Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,465
- 4,678
Hivi ni visa vya kweli vinavyotokea ili tujifunze graduate na wapambanaji wengine someni hapa. Hakuna cha nitaendelea nitafupisha zaidi iwe fupi.
Ni Mimi pastor prakatatumba abaabaabaabaa etumba etumba.
Ndugu zangu kwanza nikiri jiji la Dar es Salaam watu wanapambana saaana tena saana, kuna variation kubwa Sana kati ya wenye nacho na wasiokua nacho lakini haiondoi wewe kufurahia jiji, kuna bata la pesa ndefu Kama huko kidimbwi (sijawahi kufika), na kuna bata letu sisi wahangaikaji Kama manzese uwanja wa fisi, Sudan temeke n.k.
Nilitokea tabora kuja kuhangaika na maisha baada ya kumaliza chuo na kukaa mtaani takribani mwaka mzima mzee alivyouza pamba akanipatia million mbili, nilipewa husia takribani masaa 7 kwamba nikipoteza huo mtaji nisimwambie kitu nipotee kabisa nisirudi nyumbani maana hiyo ndio ilikua akiba yake na Mimi ndio kijana mkubwa nina wadogo zangu kama 8.
Nilifikia dar tandale kwa tumbo kwa mshikaji wangu tulisoma nae tabora lakini hakufanikiwa kuendelea na masomo, Mara ya kwanza alinichangamkia huku nikimueleza mipango yangu ya biashara n.k, nilikua sijui sehemu yoyote ile dar wala sijui biashara yoyote ile huyo jamaa yangu alikua anafanya kazi kiwandani tegeta wazo ( sina hakika Kama panaitwa hivyo) , akaanza kunitembeza kujua jiji ile kunitembeza tu week Mbili Kama laki 5 ilishakata nikajipa moyo bado hela hipo, mshikaji wangu akawa hachangii chochote nikawa nanunua misosi nikasema fresh jamaa ananisitiri.
Kufupisha story million 1.5 ilikatika ndani ya mwezi na nusu hivi Mimi bila kujua imeenda wapi (usije mjini bila mipango).
nilipobakiza laki tano nikaenda kariakoo nikanunua "sendoz" za kike kwa laki 4 na 80 hivi (nilikua nikipita naona watu wanauza sana hizo sendo wadada wamewazunguka wananunua nikaona fursa) jamaa akanikodisha Eneo lake 10,000 kwa siku pamoja turubai lake (hakunambia Kama migambo wamekataza).
Mimi sikuelewa watu ni wengi nikamwaga chini nikaanza kuuza zile sendoz nikajisemea moyoni biashara si ndio hii? Chap chap nimeshauza kama 70,000 huku nafurahia moyoni ghafla nikaona watu wanakimbia kimbia Mimi sikujali nilikua sielewi kinachoendea kuja kushtuka nimepigwa rungu la kisogo kwa akili yangu ikaanza kuniambia hawa watakua ni majambazi nini?
Hapo network imekata kichwani damu zinavuja ikabidi na Mimi nianze kukimbia kuelekea uelekeo wa wa watu wanapokimbilia, shati langu limeloa damu nikafika sehemu nikanunua maji ya kandoro nikanawa kichwa hapo nimevimba haswa kurudi kwenye mzigo wangu sikuukuta wakanambia migambo wamechukua itabidi niende nikafatilie niandae faini n.k
Nilikuwa na maumivu makali ya kichwa uchungu wa jiji la Dar nikaanza kuuona hapo kumbuka nina mwezi mmoja tu Dar, nikarudi gheto kulala huku nikiwa na mawazo tele hela nimebakiza elfu 80, mzigo wangu umechukuliwa "nikaconfirm" msemo wangu ambao unasema ukizaliwa maskini ni ngumu Sana kutoboa kwenye haya maisha yani ni ngumuuu, nikikaa barabrani nasema hawa walipataje hayo magari? Majumba yalioko mbezi kule, goba nikawa najiuliza nitatoboa kweli? Kwa 80,000?
Mshikaji wangu alikua anapenda kwenda viwanja so alikua ananipeleka maeneo mbali mbali naona vijana wadogo wakiendesha magari wameacha vioo wazi namimi nimetokea bush kuona gari labda la serikali nilikua napata mawazo Sana.
Turudi kwenye story baada ya kupigwa rungu la kichwa nimerudi ghetto mshikaji baada ya kumuelezea yaliyonikuta nikamwambia anitafutie kazi pale kiwandani nadhani kilikua kiwanda cha cement akanambia akirudi kesho yake kutoka job ataniambia.
jioni jamaa kurudi kanambia imeshindikana kupata kazi na anataka kuoa mpenzi wake anakuja so nitafute makao mengine (kumbuka hajawahi kunambia habari za mpenzi wala nini) kwakua Mimi ni mtu mzima nikajiongeza kwamba hapa hela imeisha sitakiwi.
To cut story nikaenda pale tandale kwa wauza mchele nikawa napiga story na wabeba mizigo pale, gari likaingia limetoka mbeya nikaomba kazi ya kupakua mchele kila gunia 500 nikafanya kazi ya kupakua mchele mpaka saa Saba usiku.
Baada ya kazi nikawa napiga story na mlinzi nikamwambia hali halisi ya maisha yangu nikamwambia natafuta pia chumba cha bei rahisi, akaniambia kuna mtu ataniunganisha hakuna hela ya dalali na chumba ni 30,000 nikasema sawa, usiku mzima nikalala pale akanipatia namba ya mwenye nyumba.
Asubuhi nikarudi kwa jamaa yangu nikavaa nguo zangu za kitanashati kidogo nilizotoka nazo chuo (zilizo survive maana zingine zilishachakaa na kuisha)
Nikatoka nduki mpaka buguruni malapa na begi langu la nguo mgongoni kibembe mwenye nyumba anataka miezi 6, na Mimi ninayo Kama 90,000 pamoja na hela niliyoipata baada ya Kushusha mzigo, nikamwambia mwenye nyumba nimekuja dar kufanya kazi maalumu itakayonifanya nikae mwezi mmoja na nusu sasa nikilipa miezi 6 itakua ni hasara na Mimi sina hata godoro na nguo zangu zipo kwenye ili begi la mgongoni, tena nikamwambia sidhani Kama nitamaliza miezi miwili chukua hii 60,000 baada ya mwezi mmoja na nusu nitakua nimeondoka, nimekuja kufanya kazi za serikali.
Alikua yuko excited kusikia hivyo kusikia kazi za kiserikali tena nilivyomwambia sina vyombo wala kijiko akaniamini akanipatia na godoro la kulalia kumbe muhuni ndio nimekuja kuanza maisha, amna cha kazi ya serikali wala nini sikua tu na kodi target yangu ni kwamba baada ya mwezi nitakua nimempatia kodi yake ya miezi sita.
Nimeandika sana Naendelea kuandika kwa chini sehemu ya mwisho ambalo litakua ni funzo kwa vijana wanaopambana na graduate wasiokua na ramani.