Mtazamo wangu: Walimu wa diploma ni bora kuliko ambao hawajapitia diploma wakapata degree

Nimekuwa kwenye fani ya ualimu kwa muda mrefu sasa, moja ya vitu nilivyogundua (baada ya research) ni kuwa walimu wazuri ni wale waliosomea diploma ya ualimu, wakaenda makazini, au makazini then chuo kikuu. Sababu ni
1. Wanajua teaching strategies zaidi ya ambao wameunganisha chuo kikuu.
2. Wanajituma kazini zaidi
3. Wanajua matumizi ya lugha nyepesi na inayoeleweka kwa wanafunzi.
4. Wana manage discipline ya darasa vyema
5. Wanapenda kujifunza mambo mapya

Siyo mzima ww, kapime uwezo wa ubongo wako.
 
Nimepitia maisha ya ualimu ivyo nayajua vizuri,anidanganyi mtu...
unajua kuna tofauti kubwa kati ya mwalimu wa diploma na wa degree,haswa kisaikolojia na ufahamu wa vile vitu anavyofundisha...
Walimu wa degree wanajua sana vitu,na pia wanajiamini,wanajitambua,wanaumiza vichwa usiku na mchana kutafuta maslai zaidi..
Walimu wa diploma ni wanyenyekevu kupita kiasi,wamelidhika na maisha na wako shalo vibaya kichwani..

Pia wa dip wanapenda sana vyeo ata kama havina faida yoyote,ndio maana utawaona ful kujipendekeza kwa ma afisa elimu..wanawapelekeaga vitunguu,kuku,nyanya,matunda yote ni kujaribu kukumbukwa kwenye ufalme.

Ni kama mtoa mada alivyokuja kupunguza stress zake hapa!

mbona elimu yako haijakukomboa? Jibu hoja, acha kushambulia mtu. Small minds discuss people
 
ndio tatizo lenu walimu wa diploma,mnafikiri mwalimu lazima uvae kishambashamba ndio haiba...mwalimu akivaa kileo basi mnamwita sharobaro.
Nimepitia ualimu na nilikuwa wa degree,unakutana na ticha wa dip kavaa shati la zambarau,tai ya kijani,suruali ya njano ina vidraft vyeupe alafu inamarinda kibao,kiatu brown''asante mchaga'',booonge la mkanda kiunoni,muda wote anatema jasho...sasa akikutana na mwalimu kavaa shati zuri e.g levis,suruali kadeti,kiatu ngozi safi e.g gucci ,ananukia vizuri,akiwa ofisini mara kafungua laptop mara kaingia bbm...hapo utakuta ticha wa diploma anakujengea bifu staff ukimuuliza kisa nini eti oooh uyu jamaa analinga sana kwa ajili ana degree,anajifanya sharobalo...

pinga kwa hoja mkuu!
 
kujua content na kushindwa kuiwasilisha kwa wanafunzi ni kuwa bora mwl na si mwl bora!
 
sasa nyie walimu badala ya kupigania maslahi yenu,nyie mnakomaa kushindana nani mwalimu zaidi...
Mmeridhika na vipato vyenu??
 
kwa mjadala kama huu nadhani tunaweza kuhitimisha kwa kusema, WALIMU WA CHUO KIKUU TATIZO SI LAO BALI NI LAO + MFUMO MBOVU. Nawashukuru kwa mjadala, tupunguze harakati na tufundishe watoto, hatukomoi CCM bali ndugu zetu masikini:clap2:
 
Back
Top Bottom