Mshindi wa BSS Pascal Cassian AMEFULIA MBAYA

khaaaaaaa ila pesa ambayo hukuitarajia ndo ujinga wake huu
sasa mke alimtelekeza kisa
pumbav sasa atakiona cha mtema kuni
bora angemlea mkewe amfungulie haata kamaradi wangelumbangia hata dagaa na kachumba life lingesonga
sa kamkimbia wacha dunia imcharaze bakora atarudi tu amuulize lucas mkenda ,mbwembwe zilimfanya kiislam mpaka leo anahaha kurudi alipokuwa lakini waaapi imebaki store"
 
Asante mkuu kwa kutujuza japo watu wengine hapa wameponda,kwa kweli hilo ni fundisho na ni somo kwa wale wanaolamba bingo na kuona kama ndio maisha yameanza,kwa nini huyu jamaa hakuendeleza fani yake ya muziki aingie mkataba na makampuni mbalimbali manake ushindi wake ulimtangaza ndani na nje.
Umesema alikua anakodisha taxi kutoka MAGU to Mwanza kisa ATM ambazo zipo MAGU?shule ameenda kweli huyu jamaa?

kakomea Standad SEVEN
 
Yule mshindi wa shindano la Bongo star search (BSS) mwaka 2009, PASCAL CASSIANO
kwa sasa Account yake imeisha na kubakiza hela ya kitabu tu (kama Tsh. 3000), watu wa karibu wa msanii huyo wamedai kuwa dogo huyo zile pesa alizopata zimemponza coz jamaa alipotoka Dar na kuja kwao MAGU, Alifikia hoteli moja inaiTwa TINSELA HOTEL, cha ajabu Mama yake mzazi alipataka kwenda kumsalimia pale hotelini yule Mama alizuiliwa na kuambiwa hawezi kumuona Super star, kwa muda huo na ndipo mama huyo akaamua kurudi nyumbani mikono nyuma

(b) huyu dogo alipo kuja hapa magu aliingia na mkwala wa kununua Pikipiki mbili za bodaboda(SANLG),

(c)alikuwa akishinda na kuzurula kwenye Tax (ya kukodi)

(d)mkewe alikuwa amejifungua(mtoto wa kike), but alipomfata baba watoto wake Alimkana mkewe na kumtishia maisha na ndipo huyu mkewe aliamua kwenda Polis na kusababisha huyu dogo (pascal) kukamatwa na kupelekwa ktk ki2o cha polisi cha hapa Magu

(e)alikuwa akitaka kuchukua hela kwenye ATM, alikodi Tax na kwenda Mwanza mjini kutoa (na wkt hata ATM na pale Magu zipo )
>kwa wasio jua [ MAGU ipo km 60 kutoka Mwanza mjini]

(f)Alizimika kwa penzi la Dada mmoja wa saluni ya hapa MAGU
Na walikuwa wakienda Bar na huyu mdada walikuwa wakitumia mpaka LAKI MBILI (kula+ kulala) per day
kwa sasa ameuza NYUMBA yake aliyokuwa amenunua baada ya kutoka Bss (Tsh.10ml)
mpaka hii habari inaandikwa Magu hayupo ameikimbia familia yake (mkewe na mtoto),
---the mwisho-

Dogo hakuwa na malengo aliweka heshima baa
 
Na mara ya mwisho kutoka hapa MAGU ili aende Mwanza kumtafuta mshind wa bss ili baadae akaiwakilishe mwanza kule Dar, huyu dogo yeye na kaka yake walikuwa wakiuza keki na biskut pale KAMANGA kivukon, cha kushangaza aliporudi kutoka dar (baada ya kushinda), hakumuachia kaka yake hata hela ya mtaji ,
cku moja nimemkuta huyo braza m2 pale kamanga bado anachakalika tu na analaum eti "dogo kaja lkn alicho acha kwangu ni VIATU NA JEANS tu (na hii ni kwa sababu tu nilivijaribishia so akagoma kuvivaa tena kisa eti cwezi kuvaliana na Superstar),
 
Yote tisa, lakini la kumtolea nje mama mzazi, hili halina mjadala na lina matokeo mabaya zaidi kuliko yaliyomkuta huyo dogo.
 
Baada ya kutujuza habari ya Paschal na matumizi ya fedha zake, na wewe tuambie fedha zako unavyozitumia ili tujifunze.
 
Lile li-besi lake angelitumia vizuri angefika mbali sana.
Mapromota hawakumuona tu huyu dogo, but wangewekeza kwake wangetoka sana.
Ushauri wangu tu ni kua arudi tena kwenye mziki siriazi atarudi tu kwenye chati.
 
Hivi kumbe alishindaga BSS mwaka 2009?
Dah.
Siku zinakimbia kweli.Mi naona kama ni juzi juzi tu. Kumbe miaka ishasonga.
 
Baada ya kutujuza habari ya Paschal na matumizi ya fedha zake, na wewe tuambie fedha zako unavyozitumia ili tujifunze.

mm kwa cku huwa natumia mpaka Tsh. 6000/=
(chai+lanch+dinner)
wkt mwingine inaweza ikazid mpaka 10000/=
hapo tukiwa mm na dem wangu
 
Amyner!

Hapo ndo najiuliza kweli, inakuwaje washindi wa BSS hawatoki sana kulinganisha na wale walioshindwa mapema...??
 
Back
Top Bottom