kama anawafahamu waliomteka ,kuwataja majina kiasi ya kuelezea kisa kizima kwa yale anayoyakumbuka na kuwa yenye usaili wa kideo sio audio.