Uchambuzi wa tuhuma za Dhulma za Tajiri Saalah Dhidi ya Eliud

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Nilikuwa nafuatilia mkasa uliokuwa umeletwa siku tatu nyuma na ndugu nokwenumuya, akiwasilisha malalamiko yake kuhusu uonevu na dhulma inayofanywa na tajiri mmoja aliyemtambulisha Kwa jina la Saalah Dhidi ya Eliud.
Nikaona nitoe uchambuzi Kwa uchache ili kama taifa tuwezi kujifunza na kujua ni vipi tunatoka.
Haya tusipoteze muda;

I) Ukiona sehemu yoyote au nchi yoyote inadhulma au uonevu basi kosa sio la hao wadhulumaji Bali kosa ni la viongozi na watendaji WA serikali.
Ni ngumu na nadra Sana kukuta dhulma au uonevu kwenye taifa linaloongozwa na viongozi wenye kupenda Haki.

Matajiri na watu mashuhuri ukiona wanauthubutu wa kukudhulumu na kukuonea wala usiwalaumu wao, wakulaumiwa na viongozi na watendaji wanaoongoza,

ii) Watanzania wengi wanapenda kutia wenzao hasara alafu wakiambiwa walipie hiyo hasara wanaona wanaonewa na kudhulumiwa.
Watanzania wengi ni Wezi, wanatabia za udokozi dokozi, alafu siku ukimshika ukimuambia Lipa anaona tabu, ukitumia mabavu anasema unamuonea na kumdhulumu.
Na Kwa vile yeye ni mnyonge basi wenye Akili kama zake ambao ndio wengi watamuonea huruma na kukuchukulia wewe unaroho Mbaya Kwa kudhulumu Watu.

iii) Watanzania wengi ni Wanafiki, watasema mambo mabaya ya MTU Baada ya kugombana lakini Kabla hamjagombana naye anakuwa sehemu ya ushiriki WA hayo mabaya.
Mtanzania unaweza shiriki naye madili Fulani haramu akakaa kimya Kwa sababu naye anapatamo kitu lakini siku mkipishana na kutofautiana Kwa vile hapati chochote na yupo nje ya mfumo ndio atajifanya anayasema mabaya ya eneo Fulani.

Watu wa namna hiyo Mimi kama Taikon huwaga siwasikilizi na wala kuwatetea Kwa chochote kile, zaidi ningekuwa serikalini ningewatia ndani, Kwa sababu wanatabia ya unafiki na usaliti.

Hata kwenye viongozi wanatabia Hii, akiwa Waziri au sehemu ya uongozi, anakaa kimya mabaya yakifanyika iwe hadharani au Kwa Siri, alafu likiondolewa unakuta linaanza kupiga Kelele.
Unafiki na usaliti ni tabia ya Watu wahalifu na waovu.

Kwa kesi ya Saalah na Eliud, huyo Eliud miaka yote ameshiriki kufanya uhalifu na Hilo genge analolituhumu lakini alikaa kimya, Leo Baada ya kupishana na naye kufikikiwa na michezo hiyo michafu ndio anapiga mayowe.

Taikon huwaga nasemaga, Usisaidie Maskini iwe Maskini wa Kifikra, kiuchumi au whatever, Kwa sababu Tabia nyingi za Maskini wengi ni Mbaya.

iv) Wanaoonewa na kudhulumiwa ni Watu wasiojasiri.
Kimsingi Mimi Pesa yangu huwezi kuila kienyeji, tena kimabavu ndio kabisa haiwezekaniki. Iwe Kwa damu au roho jua au Mvua hilo halitowezekana Dunia ingalipo.
Hutoweza kunidhulumu Kwa sababu sitokudhulumi na siwezi dhulumu cha MTU. Hivyo endapo utanidhulumu tena kimabavu Kwa kisingizio chochote kile labda ATI umenizidi uwezo wa kifedha, kihashi na kicheo au kimamlaka basi jua kuwa umeingia kwenye vita nzuri Sana.

