Msaada wa ushauri kuhusu suala la hili la upimaji wa ardhi

memory card

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
252
153
Salam,

Ndugu zangu naomba ufafanuzi wa kitaalamu nilinunua kiwanja ambacho kimepimwa kabisa na kiukweli kilikuwa kikubwa sio mtaalam sana ila wakati tunahesabu hatua ilikua 60 kwa 40 na kipo kwenye makazi ya watu kiufupi kamji kanakuwa kweli huku kwetu swax.

Nilivyoona hiki kiwanja ni kikubwa nikamkatia jamaa flani migu 20 maana yake kiwanja 1 kilichopimwa mi nikamkatia jamaa miguu 20 kwa hiyo mpaka sasa vimekuwa 2.

1) Je kuna athari yeyote mbeleni huko?

2) Kuna uwezekano wa kupimwa tena vitoke viwili maana yake wagawe pale kati mpakani kwa jamaa?

3) Nikitaka hati inakuaje?
 
Aikooooo!
Unasema ulihesabu hatua ilikua 60 kwa 40 means ni 60 ft kwa 40ft . Vipimo vya ft vinawadnganya sana tena ukiwekewa no zilivyo kubwa hizo utadhani ni pakubwa sana hizo 60ft ni sawa na 18M na 40ft ni 12M Hivyo ni 18 X 12 = 216 sqm
anyway sijui nilichokua nalinganisha :confused: :confused: :confused:
 
nafikiri tujikite kwenye hoja ya msingi hayo mambo ya ft or what mimi ndo niko site wakuu huu uwanja ni mkubwa kwangu imagine niliuziwa 1000000 (1million) mi nimekata hiyo miguu 20 nikala 1020000
 
Salam,

Ndugu zangu naomba ufafanuzi wa kitaalamu nilinunua kiwanja ambacho kimepimwa kabisa na kiukweli kilikuwa kikubwa sio mtaalam sana ila wakati tunahesabu hatua ilikua 60 kwa 40 na kipo kwenye makazi ya watu kiufupi kamji kanakuwa kweli huku kwetu swax.

Nilivyoona hiki kiwanja ni kikubwa nikamkatia jamaa flani migu 20 maana yake kiwanja 1 kilichopimwa mi nikamkatia jamaa miguu 20 kwa hiyo mpaka sasa vimekuwa 2.

1) Je kuna athari yeyote mbeleni huko?

2) Kuna uwezekano wa kupimwa tena vitoke viwili maana yake wagawe pale kati mpakani kwa jamaa?

3) Nikitaka hati inakuaje?
Kama kilikuwa kimepimwa na kilikuwa na mpaka Namba ya kiwanja tayari (Plot Number) na tayari umekiuza nusu, unapaswa uwaite tena wapimaji ili wafanyie amendment mchoro wa ramani ya hilo eneo wa awali ili waweze kutoa viwanja viwili kutokana na ukubwa wa eneo lililobakia. Baada ya hayo marekebisho ndio utaweza kufuatilia process za kuandaliwa hati.
 
thanks sana blaza
 
Halafu ili Jamaa uliyemuuzia asiingie gharama zaidi unatakiwa kukitoa kwa Makubaliano ya Kumpa Zawadi (Gift Deed).
 
Salam,

Ndugu zangu naomba ufafanuzi wa kitaalamu nilinunua kiwanja ambacho kimepimwa kabisa na kiukweli kilikuwa kikubwa sio mtaalam sana ila wakati tunahesabu hatua ilikua 60 kwa 40 na kipo kwenye makazi ya watu kiufupi kamji kanakuwa kweli huku kwetu swax.

Nilivyoona hiki kiwanja ni kikubwa nikamkatia jamaa flani migu 20 maana yake kiwanja 1 kilichopimwa mi nikamkatia jamaa miguu 20 kwa hiyo mpaka sasa vimekuwa 2.

1) Je kuna athari yeyote mbeleni huko?

2) Kuna uwezekano wa kupimwa tena vitoke viwili maana yake wagawe pale kati mpakani kwa jamaa?

