Msiba: WoS afiwa na babake

Waungwana,

Nachukua nafasi hii kuwataarifu msiba mkubwa uliomfika mwenzetu, Woman of substance, wa kufiwa na Baba yake mpendwa. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN na pia awape nguvu, subira na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao. Pole sana kwa msiba mkubwa WOS.

WoS

Pole sn kwa msiba uliokufika. Mwenyezimungu akupe moyo wa subra na uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu cha majonzi kwako na ndugu zako kwa kuondokewa na mpendwa wenu.

Hiyo ni njia wote tunaifuata, muhimu kujiandaa kwa mazuri.

Thnx
 
Pole sana Women pamoja na wanafamilia wote kwa msiba uliowapata.
 
Hakuna pole inayoweza kupoza machungu uliyonayo WOS, lakini kama binadamu, tunawajibika kukupa pole kwa msiba huu mkubwa, Mungu atakuwa pamoja nawe
 
Pole sana WOS,
Mungu awatie nguvu wote walio guswa na msiba huu katka kipindi hiki cha majonzi.
 
Nawashukuru nyote kwa salamu za rambi rambi kwa mwenzetu, kufanya hivyo hakumrudishi marehemu aliyetutoka lakini inamsaidia mwenzetu kukabiliana na msiba huu mkubwa uliowafika yeye na familia yake. Ahsanteni sana.
 
Pole sana WOS.
Mungu alitoa na Mungu ametwaa. Awapeni nguvu za kuhimili kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpenzi wenu, Amen.
 
WoS, pole sana kwa msiba wa Baba, tunamuomba Mola awape nguvu, subira na imani wakati huu na baada ya maombolezo. "Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake tutarejea...".
 
Poleni sana familia nzima na msiba huu mkubwa, ninamwomba Mungu faraja na uponyaji wake wakati huu wa machozi na majonzi. Pia namwombea Mungu huruma na rehema kwa roho ya marehemu ili apumzike kwa amani milele. Amina.
 
Waungwana,

Nachukua nafasi hii kuwataarifu msiba mkubwa uliomfika mwenzetu, Woman of substance, wa kufiwa na Baba yake mpendwa. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN na pia awape nguvu, subira na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao. Pole sana kwa msiba mkubwa WOS.

Poleni sana kwa msiba mzito!
 
Pole sana dada Mungu akutie nguvu na akupe faraja katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na mpendwa wako!
 
I.L.W.I.I.R Naungana na wengine kukupa pole WoS kwa kuondokewa na nguzo muhimu katika maisha. Mungu akujaalie wepesi wa kulikabili jambo hili zito. Ameen.
 
Pole sana WoS.
Naamini Mwenyezi atawapa nguvu na faraja katika wakati huu mgumu. Na sisi wote, kwa imani zetu kila mmoja wetu, tutakuwa nanyi katika majonzi yenu.
Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu. Amen.

Fundi Mchundo
 
Last edited:
Back
Top Bottom