Msaada Wa kisheria kwenye eneo langu linajengwa secondary bila kulipwa fidia

js52471224

Member
Oct 8, 2017
36
15
Habari ndugu jamaa na marafiki kwenye hili jukwaa sheria, niende kwenye Maada moja kwa moja. Nilikuwa nimesafiri kurudi nikakuta eneo langu lenye ukubwa Wa eka 5 eka 3 nimepanda miti aina ya paina mikubwa eka 2 ndio nalima limesafishwa kwa ajili kuaza ujenzi Wa secondary.

Nikaenda ofisini kumuona mtendaji Wa kijiji mwenyekiti wakaniambia watu wamejitolea maeneo bure. Mimi nikawambia eneo langu sitoi bure nataka fidia, wakasema sawa wananitafutia eneo lingine. Lakini sasa toka mwezi 5 2023 mpaka Leo mwezi 11 2023 kimya, kila nikifatilia wanasema nisubiri.

Natayari walisha kabizi eneo kwenye uongozi Wa kata, natayari wanaendelea na majengo secondary. Naomba msaada wenu ilinilipwe fidia nikafungue kesi kwenye mahakama ipi, ya mwanzo au ya wilaya? Namna ya kufungua hii kesi? Nitashukuru msaada wenu.
 
Habari ndugu jamaa na marafiki kwenye hili jukwaa sheria, niende kwenye Maada moja kwa moja. Nilikuwa nimesafiri kurudi nikakuta eneo langu lenye ukubwa Wa eka 5 eka 3 nimepanda miti aina ya paina mikubwa eka 2 ndio nalima limesafishwa kwa ajili kuaza ujenzi Wa secondary. Nikaenda ofisini kumuona mtendaji Wa kijiji mwenyekiti wakaniambia watu wamejitolea maeneo bure. Mimi nikawambia eneo langu sitoi bure nataka fidia, wakasema sawa wananitafutia eneo lingine. Lakini sasa toka mwezi 5 2023 mpaka Leo mwezi 11 2023 kimya, kila nikifatilia wanasema nisubiri. Natayari walisha kabizi eneo kwenye uongozi Wa kata, natayari wanaendelea na majengo secondary. Naomba msaada wenu ilinilipwe fidia nikafungue kesi kwenye mahakama ipi, ya mwanzo au ya wilaya? Namna ya kufungua hii kesi? Nitashukuru msaada wenu.

Tafuta mwanasheria
 
Jitolee mkuu ijengwe shule, huoni ufahari mkuu kuwa sehemu ya mafanikio ya jamii?

Tena unabaki na eneo kubwa tu

Hela hazina mwisho kaka, na sio kila mara lazima tulipwe kwa tuyafanyayo! Hela sio kila kitu kaka
 
Huna uzalendo kwanza ujue ardhi ni mali ya umma we katafute sehemu nyingine pisha shule ijengwe we hiyo ardhi uliipataje.
 
Jitolee mkuu ijengwe shule, huoni ufahari mkuu kuwa sehemu ya mafanikio ya jamii?

Tena unabaki na eneo kubwa tu

Hela hazina mwisho kaka, na sio kila mara lazima tulipwe kwa tuyafanyayo! Hela sio kila kitu kaka
Sina eneo lingine ndugu
 
Habari ndugu jamaa na marafiki kwenye hili jukwaa sheria, niende kwenye Maada moja kwa moja. Nilikuwa nimesafiri kurudi nikakuta eneo langu lenye ukubwa Wa eka 5 eka 3 nimepanda miti aina ya paina mikubwa eka 2 ndio nalima limesafishwa kwa ajili kuaza ujenzi Wa secondary.

Nikaenda ofisini kumuona mtendaji Wa kijiji mwenyekiti wakaniambia watu wamejitolea maeneo bure. Mimi nikawambia eneo langu sitoi bure nataka fidia, wakasema sawa wananitafutia eneo lingine. Lakini sasa toka mwezi 5 2023 mpaka Leo mwezi 11 2023 kimya, kila nikifatilia wanasema nisubiri.

