' Mtambuzi jipe moyo utayashinda'

Pole sana ndugu Mtambuzi... Pamoja sana.


Mwali nimeshapoa na namshukuru Mungu, jana kwa kushirikiana na majirani tulimudu kuyaelekeza maji yafuate mkondo tukajisitiri kwa jirani kwani magodoro yote yalilowa kabisa...............
 
Pole sana Mtambuzi nadhani mwaka huu haukuwa mzuri sana kwako kutokana na matatizo yaliyokukumba. Jipe moyo.

Kuna jamaa mmoja juzi alikuwa ananitania kwamba sasa inabidi nikae kimya maana kama kila nikipata tatizo nalianika nitaonekana mlalamishi..................... Kwa kweli sikupanga kuzungumzia mkasa huu wa mafuriko ulionikumba maana nilijua siko peke yangu. naamini wako wana JF wengi waishio Tabata na ninadhani huenda nao wamepata tatizo kama langu...................
namshukuru sana Ndyoko kwa kunipigia simu jana na kujua hali ya familia yangu, kwani yeye anajua kwamba ninaishi TABATA. Nilimjulisha kwamba niko kwenye dhahama ya mafuriko na nyumba ninayoishi imejaa maji kiasi kwamba kila kitu ndanin kimelowa.......

Siwezi kutathmini hasara niliyoipata kwa sababu ni mapema mno, lakini namshukuru Mungu kwamba kaiweka familia yangu salama.......
nawapa pole wana Tabata wenzangu ambao nao wamepambana na kisirani hili cha mvua na mafuriko, naamini tupo pamoja
 
Pole sana Mtambuzi...mwaka huu umeumaliza vibaya! Nimejaribu kufuatilia matukio yaliyokukumba ndani ya hii miezi michache na mengi ni ya kusikitisha! Usikate tamaa, Mungu yupo nawe.
 
Pole sana Mtambuzi...mwaka huu umeumaliza vibaya! Nimejaribu kufuatilia matukio yaliyokukumba ndani ya hii miezi michache na mengi ni ya kusikitisha! Usikate tamaa, Mungu yupo nawe.

We bwana weee.......... haya mambo kwa binadamu yeyote ni ya kawaida, unajuwa kuna watu wanpata mitihani na hawasemi wako kimya tu.....................

nakumbuka mwaka 2003 kama sikosei ilipotokea ajali ya basi la Msae, nilikuwa naenda kibaha kwa shughuli zangu, nilikuwa nimekaa siti moja na jamaa mmoja ambaye tulitokea kuzoeana na kupiga stori kama kawaida, alionekana kuwa mchangamfu sana kwangu utadhani tunafahamiana kwa siku nyingi. Tulipofika Kibaha, tulishuka na kuagana. nilifika kwa mwenyeji wangu nikaambiwa yuko Tumbi Hospitalini kaenda kumuona mtoto wa dada yake ameungua na maji ya moto, niliamua kwenda huko Tumbi Hospitali ili kumuona mgonjwa, nilipofika nilimkuta yule bwana niliyekuwa nimekaa naye kwenye daladala akiwa pale nje na jamaa watatu wakiongea, nilimfuata na kumuuliza mbona yuko pale. Alinijulisha kwamba amekwenda pale kutambua maiti kwani katika ajali iya basi lam Air Msae amempoteza mkewe na mtoto wake mchanga na mdogo wake wa kike aliyekuwa kidato cha pili,, mkewe alikwenda kujifungua huko Moshi na ndiyo alikuwa anarudi kuungana na mumewe............... hii ina maana kwamba hata hakupata bahati ya kumpakata mwanae akiwa hai ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kuzaliwa tangu wafunge ndoa na mkewe mwaka mmoja uliopita!

Nilishangazwa sana na ujasiri wa yule bwana, na nilijifunza mengi kupitia kwake, kwamba pale tunapopata matatizo tusipige mayowe, kuna walio na matatizo zaidi yetu...........................
 
mkuu pole sana naona huu mwaka haukuwa mzuri sana kwako tuendelee kuamini katika mungu maana ni majaribu ya kidunia .. pia katika kaleda tumebakiza kama siku 9 tuahau machungu ... kuwa na moyo wa uvumilivu
 
may GOD firm hand be with you at this hard time....
pole sana mwanajamii, kwa mapito unayopitia....
 
Back
Top Bottom