Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Ni kweli maafa ya mafuriko yanaitwa natural disasters, lakini sio lazima natural disasters zilete maafa kwa raia na mali zao.
Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe, ubinafsi, kutojali, na uongozi mbovu kwa ujumla wa viongozi wa serikali. Si mara ya kwanza Dar es Salaam inapata mafuriko. Ni zaidi ya miaka 20 tunaishi kwa kudhani kwamba tatizo la mafuriko Dar dawa yake ni kumwomba Mungu atuepushe na vifo na upotevu wa mali, kutia ndani uharibifu wa miundombinu.
Mji wowote ulio pembezoni mwa bahari kuwa na tatizo la mafuriko yanayotokana na mvua kwa zaidi ya miaka 20 hakuna kingine zaidi ya uzembe. Serikali yetu imejisahau mno, hasa wakijua Watanzania sio rahisi kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa kuwa tu inafanya uzembe, ufisadi, ubinafsi nk. Kwa hiyo wanajisahau sana.
Tatizo la mafuriko linahitaji suluhisho ambalo gharama yake huenda hata isifikie gharama ya kununua ndege mbili za dreamliner, au pesa tunayolipa makampuni yanayotushitaki kukiuka mikataba.
Ikibidi, baadhi ya majengo itabidi yaondoke, yabomolewe, hata kama ni mazuri kiasi gani.
Ninatamani sana nimpigie Samia simu nimwambia nipe hii kazi nisimamie huu mkakati. Raisi Samia nakuhakikishia kwamba mji wowote uliopo kando ya bahari haupaswi kuwa na mafuriko kama tunayoona Dar. Au mwambie Prof. Tibaijuka asimamie hili.
Tatizo lililop kwako Samia ni kuteua watu ambao wanaona kipao mbele cha Dar ni kushughulika na changudoa na maandamano ya Chadema badala ya matatizo yanayoathiri wananchi na taifa kwa ujumla kwa kiwango cha juu sana. Unapewa sifa kila siku katika mambo ambayo ni routine sana, usiridhike au kudanganywa na hizo sifa. Kutoa hela za kujenga Zahanati na nini sijui sio sifa za kuwa raisi mzuri. Kwanza wengine tunaona hilo ni uongozi mbovu tu, kwa sababau pesa hizo zinapaswa kutolewa kupitia mipango ya maendeleo na bajeti za maeneo hayo. Kwa nini unakubali kuleweshwa na sifa za mambo yanayotakiwa kufanywa na wakuu wa mikoa na wakurgenzi wa miji na majiji? Fanya kazi za kitaifa tukusifie, sio mambo ya vijijini, wilayani na mikoani. Hiyo sio ligi yako.
Bado hatuoni unayofanya katika mambo makubwa ambayo yataacha legacy yako, pamoja na hili la mafuriko Dar. Japo tunaelewa ni suala la majiji haya matatu, Ilala, Kindondoni na Temeke, lakini lichukue sura ya kitaifa ili kuwe na coordination rahisi.

- Wakusanye wataalamu wa physical geography watengeneze topographical na contour maps za Dar es Salaam na ukanda wa pwani, wakionyesha ilikupata elevation na terrain ya ukanda wote wa Dar na contour lines zinavyokwenda
- Kwa kutumia topographical map na contour lines, wakusanye civil engineers wachore line kupitisha maji kwa kutumia channel za ukubwa wa kiasi na kupeleka kwenye channel kubwa ambazo zitaelekeza maji baharini