Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,137
48,808
Watu 4 wamejeruhiwa katika msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya gari moja kuanguka huko Nanguruwe wakati wakitoka mtwara kuelekea Tandahimba.

14183868_980775645366743_2531709470379328261_n.jpg


aqaq.jpg


Majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula,

Chanzo: Radio One

=======
UPDATES:

Msafara wa Makamu wa Rais wa wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara ambapo taarifa zinasema kati ya majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu Rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari lililokuwa limebeba baadhi ya waandishi wa habari walioambatana na ziara hiyo, liliacha njia na nusura lipinduke.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba, imekuwa ikitajwa kutokuwa na kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
 
Wekeni na kapicha basi tuone ajali ilikua kubwa kiasi gani!
 
Watu 4 wamejeruhiwa katika msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya gari moja kuanguka huko Nanguruwe wakati wakitoka mtwara kuelekea Tandahimba.

View attachment 396808

Majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula,

Chanzo: Radio one
Sasa huyo ef ef you hayo mabomu yakilipuka si ndo atawaongeza majeraha?
 
Back
Top Bottom