Msaidizi wa Mwl. Nyerere (Mzee Kasori) alivyowashukia viongozi wa serikali ya awamu ya nne

mengi tutayasikia ila huyu mzee Samwel. H. Kasori lengao ake nini hasa? atangaze kabisa yuko upande gani asijifanye kuleta porojo. yote hayo ni vita juu ya urais haswa kwa watu wa kaskazini na haijaanzia leo toka kwa kina mang mariale ,sokoine na sasa EL. Nyerere hakuwahi kutaman nchi hii ikamatwe na rais toka kaskazin ndo maana that time akaamua kumchafua EL.


kwa hiyo safari hii "zamu yenu" sio;hoja zako kwa nyerere zingekuwa na maana kama kanda ya nyanda za juu kusini nayo imewahi kutoa angalau waziri mkuu ukiacha huyu pinda aliyepata kwa bahati mbaya tu baada ya ile ajali yenu ya kisiasa!nyie mmeshatoa mawaziri wakuu wangapi mpaka sasa na naibu waziri mkuu juu????tukifuata hayo nchi haitatawalika!
 
wamaanisha hayo mengi aliyovurunda mchonga yanahusu ufisadi? Waweza kututajia...? Sitaki kukubaliana na makala ya mzeeel masori wala kukataa aliyoyanena, ninachofanya ni kutafaki kwa kina na kupata jibu pasi kukurupuka.
nyie ndo mna mtreat nyerere kama muabudiwa, kumbuka yeye aliwai kusema kuwa alifanya mazuri pia mabaya, nyerere, nyerere ....., ah hanjui kuwa sometimes mnaboa, uyu nae alichemsha sana tu pia.... Ingawa hii aimfanyi el kuwa msafi... Uyu el ni mchafu balaa asa akilenga dili ya kumake ela aachii uyu kimandolu, natumai angeajiliwa benki siku moja tungekuta amiamishia strong room nyumbani kwake, uyu el fisadi ni balaa sana
 
Kama unachukia dhulma ya ufisadi nakili, kisha unukuu katika wall yako ili ushiriki kumzindua lowasa kusema ukweli.......tusaidiane katika vita hii.
 
Mkuu MTM unajua nimesoma hiyo article nikaona jamaaa anajidai eti ni mwana CCM na mzalendo wa nchi hii. Alikuwa wapi siku zote kuyasema haya. Huyu ana genge lake kati ya magenge yaliyoko CCM.

Mkuu siamini kama kweli umeisoma hii article! Sio ya juzi Iliandikwa March 18, 2008 na kuchapishwa magazetini! Tujitahidi kusoma na tusikurupuke kuchangia kwa jazba! Soma tena!
 
Kwa maoni yangu, ninaona kama vile Lowassa ana sifa mbili kubwa sana.

Kwanza anajua sana kutumia mamlaka yake tena kwa ufanisi sana, na pili vile vile ana tamaa kubwa sana ya mali. Alichanganya mambo hayo mawili kwa pamoja akafanikiwa sana mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini. Unfortunately, aliyachanganya bila kutumia busara kidogo kwa vile mazingira ya wakati ule, japokuwa Azimio la Zanzibar lilikuwa limeshaanza, record za mali zake zilikuwa bado ziko wazi sana na jinsi mali hizo zilivyokua kwa ghafla wakati wakiwa waziri wa ardhi ikawa siyo siri.

Ingawa raia wengi walikuwa wanafurahia utumiaji wake wa madaraka kwa upande wa masalahi ya nchi kule wizara ya Ardhi, hawakujua sehemu ya madaraka hayo iliyokuwa imetumika kwa masalahi yake binafsi. Angekaa kimya mwaka 1995 huenda mambo yake binafsi yasingejulikana kabisa, alipotaka mamlaka ya uraisi, ndipo Mzee Nyerere akwamwaga simbi zote nje. Yeye kama mpiganaji ameamua kupigania nafasi hiyo kwa kutumia nguvu zote hasa kwa vile sasa hivi hakuna mtu mwenye uwezo wa kumkwamisha kama Nyerere, uwezo wa kipesa unamruhusu sana, na kwa kuwa siasa za kwetu zimekuwa ni za pesa. Madoa ambayo aliyapata mwaka 1995, na baadaye yakaongezeka ya Richmond mwaka 2007 na mwishowe kulazimika kuachia madaraka na kuhusishwa na ufisadi na Gamba, ni dhahiri kuwa hata pale atakapoingia madarakani na kufanya jambo lolote kwa usafi na uadilifu wa hali ya juu, bado hatajenga imani nzuri kwa kwa raia kwa vile kila mara watu watakuwa wanahusisha na matumizi ya madaraka yake na ubinafsi wake.

