Popo tishio kwa maisha ya Wakazi wa Upanga Dar es Salaam

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
popo-pic.jpg

Na Francis Godwin
Changamoto ya Ndege aina ya popo imekuwa ni Tishio Kubwa kwa wakazi wa Mtaa wa Seaview Kata ya Kivukoni Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Madhara ya popo yanaweza kutofautiana kutoka kwa kipindi cha mwaka na eneo.

Hapa kuna madhara kadhaa yanayoweza kutokea kwa sababu ya popo:

Ikumbuke Popo wanaweza kusambaza magonjwa kama vile Ebola, virusi vya Nipah, na kadhalika. Kwa hivyo, wanaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu.

Baadhi ya spishi za popo wanaweza kula matunda na kusababisha uharibifu wa mazao, hasa katika maeneo ya kilimo.
IMG_20231020_110209_9.jpg

Mti ikiwa imepunguzwa matawi kupunguza popo

Pia Popo wakipaa usiku wanaweza kutoa sauti za kelele ambazo zinaweza kuwa kero kwa watu wanaoishi karibu na maeneo yao ya makazi.

Popo wanaweza kuacha kinyesi chao katika maeneo wanayoishi, na hii inaweza kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Aidha popo wana jukumu muhimu katika mazingira kama vile kusaidia katika udhibiti wa wadudu na kusambaza mbegu za miti. Kwa hiyo, hatua zinapaswa kuchukuliwa kwa kuzingatia athari za mazingira na afya wakati wa kushughulika na popo.

Wakazi wa eneo la Upanga ambalo linachangamoto kubwa ya Popo wanasema kuwa imekuwa ni Kero ya Muda Sasa na Njia pekee wanayoitumia ni kukata miti ama Kupunguza matawi ya miti ili Kupunguza Popo.
IMG_20231020_121820_7.jpg

Wafanya usafi eneo la Mtaa wa Kiriman Kata ya Kivukoni


Alisema Mkakati huo ni mzuri japo unachangia Kwa kiasi kikubwa kuharibu mazingira .

"Tunafanyaje hatuna Njia nyingine zaidi ya kukata miti ama Kupunguza matawi ya miti vinginevyo Popo ni Kero na wanapiga kelele Sana " alisema mmoja kati ya wafanyakazi wa hotel iliyopo eneo la Upanga .

Kuwa hotel Zenye popo wengi hata Idadi ya wageni hupungua hivyo tunaomba Serikali kuchukua hatua ya kuangamiza Popo .

Hata hivyo alisema wanashindwa kuchukua hatua ya kuangamiza wao wenyenye Kwa kuogopa kuchukuliwa hatua Kutokana na Sheria ya haki za wanyama.

Pia walisema walishafanya mkutano wa mtaa ulioitishwa na Serikali ya mtaa wa Seaview kata ya Kivukoni mkutano uliofanyika mapema Mwezi huu na moja kati ya Kero kubwa ni juu ya Popo hao kusumbua wananchi.

Kwa upande wake Asha Alli ambae ni mmoja kati ya wanakikundi Cha Usafi mtaa wa Kimara Kata ya Kivukoni alisema Kuwa wao kama watu wa Usafi wanapata Usumbufu mkubwa Sana kuwepo Kwa Popo hao Hadi wanatamaniy kuhamishwa eneo la Usafi.

Mbali ya kutojua Madhara yanayoweza kusababishwa na Popo hao hasa juu ya Afya ya mwanadamu ili alisema wakati mwingine Popo wamekuwa wakiwakojolia ama kuwanyea wakati mwingine popo wamekuwa wakichafua mazingira Kwa kukata majani ya miti hivyo kulazimika kufanya Usafi zaidi ya Mara moja eneo moja.

Huku baadhi ya Vijana wanaofanya kazi za kusafisha viatu chini ya miti wanadai kuwa mbali ya miti kuwa na kivuli kizuri ila wanalazimika kutumia miamvuli Ili kujikinga na mkojo na kinyesi cha popo kwani wamekuwa wange zaidi .
IMG_20231020_122707_4.jpg

Wasafisha viatu eneo la Upanga wakiwa chini ya miamvuli kujikinga na popo

"Hii miamvuli unayoiona sio kwa ajili ya mvua tunalazimika kuingia gharama kununua miamvuli Ili kujikinga na kinyesi na mkojo wa popo kama unavyoona sisi wenyewe hatutaki miamvuli tunataka kivuli safi cha miti ila tunafanyaje"

Hata hivyo uongozi wa Serikali ya mtaa huo haukuweza kupatikana kuelezea mikakati ya Kupunguza Kero hiyo kutokana na kutokuwepo ofisini Ijumaa Octoba 20 mwaka 2023 majira ya Saa 6:45 mchana .

Aprili 19 mwaka 2023 akiwa ndani ya bunge Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameiomba Serikali kupeleka haraka watalaam katika kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam ili wakawaondoe popo waliogeuka kero.

Sheria za kulinda wanyama na ndege zinalenga kudhibiti shughuli za kibinadamu ambazo zinaweza kuathiri mazingira na viumbe hai. Sheria hizi zinaweza kujumuisha:

Sheria za Uhifadhi wa Wanyama: wanyama wanaweza kuwindwa na kwa muda gani. Pia, hulinda spishi za wanyama walio hatarini kwa kutoweka.

Sheria za Mazingira: Zinaweza kudhibiti uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa makazi ya wanyama na ndege.

Chanzo: Matukio Daima Media
 
Waleteni wakaazi wa Wuhan wawafundishe namna ya kuwageuza kitoweo. Ni miezi michache tu wote watatoweka
 
Ndege aina ya popo
Is a bat a bird or a mammal?

VISUAL COMPARISON​

MammalsBirds
Body CoveringHair or FurFeathers
MetabolismLowerHigher
OffspringLive BirthEggs
Parental CareExtended, with nursingVaries, no nursing
LungsSpongy, sac-filledAir sacs, continuous airflow
LocomotionDiverse (walking, running, swimming, flying)Primarily flight (some exceptions)
Heart and CirculationFour-chambered heart, double circulationFour-chambered heart, efficient double circulation
Sensory PerceptionStrong smell and hearing, variable visionExcellent vision, variable smell and hearing
Vocal CommunicationLess common, less complexFrequent, often complex
LifespanVaries, often several decadesVaries, often several years to decades
Diet and Teeth/BeakVaried diet, specialized teethVaried diet, specialized beaks
Adaptation to EnvironmentsTerrestrial and marine habitatsAlmost every available habitat
Social StructuresVaries from solitary to socialVaries from solitary to gregarious
Brain Size and IntelligenceLarger brain/body size ratio, high intelligence in someSmaller brain/body size ratio, high intelligence in some
Conservation StatusMany endangered speciesMany endangered species
 
Back
Top Bottom