Sisi ni Watu ambao hatumuachii Mungu,

Acha niwape kisa kimoja kilichotokea miaka ya 2019 kinanihusu Mimi mwenyewe;

Watanzania wengi ni Watu waoga waoga Sana. Niliwahi kufanya kazi sehemu Fulani hapa Dar, ndio nikagundua Watanzania wengi ni Watu waoga kudai Haki zao nafikiri ni Kwa sababu wengi sio waaminifu.

Mimi ninaamka na ninakuja Kwa wakati kazini, ninakufanyia kazi zao vizuri, matunda ya Kazi yanaonekana, hujawahi nilalamikia Kwa chochote, kama nimekuwa mwaminifu kwako Kwa kiwango cha 100% basi elewa kuwa utakapo nizingua nitakuwa mwaminifu Kwa asilimia zilezile 100% kukulipa unayonifanyia bila kujali Matokeo.

Yule Tajiri akapata Crisis ya kiuchumi ila hakutuambia Sisi wafanyakazi wake, hivyo akawa analipa baadhi ya wafanyakazi ikiwemo Mimi Ila wengine akawa anashindwa kuwalipa, wale ambao hawakulipwa walifikisha miezi mitatu na ndipo nami akashindwa kunilipa. Mpaka taasisi inafungwa Mimi sikulipwa Kwa miezi mitatu, huku wenzangu wakiwa hawajalipwa miezi sita.

Nilikuwa ninabiashara zingine hivyo sikuwa naitegemea Sana Ile Pesa.
Akatupiga Kalenda wee, Mimi nikawa namuelewa, tulikuwa tunaishi kwenye compound ya Kampuni, tukashangaa siku moja wamekuja Mapolisi Wawili wakiwa na Sare, wakatuambia kuwa ATI kuna kitu kimeibiwa kwenye Ile Compound ya Kampuni, na washukiwa WA wizi huo ni Sisi.

Mimi; Wewe unajua Sisi humu ndani tupo wangapi na ni kina Nani? Maana ninyi mmesema ni Polisi.
Polisi: hatujui ninyi ni kina Nani
Mimi:. Kama hamjui Sisi ni kina Nani, bila Shaka pia hamjui Kwa nini tupo ndani ya eneo hili, si ndio?,
Polisi: wewe mbona unajifanya Mjuaji, Sisi hatutaki tutumie nguvu,
Mimi: Kutumia nguvu ya nini, mnaweza onyesha uhalali WA ninyi kuwa hapa?

Polisi: unasikia wee, usijiingize kwenye matatizo (akaongea Polisi wa pili)
Mimi: Kwa hiyo Mwenye kampuni ndio amewatuma ili mje kututisha? Yeye tunayemdai hatujampeleka Polisi wala serikali kwani tulichukulia Hii ishu itaisha Kwa Amani lakini yeye kawaita ninyi polisi(nikacheka)
Mimi: Mlivyopita pale getini hamkuona Mlinzi? Yeye kazi yake ni kulinda Mali zilizomo humu, yeye ndio wakuulizwa vitu vilivyopotea. Sisi sio walinzi WA eneo hili.

Hapo tukaanza kujibishana hovyohovyo. Huku wafanyakazi wenzangu walionizidi wakinizuia nisijibishane nao kwani nitajipata kwenye matatizo.
Nikawaambia huwaga sioni Shida kujipata kwenye matatizo nikiwa napigania Haki zangu. Ikiwezekana hata Kufa au kuuana hiyo kwangu sio Shida.

Sasa ukiongea maneno haya lazima Watu wakutazame Kwa Makini alafu walinganishe maneno yako na vile unavyoonekana😂😂. Sasa muonekano wangu ulikuwa mbali Mno na maneno yangu. Walikuwa wakiniona kama kijana mpole mwenye uso mtulivu na pengine barubaru. Lakini walisahau kuwa Sura sio Roho.