Ningekuwa mimi Lowasa, ningeamua kuendelea na biashara zangu kimya kimya na kuachana kabisa na siasa za Tanzania kama ambayo Rostam alivyofanya. Sote tunajua jinsi Rostam alivyofaidika kwa kuwemo ndani ya CCM lakini mwishowe akaona kuwa sasa inatosha.
 
WanaJF hivi kweli huwa tunafuatiliaga hizi makala kwa umakini na kuweka muunganisho?

Maana sio siri tunahitaji major brain over hauling ili kuweza kuikomboa hii nchi,maana hawa CCM wananuka sana na wameshindwa kuondoa nyanya mbovu kwenye tenga hivyo wanazidi kuoza..Tubadili mueleko na kuanza upya....Wahenga walisema;"Kuanza upya sio ujinga".....

Hii makala ya katibu wa Nyerere ina maana sana ktk mustakabali wa nchi yetu....
 
Ni kweli kabisa, kiongozi anapaswa kuwa muadilifu na kusimamia kweli wakati wote.

Umesomeka mkuu hongera kwa makala yako nzuri, ingawa kwa sasa inaonekana dhahili kuwa maslai ya chama tawala na baadhi ya vigogo ndio viko mbele kuliko taifa na utaifa. Unafiki mkubwa sana unafanya na viongozi wetu ktk mambo mengi ya msingi.

Sheria ni msumeno ktk nadhalia tu,na sikatika matendo hata kidogo! Lakini muda ndio utakao amua. Kukubali ukweli na kuwatayali kubadilika ni swala muhimu. Mungu mkubwa yote yatakuwa wazi na watanzania tutaamua hatma yetu.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja, huyu Mzee Kasori katueleza mambo mengi sana kuhusu Lowassa na hata alivyoombwa na Lowassa kuwa amuoombee kwa hayati mwalimu aende kumsafisha kule MONDULI ILI ASIKOSE UBUNGE!! Lowassa mwenyewe yuko hai na bila shaka anamfahamu huyu Kasori kwanini basi hajitokezi na kukanusha habari hizi kuwa sio sahihi.!Mimi binafsi nina fahamu kuwa Lowassa kwa muda mfupi alipokuwa mkurugenzi wa AICC pale Arusha alifanya madudu mengi sana ambayo yangeweza kumpeleka Lupango.
 
Naomba mods na Invisible, hii thread muinganishe na zingine zinazomuhusu Lowasa, tumechoka na hizi crap thread za Lowasa kila siku.
Pls mods do needfull
 
Ndugu yangu Nyerere is not god. Yeye mwenyewe ana mengi amevurunda na tungependa atupe majibu lakini ametangulia mbele za haki hivyo case closed na tunamheshimu na kumpenda kwa sababu pia kafanya mengi mazuri most notably ni kuishi maisha ya 'ujamaa' alivyokuwa anahubiri

Ni muhimu kumuenzi nyerere lakini hana mamlaka ya kutuamulia tunataka nini na nani awe kiongozi wetu

Binafsi simtetei lowassa but kuwa kwake tajiri ndo iwe sababu ya kumnanga na kuona hana sifa ya kushirika? Je ni ishu ya richmond, if so to be sincere tangu zimwi la richmond lilipoenda public sijawahi thibitishiwa pasipo shaka kuwa EL ndie mhusika mkuu, instead what I see and learnt of thatc is gutter and mud slinging politics at its best hearing towards character assasination. Nothing more than that.......coz there are a lot of 'super richmonds' in our country but zinazimwa makusudi kabisa

Kama nyerere alitamka alichosema it's just his own opinion and he may not be right as well......

