Msishangae CCM ikishinda Arumeru Mashariki

CCM ina nafasi kubwa ya ushindi kwa sababu CHADEMA wameingia kwenye uchaguzi huo bila kudai kuboreshwa daftari la NEC la wapiga kura!Kumbuka vijana waliokuwa na miaka 16 mwaka 2010 sasa wana miaka 18 na wangekuwa na haki ya kupiga kura,na inajulikana kuwa vijana ni wafuasi wa upinzani kwa hiyo bila kuwaandikisha hawa upinzani umezikosa kura maelfu za vijana!

CCM wao wanajivunia base yao ya wazee na wanawake wasiopenda mabadiliko;na tukumbekeni kuwa ngome yao ya wapiga kura haijatingishwa na kitachaofanyika sasa ni kuwabadili tu mawazo toka kwa Sumari marehemu kuja kwa mtoto wake na kama Lowassa ataweka mkono wake wa pesa jimbo kiurahisi kabisa linarudi CCM

Sijajua hadi leo kwa nn CHADEMA hawajapigia kelele NEC kuhusu kuandikishwa kwa wapiga kura waliofikisha umri kabla ya uchaguzi huu ila najua April baada ya matokeo ndiyo watalizungumzia suala hili!
 
naomba nikukosoe kidogo kua...chadema inaweza kushinda arumeru ila cccm wakachukua/kutangazwa washindi. ipo tofauti kati ya aliyeshinda na aliechukua jimbo au kutangazwa mshindi kutokana na mizengwe ya chaguzi zetu. tafakari
 
KUSHINDA NI KUSHINDA TUU,UNAWEZAJE KUSEMA KUWA CHADEMA WALISHINDA IGUNGA WAKATI MTU WA KWANZA KUTANGAZA KUWA CCM IMESHINDA ALIKUWA ZITTO ZUBERI KABWE??

HATA KABLA TUME HAIJATANGAZA NANI KASINDA IGUNGA ZITTO ALISEMA KWENYE TWITER YAKE """We have lost the election. Chadema conceded NOT. Contemplates petition"""

IKUMBUKWE HII ILIKUWA KABLA YA TUME KUTANGAZA MATOKEO.SASA MKISEMA CCM ILIIBA KURA IGUNGA INASHANGAZA,ILA NI KWELI KWAMBA WATZ WANAFANYA MAAMUZI MABAYA MARA NYINGI NA HII HAITAKUWA MARA YA KWANZA WAKIFANYA HIVYO ARUMERU EAST
 
MImi nitashangaa zaidi CHADEMA ikishinda. Historia, MiundoMbinu, itifaki na mazingira hayako upande wa CHADEMA. AruMeru ni ya CCM(L) hata bila kutumia misuli na mitulinga. Marafiki zangu Wameru hapa Dar wako kwenye maandalizi ya kumpongeza Siyoi mapema mwezi ujao. Kazi kubwa kwao ni ile iloisha jana. CC ya akina Nape, Chiligati, Msekwa,...,imenasa.
 
Kudhani kuwa Slaa alishinda 2010 ni upumbavu usiokuwa na mfano. Kama mtu anayejiita great thinker anaweza kuwa na fikra hii, sishangai kwanini CCM inashinda miaka yote!
 
Unakusea sana kuwalaumu wa tanzania.

Watanzania huwa hawafanyi kosa sanaaa.

Heko kubwa na bao la ushindi wafungalo ccm dhidi ya wapinzani ni kuiba kura.Wakishilikiana kwa karibu sana na hawa chui wavaao ngozi ya kondoo si wengine ni usalama wa taifa..

Kama huko arumeru watawakamata koo mpaka mwisho kuhakikisha hawapati mwanya wa kuiba kura hakika tutarajie maajabu makubwa.

Heko nyingine na bao la dochi walifungalo ccm ni umasikini wa watanzania.
Asilimia kubwa na wafuasi wakubwa wa ccm ni wale watanzania wa kipato cha chin.
Ambao hukubali kulubuniwa na pombe za kienyeji,vyakula,nyama choma,mashati,t-shirt,kapero ,kanga na skaf,vitambaa
na kuhongwa vijisent vidogo ili waipigie kura ccm.

pamoja na yote hayo,ila siku zote nitasema Watanzania walio wengi ambao wamechoshwa na dhahama hizi za maisha wanafikiri siku zote kuhusu kuibiwa kura,ILA WENYEWE HAJITOKEZI KUPIGA KURA KWA MAWAZO HAYAHAYA...tubadilike ni
vigum sana kuiba kura zaidi ya milioni 10...Hata kama zitaibwa lakini si kwa kiwango hicho,hilo ni suala ambalo inabidi watu hasa vijana wabadilike.Pia vijana wengi huona kupiga kura ni kumpa mwenzako ulaji,dhana potofu
 
chadema chadema chadema,

msijipe moyo kuwa mtashinda arumeru mashariki,watanzania ni watu wa ajabu sana,labda niwakumbushe kidogo wakati kashfa kuu kwa serikali ya richmond kulikuwa na uchaguzi wa ubunge tunduma na ccm yenye kashfa ikashinda,tukiwa kwenye hali mbaya kiuchumi,kisiasa na kashfa kede uchaguzi mkuu 2010 watanzania walimchagua jk na ccm yake kwa zaidi ya asilimia 60,juzi juzi igunga pamoja na matatizo yote waliyonayo magamba bado watanzania wakaichagua ccm,uzini nayo mmejionea,watanzania watanzania watanzania ni nani awakomboe.ndugu zangu siwakatishi tamaa ila msishangae ccm ikiibuka na ushindi mnono arumeru mashariki wananchi wa tanzania ndivyo walivyo bado hawako tayari kukombolewa.