Nikachukua simu nikampigia Yule Tajiri, akapokea,
Mimi: Shikamoo Boss, Kwa kweli leo umefanya Jambo la ajabu Sana. Sisi tunayekudai hatujakuletea polisi, hatujaenda hata serikali za mitaa, wala hatujaenda hata Mahakama za usuluhishi kukushtaki, tumekuvumilia Kwa sababu tunaroho ya Mungu juu yetu, wewe mwenyewe ndio ulituambia tubaki humuhumu ndani ya compound yako mpaka utakapotulipa pesa zetu, ukasema ndani ya miezi miwili utafanikisha Hilo, huu ni mwezi wa tatu hujafanya hivyo, lakini tumekuwa Wema kwako, hatujakutukana wala kusema neno lolote baya juu yako"

" Wala kukushtakia popote pale hata Kwa Mungu hatujasema neno lolote zaidi ya yote tunakuombea ili mambo yako yafanikiwe ili utulipe Pesa zetu ili tusiachane Kwa kinyongo. Leo hii unatuletea polisi!! Sisi Leo tumekuwa Wezi? Baada ya kukutumikia Kwa uaminifu wote leo hii Sisi tumegeuka Wezi? (Nikacheka)"

"Nimewapa Leo na kesho tuu muondoke hapo, nataka kufanya shughuli zingine. Pesa zenu mtapewa"
Yule Tajiri Mwanamke akasema,

Mimi: sasa kama ulikuwa unataka tuondoke si ungetuambia tuu. Ulifikiri kila MTU anaogopa Polisi? Ulidhani tutatishika?
Haujafanya Fair kabisa,
Boss hivi unawafukuza Watu ndani ya siku Mbili wawe wameondoka, hivi haujui humu kuna wanaume na familia zao wameziacha mkoani, wengine Mwanza, wengine Musoma, na wengine Dodoma.
Hawa wote wanafamilia, Nauli Watatoa wapi? Na wakifika majumbani mwao mikono mitupu ilhali walikufanyia kazi unafikiri hiyo imekaaje?

Kwa udhalimu ulioufanya ninauhakika utaulipia tuu kivyovyote vile"

Hapo akakasirika Sana, akaanza kunijia juu huku akionyesha kiburi chake;
Tajiri Mwanamke: Nisikilize Robert, Kwa vile unajifanya Mjuaji Pesa zako sitakupa, nitawapa wenzako Ila wewe sitakupa, wewe si unajifanya mjuaji, tuone Nani ataumia, nenda polisi, nenda Mahakamani, nenda popote lakini Pesa yako sitakupa, alafu tuone utafanya nini.

Mimi: (Nikacheka) unafikiri kila mtu anamawazo kama yako, Mimi jasho langu halijawahi kuliwa popote pale. Pesa yangu lazima uitoe, simu hii nimekupigia ili uwalipe hawa wenzangu pesa Yao maana yangu ninauhakika 100% utaitoa tuu.
Kama nilivyokuwa mwaminifu kukufanyia kazi na hata wewe ni shahidi vivyohivyo nitakuwa mwaminifu kuhakikisha utailipa Pesa yangu, utaamua mwenyewe uilipe Kwa namna gani Kwa nguvu au Kwa hiyari, Kwa jasho au Kwa damu, wewe au Watoto wako. Kwa sababu mchuma janga hula na wakao. Kwa vile wewe umekuwa dhalimu na hiyo Pesa ninauhakika umekula na familia yako, hivyo lazima nao wahusike"

Kufikia hapo akakata simu,
Wale Polisi wakawa wananitazama, na wafanyakazi wenzangu wakawa wananishangaa.

Polisi: Sasa Ndugu huoni hiyo inaweza kuwa shida kwako kama wakiamua kukupeleka Mahakamani? Fuatilia mambo haya polepole yanaweza kukuletea matatizo
Mimi: ninyi polisi ni Vijana wadogo Kwa mnavyoonekana, nafikiri tupo rika Sawa.
Msipende kuingilia mambo yasiyowahusu hasa yanayohusu jasho la Watu... Huo ni ushauri tuu nawapa, mnahiyari ya kuupokea au kuukataa.

Mara simu yangu inaita Kwa namba ngeni. Napokeo simu,
Mimi: Hello
Unknown; Hello, naongea na Mr. Robert
Mimi; Ndio, Nani mwenzangu?
(Anajitambulisha)
Mimi: Ndio Mume wa Boss,
Mume wa Boss: Tafadhali nakuomba usiingize familia kwenye mambo yenu.
Vinginevyo nitakufanya kitu kibaya hutokuja kusahau.