Kichwa chako naona kizito kidogo. Swala siyo utajili. Kwani yeye ni tajili kuliko wote duniani?. Ameupataje huo utajili? Kwa nini Mwalimu Nyerere asituchagulie viongozi kama yeye alikuwa anawafahamu vizuri? Wewe uliujua extent ya wizi wa Lowassa enzi hizo?. Tena ana bahati Sokoine alishatangulia mbele ya haki. Angemchoma mshikaki.
 
Hakika Pesa na Madaraka mtu akakosa busara basi ni janga.Lakini kwa kuwa SPIRIT YA MWALIMU hiko ndani ya mioyo ya Watanzania urais atausikia barabarani,acha wenye akili zao wamchakachue fedha alizochukua mpaka watapo ona zimeisha kisha wazibue akili yake kuwa wakati wote na mbio zote hakuna ajualo, akikosa kiharusi basi amshukuru Mungu aludi Monduri akakae shamba.
 
Ameyaanza mwenyewe, mizimu imetibuka. Hizi bado rasharasha, masika hayajaanza!
 
ndugu yangu
nyerere is not god. Yeye mwenyewe ana mengi amevurunda na tungependa atupe majibu lakini ametangulia mbele za haki hivyo case closed na tunamheshimu na kumpenda kwa sababu pia kafanya mengi mazuri most notably ni kuishi maisha ya 'ujamaa' alivyokuwa anahubiri

ni muhimu kumuenzi nyerere lakini hana mamlaka ya kutuamulia tunataka nini na nani awe kiongozi wetu

binafsi simtetei lowassa but kuwa kwake tajiri ndo iwe sababu ya kumnanga na kuona hana sifa ya kushirika? Je ni ishu ya richmond, if so to be sincere tangu zimwi la richmond lilipoenda public sijawahi thibitishiwa pasipo shaka kuwa el ndie mhusika mkuu, instead what i see and learnt of thatc is gutter and mud slinging politics at its best hearing towards character assasination. Nothing more than that.......coz there are a lot of 'super richmonds' in our country but zinazimwa makusudi kabisa

kama nyerere alitamka alichosema it's just his own opinion and he may not be right as well......




ndugu yangu mmasai wewe unataka lowassa awe rais!jua tu ata afanyeje atakuwa rais!!sasa anajiona kashinda kimkakati!na ukweli atashinda ndani ya ccm,hilo linajulikana ila subiri uone kama atakuwa rais wa nchii hii!!!labda nyerere akuipigania nchii hii kwa dhati!!!laana ya mungu itamwanda!! Natamka leo laana ya mungu itamuandama yeye na uzao wake wote!!!na hili litaonekana tu!
 
Mkuu MTM unajua nimesoma hiyo article nikaona jamaaa anajidai eti ni mwana CCM na mzalendo wa nchi hii. Alikuwa wapi siku zote kuyasema haya. Huyu ana genge lake kati ya magenge yaliyoko CCM.[/QUOTE]


WEWE HUJUI LOLOTE!!!HUYU MZEE ALIYANENA HAYA 2008!!
 
Mzee kasori asante sana kwa maelezo yako.
Katika vitu vimekuwa vinanisikitisha ni kuona tanzania imeishiwa hata wazee wanaosema ukweli.
Mwalimu kama alifanya makosa ni ya kibinadamu lakini nikili alitupenda watanzania wote upeo. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen. Kama siyo sera zake za kunisomesha bure nigelikuw anaozea kijijini. Kilasiku namuombea! Ukitaka kujua wema wake angalia haya mafisi aliyotuachia1
 
Mzee kasori asante sana kwa maelezo yako.
Katika vitu vimekuwa vinanisikitisha ni kuona tanzania imeishiwa hata wazee wanaosema ukweli.
Mwalimu kama alifanya makosa ni ya kibinadamu lakini nikili alitupenda watanzania wote upeo. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen. Kama siyo sera zake za kunisomesha bure nigelikuw anaozea kijijini. Kilasiku namuombea! Ukitaka kujua wema wake angalia haya mafisi aliyotuachia1

Kwa maneno haya nimeishiwa maneno ya kusema
 
Back
Top Bottom