Msiba: WoS afiwa na babake

Our Dearest WOS,
Tumuombee mungu mpendwa wetu alale mahala pema peponi na muumba wetu amjalie kila la kheri katika makazi yake mapya.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LITUKUZWE!
 
Mungu ailize mahali pema peponi...roho ya marehemu.Tuko pamoja katika wakati huu mgumu...
 
WoS umepoteza kitu kikubwa mno katika maisha yako. Jipe wakati huu mgumu na Mola atakusaidia kukabiliana na hili.
Pole sana Wos.
 
Pole WOS. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. Mungu awatie nguvu kwa kipindi hiki kigumu cha majonzi kwa kufiwa na baba mzazi.
 
Raha ya Milele umpe ee Bwana, na Mwanga wa Milele umwangazie, Apumzike kwa Amani. Amina
 
Pole sana WoS na wafiwa wote. Mpendwa wenu mlimpenda sana lakini Mungu amempenda zaidi. Mungu aiweke roho yake pema peponi.

Amen
 
Pole sana Dada WoS, Mungu akutie nguvu wewe na jamii yako na kuwafariji kwa faraja yake ipitayo faraja zote.
 
Pole sana Woman of Substance. Msiba wa Mzazi ni mgumu sana. Nakuombea wewe na familia yako, kwa Mwenyezi Mungu mpate nguvu za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu.

Njia pekee ya kufika kwenye uzima wa milele ndio hiyo. Sisi wote ni wasafiri katika njia hiyo.

Mungu ailaze roho ya marehemu Baba yetu mahali pema peponi. Amen
 
Wapendwa wana JF
Awali ya yote napenda kuwasalimu kwa jina la upendo , amani na mshikamano. Aidha nimefarijika na kuguswa sana na moyo wenu wa undugu na mshikamano mliouonyesha kwangu mimi binafsi na hata familia yangu katika kipindi kigumu cha msiba wa mzazi wangu. Nimejiona nina ndugu zaidi ya wale nilio na nasaba nao maana sikutegemea kabisa kwamba JF ingeweza kuwa ni mtandao wa kuendeleza pia undugu over and above kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi na kijamii bila kusahau burudani.

Najiona nimebarikiwa kwa namna ya pekee kukutana na nyie wote katika hili jamvi na ninamuomba mwenyezi mweza wa yote awabariki na kuwazidishia afya na mafanikio katika kila mfanyacho. Napenda kutambua kila mmoja aliyenipa pole au kunitumia salamu za rambirambi kupitia PM na hata E-mail kama ifuatavyo: Kwanza kabisa Bubu Ataka Kusema aliyeujulisha umma wa JF kuhusu tukio,halafu wanaJF walioguswa na kunitumia pole – QM, GM, Next Level, Gamba la Nyoka, Kuntakinte, Kifimbocheza; bila kuwasahau Masanilo, BabaDesi, Morani75, ThinkPad, mdau, Nyani Ngabu, Zakumi, Masanja Hofstede, Dark City, jujuman, BelindaJacob, Shy. Nimefarijika kumsikia Aljuniortz ambaye sikumbuki kukutana naye hapa JF lakini kwa moyo wa upendo amenifariji; Siwezi kuwasahau Koba, Ogah, August, Mtindiowaubongo, Mpita Njia, Rwabugiri, Jasusi, Shadow, Mfumwa, Sura-ya-Kwanza, Nziku, Mzalendohalisi, Mzee Mwanakijiji, Kipunguni Amelie, Kweli, Kaka K, Fundi Mchundo, Bibie, na Pasco. Nitakuwa mtovu wa shukrani kama nitaacha kuwataja wakuu kama Mwawado, kafara, Yo Yo, Sober, Kaizer, Mwakilishi, Pundamilia07, Lunanilo, Kibunango, Phillemon Mikael, MwalimuZawadi, Uwiano Maalum, Field Marshall ES, JokaKuu, MaxShimba, Kichuguu, FairPlayer jmushi1, Kijunjwe, Buswelu Tuipendeinchiyetu, Roya Roy, Maane, Ndege ya Uchumi, Jitume, Ibrah Recta na Ngorunde.Nawashukuru pia edwinito, Baba_Enock na wale wote ambao nitakuwa nimepitiwa kuwataja.
Asanteni sana!
WoS
 
Tunakushukuru WOS kama faraja hii imekuliwaza ktk kipindi hiki kigumu. Mungu aendelee kuwapa faraja. Kuondokewa ni kugumu lakini marafiki kama wa JF na wengine husaidia sana kupita ktk vipindi hivi.
Bwana ametoa, bwana ametwaa.Daima ahimidiwe.
 
Pole sana WoS pamoja na familia kwa ujumla. Mwenyezi Mungu aendelee kukupeni faraja na nguvu ya kustahimili majonzi katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole Sana WoS. Ni Maombi Yangu Kwa Mwenyezi Mungu Aiweke Pahali Pema Peponi Roho Ya Marehemu Baba Yako Na Kuwapa Amani Na Matumaini Wanafamilia Wote Katika Kipindi Hiki Kigumu Kwenu. Amina.

SteveD.
 
Pole Sana WoS na familia yako kwa kufiwa na mzazi. Ni msiba mzito sana.
Mungu ailaze roho ya baba mpendwa mahali pema paponi. Amina.
 
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAAA JINA LAKE LIBARIKIWE...POLE SANA WoS NA MUNGU AWAPE FARAJA.
 
WoS
Pole sana wewe na familia nzima kwa MSIBA huu mkubwa.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana LIHIMIDIWE - AMEN
 
Back
Top Bottom