Mimi: sasa Kaka mkubwa, Mimi nikifikiri Kwa kuwa wewe NI mwanaume utakuwa na hekima angalau kidogo lakini kumbe wewe ndiye mpumbavu Kabisa.
(Ananikatisha lakini NAMI nakazana) sikiliza... Sikia.... Sikiliza...( Anaamua kutilia)

Mimi: nilitegemea ungeniambia, Bwana Mdogo huna haja ya kupaniki, tunajua tumechelewa kuwalipa Kwa wakati hivyo tunaomba Radhi, lakini tutawalipa ndani ya muda mfupi, jukumu hilo nitalifuatilia mwenyewe kuhakikisha mnalipwa Pesa zenu. Huna haja ya kufikia kuingiza wasiohusika kama Familia.

Mimi: Hivyo tuu ningekuona unaakili. Lakini Kwa vile ni mjinga unadhani Vitisho vyako ndio Suluhu ya Jambo hili. Nisikilize (nataja jina lake) katika Jambo hilo ninakuhakikishia hakuna atakayekusaidia, labda sio Mimi. Kama unafikiri kuna msaada nakuhakikishia hautaupata.

Mume wa Boss: utanifanya nini wewe kapuku? Kwani hamna kwenu, ondokeni hapo, usitake nikufanye kitu mbaya.

Mimi: Kitu kibaya zaidi ya kunicheleweshea Pesa yangu sidhani kama unazaidi.
Watoto wa WENZENU wanapata shida Kwa sababu Baba zao hamuwapi pesa, huyu mmoja MKE wake alijifungua kidhalili na Kwa kusikitisha kisa udhalimu wenu, lakini ninyi hamtaki familia zenu ziumizwe Kwa Makosa yenu, Watoto wenu wacheke, wafurahie Maisha, wasome shule nzuri kisa na mkasa ninyi ni maboss, kipimo mlichotupimia ndicho hichohicho nitakachokitumia. Kwa Njia ipi subirini mtaona"

Nikakata Simu.
Akapiga, nikakata, akapiga nikakata tena.
Kisha simu ya polisi mmoja ikaita, akapokea, Yule polisi akaambiwa maneno Fulani ambayo nilikuja kuyaelewa kuwa ameambiwa anipe simu.

Mimi: Nini?
Polisi: Ongea naye
Mimi: Nani?
Polisi: Boss wako.
Mimi: wewe si ulisemwa haukutumwa na Boss, huyo boss amepata wapi namba zako? Kwa hiyo wewe haukutumwa na mkuu wako WA kituo? (Nikawa nasoma Kwa Sauti namba na jina lilikuwa kwenye Beji ya kwenye Shati lake)
Polisi: Amekataa, ngoja tuwaachie mambo yenu.

Wale Polisi wakaondoka, lakini tayari nilikuwa nimechukua namba na majina Yao. Nikayafuatilia majina Yao. Nikagundua Yule polisi aliyekuwa anaongea na kufokafoka Sana alikuwa ni mdogo wake na Mume WA Boss wetu(yaani shemeji wa Boss).

Wenzangu (walikuwa watano) wakaingiwa na hofu. Wakaazimia kuondoka kesho yake.
Kwa upande wangu sikutaka kujihakikishia najiamini Sana, sikutaka kupuuzia vitisho nilivyopewa. Nilijua ninatakiwa kuchukua hatua kadhaa,
Nikachukua Dairy yangu nikaandika tukio la siku Ile Kwa ufupi mambo muhimu kama Siku, Tarehe, masaa, mazingira, Wahusika na majina Yao, baadhi ya maneno, kisha Ile Record nikaiweka kwenye Memory card yangu ya akiba ambayo huwaga naiwekaga sehemu maalumu.

