Kiresua
JF-Expert Member
- May 13, 2009
- 1,184
- 259
Ni muda sasa naamini hapa Jukwaani ni kisima na msaada tosha kwa mambo mbalimbali. Wadau, nilinunua redio ya SONY model no. HCD-GNZ55D miaka 2 iliyopita. Redio hi imepata tatizo la power. Umeme hauingii. Nilipeleka kwa wakala wa sony pale Kipata st. Kwa kuwa warant imeshapita niliomba kufanyiwa ispection then service. Baada ya muda wakanipigia sim kuniambia kuwa inahitaji replacement ya POWER BORD na gharama zake. Yani garama yake ni 68% ya original value kubadilisha power bord. Nikaona haina afya kiuchumi, nikabeba redio yangu. Sasa bandugu nilihisi naibiwa na wale wahindi, Je kuna msaada wowote nitakavyoweza kuipata hiyo bord niendelee na kupata mziki ndani kwangu? Msaada jamani wana Jf.