Pure nomaa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2011
- 1,158
- 1,382
Pole sana mkubwa ila kumbuka matatizo yakizidi sana ujue neema inakaribia
Pole baba mkwe.
pole sana kuu,,,,, kwani ulijenga bondeni????
We bwana weee.......... haya mambo kwa binadamu yeyote ni ya kawaida, unajuwa kuna watu wanpata mitihani na hawasemi wako kimya tu.....................
nakumbuka mwaka 2003 kama sikosei ilipotokea ajali ya basi la Msae, nilikuwa naenda kibaha kwa shughuli zangu, nilikuwa nimekaa siti moja na jamaa mmoja ambaye tulitokea kuzoeana na kupiga stori kama kawaida, alionekana kuwa mchangamfu sana kwangu utadhani tunafahamiana kwa siku nyingi. Tulipofika Kibaha, tulishuka na kuagana. nilifika kwa mwenyeji wangu nikaambiwa yuko Tumbi Hospitalini kaenda kumuona mtoto wa dada yake ameungua na maji ya moto, niliamua kwenda huko Tumbi Hospitali ili kumuona mgonjwa, nilipofika nilimkuta yule bwana niliyekuwa nimekaa naye kwenye daladala akiwa pale nje na jamaa watatu wakiongea, nilimfuata na kumuuliza mbona yuko pale. Alinijulisha kwamba amekwenda pale kutambua maiti kwani katika ajali iya basi lam Air Msae amempoteza mkewe na mtoto wake mchanga na mdogo wake wa kike aliyekuwa kidato cha pili,, mkewe alikwenda kujifungua huko Moshi na ndiyo alikuwa anarudi kuungana na mumewe............... hii ina maana kwamba hata hakupata bahati ya kumpakata mwanae akiwa hai ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kuzaliwa tangu wafunge ndoa na mkewe mwaka mmoja uliopita!
Nilishangazwa sana na ujasiri wa yule bwana, na nilijifunza mengi kupitia kwake, kwamba pale tunapopata matatizo tusipige mayowe, kuna walio na matatizo zaidi yetu...........................
Baba Mkwe!? au ndio unajiandaa kumchumbia mwanangu Ngina?
Ahsante sana Fidel80
Dingi tulia! Ni Cantalasia huyo, mahari yako ntahakikisha unaletewa.
Pole Mkuu, Mungu atatunusuru na hili janga
Haaa haaa haaa,Dingi tulia! Ni Cantalasia huyo, mahari yako ntahakikisha unaletewa.