Msisikitike, kuna njia ingine

Miaka kadhaa iliyopita Kibaki alitaka kufanya hichi anachokifanya sasa Jakaya ya kuandika katiba anayoitaka yeye sasa baadae kutakiwa kuwa na kura ya maoni kuikubali au kukataa njia hii.Wapenda mageuzi wa kweli wakajipanga na kupita nchi nzima kuipinga na kuwashawishi watu waikatae kwa kupiga 'NO' walijulikana kama orange,na upande wa Kibaki wa 'YES' ulijulikana kama ndizi.
Upande wa 'NO' au Orange ulishinda na hivyo kumlazimisha Kibaki kutumia njia ya kuwashirikisha Wakenya wote katika kuandika na kupitisha Katiba hii nzuri waliyoipata sasa.
Kwahiyo ni kujipanga tu wakati wa kura ya maoni kuhamasisha wananchi kuikataa Katiba hii,inawezekana kila mmoja akishiriki kikamilifu.

Mkuu' muswaada unasema kama kura za hapa zitashinda' basi katiba iliyopo itaendelea.
 
Mkuu' muswaada unasema kama kura za hapa zitashinda' basi katiba iliyopo itaendelea.

Afadhali umewaweka sawa, CCM wanataka kujua popo ni mnyama au ndege??? jibu peleka popote ni sawa.Tukipiga kura ya No maana yake HATUTAKI KATIBA MPYA TUENDELEE NA YA ZAMANI in maana hadi baada ya miaka 50.Tukipiga YES maana yake KATIBA YA KIKWETE itakubalika.hapo ni kulia na kusaga meno.KAZI KWETU
 
Mkuu uporoto kuna kitu nataka ujue,tukikosea step tukakubali kura ipigwe tumekwisha lazima watashinda,hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindanna na ccm tunapoongea mambo ya kura,ni wazoefu wa kuchakachua,hilo siafiki hata kidogo
mimi mwenyewe sikubali kura ipigwe na kama ikipigwa isimamiwe na nani? Mbona imezoeleka kila siku tunachagua nyekundu tunaletewa kijani
 
Mchakato huu hauna tofauti na mbuni aliyeficha kichwa chake shimoni hali mwili wote uko nje. Bunge limetumika kupitisha uozo mwingi sana wa serikali ya CCM, matokeo yake tunayajua. Hatujakoma tunazidi kufanya madudu yaleyale, na matokeo yatakuwa yaleyale. Mchakato mbovu, utazaa kamati mbovu, itakayokusanya maoni na kurudisha ripoti mbovu, itapelekwa kwenye bunge la katiba bovu, lenye idadi kubwa ya wawakilishi walioanzisha mchakato mbovu, watapitisha rasimu ya katiba mbovu, kwenda kupigiwa kura ya maoni itakayosimamiwa na tume mbovu. KATIBA ITAKUWA MBOVU
nimeipenda hii, saluti mkuu!
 
Mimi namwamini sana Dr.Slaa na uongozi wake, naamini hawatakubali lakini kama watakubali tukae kimya na kukubali tuende kwenye kura mimi nitakuwa wa kwanza kuwa mkimbizi na kuomba hifadhi Rwanda kwa kagame, najua watanipokea kwani wao tuliwahi kuwapokea kama wakimbizi.
 
Mkuu uporoto kuna kitu nataka ujue,tukikosea step tukakubali kura ipigwe tumekwisha lazima watashinda,hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindanna na ccm tunapoongea mambo ya kura,ni wazoefu wa kuchakachua,hilo siafiki hata kidogo

kwani hawatachakachua?
 
REVOLUTIONALISTS NEVER GIVE UP NO MATTER WHAT.Movement ya kuipinga hiyo rasimu ili isipite ni muhimu iwekewe mikakati ya kutosha kuanzia sasa.ALUTA CONTINUA.
 
dawa ni maandamano bila hivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
 
Ni upuuzi kutufanya sisi wachache ni wapuuzi wakati uwingi wenu unaimarisha uppuzi pia,nani mnaendanganya kama mtoto,nani mwenye uelewa japo mdogo yuko tayari kwenda kwenye hatua ya upiga kura wakati upigaji wa kura utasimamiwa na NEC ya ikulu.hivi mnadhani tumerogwa au tumechanganyikiwa wengine tunaosema wazi ya kwamba huu ni wakati muafaka wa kuingia barabarani kudai katiba ya watanzania?leo mmepitisha mswada ili baadae mtoe katiba ya CCM mlete katiba ya IKULU.No way.Tutaidai haki hii mpaka kwenye vibanda vyenu,msinajifanya viziwi na vipofu pia?
 
Back
Top Bottom