Kwa hiyo wewe unakubali kabla ya kupambana kushindwa huku ukidanganya kwamba hukatishi watu tamaa: hii nchi itabidi tuanze kupigana viboko ili tujikomboe,unatoa lugha laini huku unahalarisha ushindi wa CCM kabla ya kura ,wewe hukuona wala kufuatilia nini kilitokea Igunga,unabariki matumizi ya dola kusaidia CCm,unabariki mauaji kubariki ushindi wwa CCM ,unabariki propaganda za kidini ,kwa kweli safari ni ndefu ya ukombozi ,acha hiyo wallugha ya mzunguko, kuhalalisha zambi ya CCM nadhani tuwape moyo wananchi wa arumeru wachague mbunge wanayemtaka kwa haki
 
Nimekushusha sana CV kwa kusema eti JK alishinda 2010.Mental ill

Yani wewe kijana unashangaza kweli wakati viongozi wako wa CDM wanatambua kama JK alishinda na ni Raisi wao wewe mfuasi usiyejua CDM ilipotoka na inapokwenda hutaki kukubali ushindi wa JK kweli wewe ni kilaza!
 
KUSHINDA NI KUSHINDA TUU,UNAWEZAJE KUSEMA KUWA CHADEMA WALISHINDA IGUNGA WAKATI MTU WA KWANZA KUTANGAZA KUWA CCM IMESHINDA ALIKUWA ZITTO ZUBERI KABWE??

HATA KABLA TUME HAIJATANGAZA NANI KASINDA IGUNGA ZITTO ALISEMA KWENYE TWITER YAKE """We have lost the election. Chadema conceded NOT. Contemplates petition"""

IKUMBUKWE HII ILIKUWA KABLA YA TUME KUTANGAZA MATOKEO.SASA MKISEMA CCM ILIIBA KURA IGUNGA INASHANGAZA,ILA NI KWELI KWAMBA WATZ WANAFANYA MAAMUZI MABAYA MARA NYINGI NA HII HAITAKUWA MARA YA KWANZA WAKIFANYA HIVYO ARUMERU EAST
Mkuu ninaishi igunga, ccm walimwaga pesa mpaka basi, si takukukuru wala nani ambaye angeweza kuwazuia maana walitapakaa jimbo zima kama nzige wakagawa pesa hadi kwa wachumgaji, shahada zikanunuliwa, tisheti, kanga, kofia na vitambaa vikakasambazwa, zakaingia na propaganda za akina wasila, magufuri na wengine, selikari ikaamia igunga, polic nayo ikacheza nafasi yake ikishirikiana na ccm. Ikumbukwe tume na msajiri zote ni organ za ccm Tendwa ameanza mmemuona. Kwa maana hiyo nakubaliana na mleta mada kwa move hizo ccm ina nafac kubwa ya kushinda.
 
CCM watashinda kwa kuiba kura na kutumia nguvu ya dola. Nje ya hapo hakuna kitu. Na pia itafika mwisho tu kwa udhalimu wao.
 
Mkuu ninaishi igunga, ccm walimwaga pesa mpaka basi, si takukukuru wala nani ambaye angeweza kuwazuia maana walitapakaa jimbo zima kama nzige wakagawa pesa hadi kwa wachumgaji, shahada zikanunuliwa, tisheti, kanga, kofia na vitambaa vikakasambazwa, zakaingia na propaganda za akina wasila, magufuri na wengine, selikari ikaamia igunga, polic nayo ikacheza nafasi yake ikishirikiana na ccm. Ikumbukwe tume na msajiri zote ni organ za ccm Tendwa ameanza mmemuona. Kwa maana hiyo nakubaliana na mleta mada kwa move hizo ccm ina nafac kubwa ya kushinda.

mwenye nguvu ndo anakula mzigo
 
Mkuu nilipoisoma thread yako kabla ya kuifungua nilikuwa tayari nimeandaa nondo kali ya kukuponda nayo..umeninyong'onyeza...Ni kweli mi-tanzania ni ya ajabu sana...uwa haitazamani mbele,ikipewa wali maharage inasahau shida zote.Ila kwa Arumeru nawaombea pepo huyo ashindwe kwa jina la Yesu.
 
CCM itashinda Arumeru. hii nasikitika kusema. Chama hiki hushinda by election nyingi ukiondoa ule wa Temeke wa Mrema.
Kundi la Membe, ambako mtu wake Sarakikya alitoswa, halina nguvu ya kumvuruga mkwe wa Lowassa.
Chadema wana nguvu, ila vijiji vya ndani haviwajui sana
 
...sitashangaa ccm ikishinda kwa sababu nia yao ni kushinda. Na kushinda kwao ni vyovyote inavyowezekana. Pia wana-ccm huwa hawaachi kupiga kura ukilinganisha wanachama wa vyama vingine ambao hubaki kushabikia bila kutenda. Mwisho wa siku inasemekana kuna wizi wakati mazingira ya mchezo yanafahamika.
...tutabaki kusema uwanja umejaa maji, ooh baridi, eeh wanabebwa japo hatukatai kucheza nao na mwisho twafungwa sie.
...vijana wa Arumeru wakilala, wazee watatumia uzoefu wao wa kuchagua na hawatamtupa "mzee mwenzao" ccm.
 
Dalili ya mvua mawingu.

Magwanda wanapojijuwa kuwa hawashindi huwa wanaanza visingizio kila namna.

Hivi kiuhalisia haswaa, ni magwanda gani anaesema mtashinda Arumeru?

Magwanda walikuwa wanaomba Mungu Sioi asigombee, wanajuwa huyo akigombea wao wamekwisha.
 
Back
Top Bottom