3) Nikitaka hati inakuaje?
Nyinyi watu wengine mnaboa sana, hata mnaweza kufanya mtu akajuta kufungua nyuzi zenu.

Unasema kiwanja kimepimwa kabisa kwa hiyo kitakua na documents halali (leseni, offer au title deed) kisha unakuja kuzungumzia habari za miguu, kwa hiyo documents za kiwanja zinaonyesha vipimo vya miguu??

Yaani karne hii bado mtu anazungumzia habari za miguu, hakuna tape measure madukani?
 
Salam,

Ndugu zangu naomba ufafanuzi wa kitaalamu nilinunua kiwanja ambacho kimepimwa kabisa na kiukweli kilikuwa kikubwa sio mtaalam sana ila wakati tunahesabu hatua ilikua 60 kwa 40 na kipo kwenye makazi ya watu kiufupi kamji kanakuwa kweli huku kwetu swax.

Nilivyoona hiki kiwanja ni kikubwa nikamkatia jamaa flani migu 20 maana yake kiwanja 1 kilichopimwa mi nikamkatia jamaa miguu 20 kwa hiyo mpaka sasa vimekuwa 2.

1) Je kuna athari yeyote mbeleni huko?

2) Kuna uwezekano wa kupimwa tena vitoke viwili maana yake wagawe pale kati mpakani kwa jamaa?

3) Nikitaka hati inakuaje?
Jina lako haliendani kabisa na hicho ulichofanya, vinatofautiana sana.
Kama kiwanja kimepimwa, yaani Surveyed Plot, Je, ulifuata hatua zote za kisheria ktk kununua kiwanja hicho?Ni kiwanja namba ngapi, kitalu gani na kipo eneo gani hasa (location)? Je, ramani ya upimaji (survey map) ya hicho kiwanja umewahi kuiona au unayo nakala yake? Je, nyaraka za umiliki za hicho kiwanja unazo?Kiwanja hicho kina ukubwa gani hasa? Kiwanja hicho kimepangiwa matumizi gani hasa kwa mujibu wa mchoro wa mipangomiji?
Kitendo ulichofanya ni makosa makubwa, ilipaswa kwanza ujue taarifa zote muhimu kuhusu kiwanja hicho kabla ya kujaribu kufanya muamala wowote ule kuhusu kiwanja husika. Inaweza ikakuwia vigumu sana hapo baadaye katika kufanya mchakato wa kukigawanya (subdivision) ya hicho kiwanja. Umefanya UHOLELA sana ktk kushughulikia suala la kiwanja hicho.
 
Chief unakitu naomba unisaidie hiki kitu.
Je?, Unaponunua kiwanja hasa mjini ni nyaraka zipi muhimu kuwa nazo na je? Ni taarifa zipi muhimu napaswa niwe nazo juu ya kiwanja husika.
 
Hapo inabidi umtafute mtaalamu wa upimaji yeye .atachukua vipimo kwa hilo eneo na kufanya search ,Hiyo search itakuja na majibu iwapo eneo limepimwa au laaah,matumizi ya hilo eneo kama ni kwa makazi,biashara n.k gharama zake sio kubwa ni 50k - 80k
Kama majibu ya hio search mtaalamu atakushauri ununue ilo eneo basi utatafuta mwanasheria ili zoezi la mauziano liwe official.
Poa kuhusu hali ya eneo ni juu yako sasa ucheze na majirani vizuri wakupe info zake .mfano migogoro,mafuriko
 
Kuna kitu mzee wangu alinifundisha kuhusu kupima viwanja kwa "miguu".
Alisema, kuanzia hatua ya kwanza, hua inakua kubwa lakini anaviendelea kupima hatua inazd kupungua (kibinadamu) maana hawez kuendelea kupanua mguu kama mwanzo.
Kwaio kawaida sana kupunjana.
Ni heri ujatoa hela kdg ukaenda na mtaalam wa upimaji akakusaidia.
 
Back
Top Bottom