Machozi ya Mwita Waitara (Mb) Vs Ubabe wa RC Mzee: Hitajio la Busara za Rais Samia Suhuhu

Chipoku

JF-Expert Member
May 19, 2011
254
181
Machozi ya waitara,ubabe wa

Julius Marwa

Tarime - Mara


Bila shaka yanayoendelea mkoani mara wilayani tarime kata ya nanyungu si ya kuachwa na kutazamwa yapite bali busara za mama zinahitajika haraka

Labda niwakumbushe kidogo watanzania wenzangu eneo hili lenye mgogoro ni eneo muhimu na la kimkakati kwa taifa lakini ni eneo tegemeo kwa jamii inayoishi hapo hasa kwenye kulisha na kunywesha mifugo yao.

Ni eneo ambalo siku za karibuni limekuwa ni uwanja wa vita kati ya wananchi na tanapa

Askari wa tanapa wanapoteza maisha na wananchi na mifugo yao ikipotea pia. Hivi karibuni imeripotiwa kuwa askari mmoja wa tanapa aliuwawa kwa kuchomwa mshale wa sumu na baadae wananchi tisa (9) wameripotiwa kupotea huku mamia ya ng’ombe pia wakiripotiwa kupigwa risasi.

Wakati eneo hili upande wa tanzania limekuwa ni uwanja wa vita upande wa pili kwa jirani zetu kenya eneo hili limekuwa ni neema kubwa kwa utalii,taifa hili jirani likinufaika kiuchumi kwa uwepo mbuga maarufu ya masai mara na pengine hili ndipo jambo ambalo linawafanya tanapa kuhisi hawataimzi majukumu yao lakini kosa kubwa linalofanywa hapa ni matumizi makubwa ya nguvu na vitisho dhidi ya wananchi hawa

Mkuu wa mkoa dhidi ya chama cha mapinduzi .

Mkuu wa mkoa amekuwa anatisha viongozi wa chama cha mapinduzi,diwani na mbunge wa eneo husika

Ni juzi tu mwenyekiti wa wazazi taifa amekipongeza chama cha mapinduzi wilaya ya tarime na chini ya mwenyekiti wake komredi ngicho kutaka mwenyekiti wa chama hicho wilaya komrade ngicho na mwenzie wa mkoa komrade chandi waachwe wafanye kazi,hata wiki mbili hazijapita mkuu wa mkoa tena kwa vitisho vikubwa anamvaa komrade ngicho tena kwa vitisho na dharau kuwa hatamheshimu na atapambana nae.Bila shaka hii ni vita kati ya mkuu wa mkoa na ccm wilaya ya tarime na mkoa wa mara

Mkuu wa mkoa na dhana ya kushushwa cheo” demotion “

Tarehe 17 februari 2023, katika kikao alichoitisha mkuu wa mkoa kujadili maendeleo na mambo muhimu ya mkoa pamoja nae na wabunge wa mkoa huu mkuu wa mkoa anasisitiza yeye si mwanasiasa na uwepo wake hapo ni matokeo ya kushushwa cheo na raisi samia

Hili ni jambo la kushangaza mno kwa mteule wa raisi kusema haya hadharani bila shaka lipo jambo nyuma ya haya yote

Vita yake dhidi ya mbunge Waitara na diwani Richard Tiboche wa kata ya Nanyungu

Kote duniani chama hubaki na wananchi hata kama kwa kuwapa matumaini ambayo hayapo na ni chama ndio chenye kazi ya kuikosoa na kuirekebisha serikali inapokosea. Dhana hii imekuwa ngumu kueleweka kwa mteule wa raisi mkuu wa mkoa ambaye sio tu hataki kuwasikiliza na kuwapa nafasi wananchi amekuwa akitumia nguvu kubwa na vitisho dhidi ya wananchi na wawakilishi wao (diwani na mbunge) na sasa chama tawala

Hatari ya ccm kuyakosa majimbo yote ya uchaguzi tarime

Tarime kuna changamoto nyingi zinasosababishwa na watendaji wa serikali kuanzia mkurugenzi anayechelewesha miradi na DAS mwenyenguvu kubwa inayotokana na kukaa hapo muda mrefu na migogoro lukuki inayoshindwa kutatuliwa na wateule wa raisi licha ya raisi samia kupeleka pesa nyingi za miradi

