Msishangae CCM ikishinda Arumeru Mashariki

Mkuu, hizo njano na kijani ulizivalia mitaa gani? kumbuka siyo asilimia 60 walioshangilia, pia kumbuka katiba yetu iliyopo hairuhusu kupinga matokeo sehemu yeyote ile, iwe mahakamani au kuandamana.
mbinu yao mojawapo ni kuwachaganya wapiga kura ili wizi wa kura uwe mrahisi. Mf wapiga kura kutoona majina yao kwenye vituo vyao vya kupigia kura. Haijalishi ccm imeshindwa kwenye kura lakini watamtangaza mgombea wao kwa nguvu. Ndipo hapo wengine roho zinawauma zaidi
 
Kudhani kuwa Slaa alishinda 2010 ni upumbavu usiokuwa na mfano. Kama mtu anayejiita great thinker anaweza kuwa na fikra hii, sishangai kwanini CCM inashinda miaka yote!
Mkuu lugha yako inashangaza sana. Tupo ambao wala hatudhani kuna aliyeshinda kabisa. Unadhani mwenye akili timamu na aliyeelimika anaweza kudai kuwa kuna aliyeshinda? Atakuwa anatumia vigezo vya kihuni awaye yeyote atakayedhani amependwa na kuchaguliwa na Watanzania kuiongoza nchi katika uchaguzi wa 2010.
Kama unaakili timamu na umeelimika hutakubali kachaguliwa na pasenti ndogo namna ile ya Wantazania na zaidi ya hapo jinsi ambavyo matokeo yalicheleweshwa, na wananchi wengi zaidi waliojiandikisha kushindwa kupiga kura kwa sababu zisizoelezeka. Ungefahamu jambo hilo lilivyo kielelezo na sababu za wazi zinazoletea kuathirika kwa uchumi wa nchi yetu, kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara nk. usingetamka maneno hafifu namna hiyo. Lugha yako unaonekana ni kati ya wale waliokanyaga ndani ya bakuli la uji baada ya kushiba sana. Nadhani na ulimbukeni unachangia. Pole sana. Kwa kifupi fahamu kuwa mpaka sasa Tanzania haijawahi kupata bahati ya kuwa na demokrasia ya kweli, wala uchaguzi wa raisi ulio huru wala wa haki. Wote uliopita ni ulaghai mtupu, uchafu, ushenzi, uhuni na uuwaji wa Taifa zima. Inasikitisha kusikia kuna mtanzania wa leo anayeamini kuwa ameshakuwa na raisi aliyechaguliwa na wananchi kupitia demokrasia ya kweli.
 
Ccm haiwezi shinda huko,nadhani umeandika haya ukiwa mwanakwerekwe.2po meru sisi
 
CDM walianza hivi hivi Igunga lakini mwisho wake tumeuona. Ni kawaida yao humu JF, mkwara mzito wakati wao wenyewe hawana hata kadi za CDM.
 
Tutashinda kwa kishindo namaanisha CCM!!!!

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Binafsi nitashangaa sana ccm wakishinda maana hawakubaliki kabisa huko!
 
Back
Top Bottom