Natayari walisha kabizi eneo kwenye uongozi Wa kata, natayari wanaendelea na majengo secondary. Naomba msaada wenu ilinilipwe fidia nikafungue kesi kwenye mahakama ipi, ya mwanzo au ya wilaya? Namna ya kufungua hii kesi? Nitashukuru msaada wenu.
Awali ya yote pole kwa majibu ya wadau akina saigilomagema. Kujitolea ni hiari ya mtu ingawa kuna hiyari ya lazima.

Hilo eneo ambalo wamelichukua kimsingi ni sehemu ya maisha yako, maana umesema huwa unalima. So kitendo cha serikali ya kijiji kuchukua eneo bila wewe kuridhia ni unyang'anyi uliofanywa na Kijiji.

Ushauri wangu, waandikie barua serikali ya kijiji kuwataka wasitishe harakati zao. Nakala peleka Kata na Halmashauri.

Pia nenda Mahakamani kaweke zuio (court injunction). Mahakama itatoa zuio hadi pale wewe na kijiji mtakapokubaliana.

Watu wanapiga mabilioni huko halafu wewe kapuku unasema unajitolea? Wakupe fidia ya pesa au fidia inkind. Au kama utawapa bure, wafuate taratibu za kukuomba. Sio wanajichukulia tu wakati umevuja jasho

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Habari ndugu jamaa na marafiki kwenye hili jukwaa sheria, niende kwenye Maada moja kwa moja. Nilikuwa nimesafiri kurudi nikakuta eneo langu lenye ukubwa Wa eka 5 eka 3 nimepanda miti aina ya paina mikubwa eka 2 ndio nalima limesafishwa kwa ajili kuaza ujenzi Wa secondary.

Nikaenda ofisini kumuona mtendaji Wa kijiji mwenyekiti wakaniambia watu wamejitolea maeneo bure. Mimi nikawambia eneo langu sitoi bure nataka fidia, wakasema sawa wananitafutia eneo lingine. Lakini sasa toka mwezi 5 2023 mpaka Leo mwezi 11 2023 kimya, kila nikifatilia wanasema nisubiri.

Natayari walisha kabizi eneo kwenye uongozi Wa kata, natayari wanaendelea na majengo secondary. Naomba msaada wenu ilinilipwe fidia nikafungue kesi kwenye mahakama ipi, ya mwanzo au ya wilaya? Namna ya kufungua hii kesi? Nitashukuru msaada wenu.
Pole kwa changamoto.

Kimsingi mtu yeyote anaemiliki ardhi Tanzania na kuendeleza, ikiwa itatokea kwa maslai ya umma serikali itahitaji eneo lake basi sheria ya ardhi inaitaka serikali kumfidia mtu huyo haraka na fidia ya kutosha.

kulingana na swala lako niwazi kuwa unaidai serikali ya Kijiji ambayo imechukua eneo na kujenga shule bila kukupa fidia.

NINI UFANYE
Kwakuwa serikali ya Kijiji ipo chini ya serikali KUU ambayo maswala yote ya kisheria kuhusu serikali yako chini ya usimamizi wa mwanasheria mkuu wa serikali basi sheria inaitaka shauri lolote la madai dhidi ya serikali lielekezwe kwa mwanasheria mkuu. Yaani unamshtaki mwanasheria mkuu wa serikali.

UTARATIBU.
1. Unapaswa kuipa serikali taarifa (notice to sue) kwa siku zisizopungua 90 kabla ya kufungua kesi yako hakamani.

2. Unafungua wapi kesi? Kesi zote zakuishtaki serikali zinafunguliwa mahaka KUU.

3. Unaomba nn mahakamani? ukiishtaki serikali huombi zuio la muda. Bali unaomba tamko. Ili kusubiria kesi mama.

- pia unaomba makama itoe amri yakuitaka serikali kupitia kwa mtunza hazina ikulipe kiasi Cha fedha unachodai.

NB: Kabla yakufikia huko unaweza kuandika barua kwenda kwa waziri/katibu/mkuu wizara ya ardhi ilikuelezea malalamiko yako juu yakutoridhishwa na kitendo kilichofanywa na serikali ya Kijiji.

KWA MAELEZO NA HATUA ZAIDI. WASILIANA NA MWANASHERIA WAKO ILI KUPATA HAKI YAKO.
 
Back
Top Bottom