Eneo maarufu la lebu sokoni ambapo wananchi walalahoi walikuwa wakilitumia kuuza ndizi zao halipo tena na wajanja wenye nguvu kiuchumi wamelichukua na hakuna wa kuwatetea wananchi hawa ambao hawana sehemu ya kuuza bidhaaa zao tena,mkurugenzi na maafisa wake ardhi na sheria nao wamekuwa sehemu ya tatizo na kuchagua upande wa waporaji wa eneo hili.Yuko wapi mkuu wa mkoa katika hili?Hapa angalau mbunge wa tarime mjini bw kimbaki anonekana akiangaika na wananchi mara mahakamani mara kule

Yuko wapi mkuu wa mkoa kwenye kuwatetea wananchi wa nyamongo wenye kusaidia fidia dhidi ya mgodi wa north mara,

Mambo kama haya ndio agenda za wapinzania kwenye majimbo haya ambazo ndio zitakofanya chama tawala kipoteze majimbo haya kama busara za raisi samia hazitatumika sasa

Waitara kama mbunge wa kupigiwa mfano

(machozi yake yana maana pana kwa siasa za tarime)

Kwa wasiomjua mh waitara ambaye ni mbunge wa tarime vijiji ni mtu wa hisia mno hasa linapokuja suala nyeti la kupigania wananchi wake ni kawaida yake kutoa machozi kwa hisia mara nyingi inapoanza mijadala ya maslahi ya jimbo lake(nimeona hii mara kadhaa kwenye mijadala baina yetu).

Machozi kwa mheshimiwa ni njia ya kuondoa maumivu ya hisia za uonevu kwa wananchi wake.

Kwa anayezijua siasa za tarime ambazo ni siasa za kikabila na kikoo “ethnopolitic “ mh waitara amekuwa ni alama ya uimara wa chama tawala eneo hilo na hili limeongezeka baada ya hivi karibuni wazee wa kabila la wakulya kumtawaza kuwa chifu wa wakulya eneo hili.

Si busara hata kidogo kwa mkuu wa mkoa kutoyaona na kuyaheshimu haya kwenye eneo lenye siasa za namna hii

Kwa nini busara za raisi samia zinahitajika sasa tarime na mkoa wa mara

Busara za raisi samia zinahitajika kwa kuwa eneo hili ndilo eneo pekee nchini ambalo uchaguzi huwa ni vita baina ya ccm na chadema na kuna kila dalili haya kutokea 2025 kwa namna mambo yanavyokwenda

Kila wananchi wanapohojiwa na vyombo vya habari huwa wanaomba mama aingilie kati yanayojii katika eneo hili

Eneo la tarime ni mpaka muhimu kati yetu na kenya na siasa za tarime zinaathiliwa sana na siasa za kenya hapa kuna mpaka wa kimkakati wa silali utulivu wa eneo hili ni utulifu wa tanzania

Uwepo wa kundi kubwa ambalo ni matokeo ya uchaguzi wa ndani wa ccm ambalo bila kupepesa macho halina na halikubaliani na matokeo ya chaguzi za ndani za ccm na kumpinga wazi raisi samia ni nukta nyengine muhimu kuonyesha umuhimu wa busara za raisi samia

Wafadhili wengi wa chama na wadau wakubwa wa maendeleo wamekuwa wahanga wa maamuzi ya wakuu wa wilaya na mko waliopota hasa mh malima na dc luoga (rejea yaliyomkuta mafanyabiashara peter zakari) ambaye licha ya madhira na majanga aliyopitia bado amekuwa msaada mkubwa kwa chama eneo lote la kanda ya ziwa na kutokana na umuhimu wa eneo hili kwenye siasa za 2025 ni muhimu busara za raisi samia ziwatambue hawa na angalau kupongeza kwa kuendelea kukiunga mkono ccm maana wasaidizi wake waneshindwa kufanya hilo

Ipo dhana maarufu tarime iliyoenea sana kuwa waitara hapendwi ccm hq chini ya mwenyekiti wake ccm ndio maana alitolewa baraza la mawaziri na hawezi kupewa fursa hii 2025

Ni vyema dhana kama hizi au mfano wake zifutwe na busara za mh raisi samia

Kwa kumbukumbu tu mh waitara kwa muda mrefu kabla ya kuwa mbunge amekuwa afisa chini ya katibu mkuu wa chadema wakati huu dr w. Slaa akiongoza kikosi kazi kidogo cha tafiti na matokeo ya tafiti hizi yaliyopelelea ushindi mkubwa wa majimboni wa chama hicho ni mwalimu kwa taaluma anayejua nini anafanya kwenye siasa za tanzania.

