Walimu wa awali wenye ujuzi wazingatiwe ili kuinua elimu nchini

hot boy

Member
Jan 17, 2023
85
167
Habari za mida hii Wana jamii forum.

Mimi ni mdau wa ELIMU na mtaalamu wa ELIMU ya AWALI lakini nimegundua mapungufu baadhi katika ELIMU ya AWALI ambayo yakifanyiwa kazi tatizo la kusoma na kuandika halitakuepo Kwa wanafunzi wa shule za msingi.

1.Walimu wengi wanaofundisha madarasa ya AWALI sio waliosomea ELIMU hiyo, Kwa maana kwamba wapo WALIMU ambao wamesomea ELIMU ya kawaida msingi lakini wanafundisha madarasa ya AWALI hapo tayari Kuna utofauti, vile vile wapo walimu ambao hawana taaluma rasmi ya ualimu ila Wana uzoefu wa kufundisha ELIMU ya AWALI hawa ni wale wazee au wamama/wadada walioonekana wanajua kufundisha lakini hawana taaluma ya ELIMU ya awali.

Hawa mara nyingi hupata wakati mgumu yanapotokea mabadiliko ya mtaala kwani kuwapeleka semina ni vigumu mana sio walimu waajiriwa wa serikalini Kwa maana hiyo semina za mitaala mipya wengi huzikosa na hata kama wakipatiwa semina hizo ni kupitia Kwa walimu wengine ambao walienda semina.

2. Wataalamu wa ELIMU ya awali kupangiwa majukumu mengine. Zipo shule ambazo walimu wa awali wenye ujuzi hupewa majukumu ya kufundisha madarasa ya juu kama darasa la Tano mpaka la saba hasa pale wanapoonekana kuwa na ELIMU ya stashahada (diploma) au shahada (degree).

3. Kukosekana Kwa ubunifu wa michezo zana za kujifunzia na kufundishia Kwa ELIMU ya AWALI badala yake watoto kukaa darasani tu Kwa muda mrefu. Hii imechangiwa na kukosekana Kwa walimu wenye ujuzi na ELIMU ya AWALI, katika vyuo vya ualimu mwalimu wa ELIMU ya AWALI hujifunza michezo nyimbo na mbinu nyingi za kutengeneza zana za kufundishia na kujifunzia lakini ukija kwenye uhalisia ni wachache hufanya hivyo zile mbinu zinasahaulika kabisa watoto wanajifunzia ndani ya darasa tu jambo ambalo sio sahihi.

Mwisho, ombi langu Kwa wizara ya ELIMU ; Mtaala wa ELIMU ya AWALI upo vizuri ila wataalamu ni tofauti sio wale walioandaliwa kufundisha ELIMU ya AWALI wanaofundisha huko wengi wao ni walimu wanaokaribia kustaafu na wazee jambo ambalo sio sawa.

Ifike mahali ELIMU ya AWALI ifundishwe na walimu walioandaliwa Kwa ajili ya ELIMU ya AWALI na sio ELIMU ya msingi au wadada wasio na taaluma ya ualimu.

Asanteni sana
 
Back
Top Bottom