Madudu mengi ya tarime na mkoa wa mara yanafanya hitajio la busara la raisi samia wakati huu

Kuanzia soko la matunda la afrika mashariki ambalo kwa sasa ni banda la miti tu,mnada wa mifugo afrika mashariki ambao licha ya kupelekewa mamilioni ya pesa kuna kijumba cha afisa mifugo na ng’ombe wake nane wa maziwa huku yeye akiwa hana kazi hapo (yote haya yanakosesha serikali yetu mabilioni ya pesa)

Hatari zaidi ni uwanja wa ndege wa tarime ambao ukiacha umuhimu wake kutokana na utalii na ujirani na kenya ni pori na ndege hutua na kuandoka bila hata kuchunguzwa imeleta na kubeba nini jambo hatari kwa usalama wa eneo hilo la mpakani.

Ndio maana tunasema kati kati ya machozi ya waitara na ubabe wa meja jenerali mzee mkuu wa mkoa wa mara kunahitajika busara za raisi samia ili siasa za tarime na mkoa wa mara zisiwe dhidi ya ccm 2025
 
Waitara, usipoteze muda na fedha kwa Jimbo Hilo, tunza hizo Hela zitakusaidia baada ya 2025. Fungua biashara, anzisha kilimo. Wale jamaa wanacheza ngoma sebuleni kwako.
 
Wakurya hatuna chifu mura, huyo Waitara ni chifu wenu wala sio wakurya wote, lakini hili suala la Nyanungu busara inahitajika.
 
Tatizo la makala yako umechanganya mambo mawili. Siasa za Tarime na mioaka ya mbuga ya serengeti.
Ungejielekeza kwenye mipaka inayowekwa ya kutofautisha mbuga na maeneo ya wananchi na uhalalai wake.
Umechanganya mambo sana. Tarime ni sehemu ya nchi. Taratibu lazima zifuatwe.
 
Mwita amesema mazingira anayoona hawezi kushinda uchaguzi ndiyo akaanza kulia.
Kinachomliza ni uchu wa madaraka.
04EE8A00-0125-4732-B007-89830D44AE0E.jpeg
 
Natamani Mhe Rais asimsikilize huyu Mjinga na Genge lake ambao wameshagundua RC aliyepo sio mtu wa kubembeleza mtu. Kiukweli Mkoa wa Mara hauhitaji Kiongozi mwenye Siasa nyingi. Mkoa Ule unahitaji Kichwa cha Moto kama wenyeji wenyewe walivyo na vichwa vya Moto.

Utakumbuka hata Waitara Mwenyewe akiwa Chadema jinsi Kichwa Chake kilivyokuwa na nishati ya Makaa ya mate, yaani alikuwa Pasua Kichwa hasa. Baada ya kukaribishwa ccm ndio ikalazimu aishi maisha ya wenyeji wake , ailichukuwa msemo ule wa " unapoingia Vatican basi huna budi kuishi maisha uliyoyakuta Vatican ".

Watu ni wajanja sana, yaani hata uwe mtendaji Mzuri kiasi gani , wakiona unakwamisha mambo yao binafsi wanakutengenezea zengwe na linakolezwa na wanahabari, mara Bungeni na mwisho mamlaka za uteuzi zinaona aaah!! Ngoja tumuondoshe yule pale. NAKUMBUKA ISSUE YA YULE MJESHI PALE MSD. Ukiona msd kumetulia kwasasa usifikirie kuwa ndio hakuna Makandokando, Laahasha ni Kwamba NETWORK INASOMA VEMA.

Hata huyu RC alipokuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza ameleta nidhamu na Mabadiliko Makubwa sana pale hasa ya uzalishaji na jeshi hilo kufikia hatua ya kuanza kujilisha, lakini unapofika sehemu na kuwabana watu waliozoea mambo yao na kuziba upigaji kwa 100% hapo utatoka tu. Huyu RC hadi leo Askari wa vyeo vya kati na chini wanamkumbuka sana
 
Back
Top Bottom