Kilichofuata, ni kuchukua Daftari jingine na kuunda Mpango mkakati wa kukabiliana na tukio lililokuwa linaendelea,
I) tukio lilipoanzia, sehemu lilipo na upi mwelekeo.
ii) Rasilimali zipi nilizonazo naweza kuzitumia kukabiliana na ishu hii;
a) kiasi cha fedha nilichonacho,
Nilikuwa na kiasi kidogo cha fedha kama milioni tano tuu😀😀
b) Rasilimali Watu.
Ni Wahusika gani waingie katika tukio Hili, kila mhusika na Role yake, hapa bila Shaka kuna Wazazi, baadhi ya Ndugu, na wanasheria pamoja na nguvu zisizoonekana.

iii) Mkakati wa kutimiza ushindi katika tukio.
a) Mpaka naandika, tukio lile tulikuwa tumefika hatua ya pili, hivyo iliyokuwa inasubiriwa ni hatua ya tatu.
Hatua ya Kwanza ilikuwa kudai Hali yetu Kwa hiyari na Amani pasipo kutumia nguvu, hatua ya pili ni kuongeza shinikizo Kwa tajiri Kwa kumpa Alert kuwa Uvumilivu wetu umefika mwisho, hatua ya tatu ni kufuata sheria za kibinadamu kadiri ya zilivyowekwa na mawazo ya kibinadamu Hii itahusisha kuchukua Maoni na mawazo ya Watu wa karibu kuhusiana na tukio lenyewe, pili kuunda kamati ya kushughulikia Jambo Hilo, kisha kamati itatafuta Kampuni nzuri ya Wanasheria na mawakili watakaohakikisha kila kitu kinaenda Sawa. Hapo tayari Bajeti ishapangwa na Kamati.

b) Kuwa na ulinzi na tahadhari Kwa namna yoyote Ile.
Tayari nimeshatishwa hivyo sipaswi ku-relax na kuishi kama awali. Ingawaje muda wote ni mtu wa tahadhari.

Ikiwa Njia ya sheria na Mahakama ingeshindikana nini kitafanyika?
Tayari majibu yalikuwa kwenye Kamati,
Kamati ilihusisha Wahusika wenye uwezo katika Nyanja muhimu, kama Sheria na mambo ya Mahakama,
Pili, ulinzi na usalama wangu binafsi
Tatu, Njia mbadala endapo Njia za kawaida zitashindikana.

Kwenye ulinzi na usalama, tukakubalina ninatakiwa niondoke kwenye eneo lake, hata wanasheria walinitaka nifanye hivyo.
Pili, nimpe angalau mwezi mmoja wa mwisho ili anilipe Pesa yangu na kama hatalipa hatua zingine ziendelee,
Nikafanya hivyo, Wakati huo nimeshaondoka eneo lake la kazi.

Wakati huo wenzangu walishakata tamaa kabisa, na walishamuachia Mungu.
Kuna Baba mmoja tuliyekuwa tunafanya kazi wote, umri wake ni kama miaka 44 hivi yeye alinishangaza aliponiambia ATI yeye kazoea kudhulumiwa.

Mimi nikamuambia, siwezi kukubali kazi hizi za mwanzomwanzo kudhulumiwa nisije jipa mkosi wa Maisha. Mimi bado ni kijana mdogo, nikianza na kudhulumiwa ni kujiharibia CV na Falsafa ya Maisha.
Nikamuambia wewe kama umezoea kusamehe Jasho lako Mimi sitoweza kujidharau. Ndio maana ninakuwa mwaminifu ninapopewa kazi ya MTU.

Nikawaambia nimetafuta kampuni la sheria litakaloshughulikia Jambo letu. Kwa sababu kampuni hilo ni ndugu zangu wamesema watatusaidia Kwa gharama nafuu. Hivyo ninyi mtakachokifanya ni kutoa Pesa ya Wakili kila kesi itakapotajwa. Nikawatajia kiwango, tukaenda Posta kwenye Ofisi ya Kampuni Ile, kisha tukakubalina.
Shida ikaja kuwa wafanyakazi wengine wakawa wameona tunapoteza nguvu na Pesa Bure kwani Kwa uzoefu wao na umri wao waliwahi kufanya hivyo wakashindwa.

Nikawaambia mlishindwa Kwa sababu hamkutaka kushinda. Mngekaza kivyovyote vile. Kupokea milioni 10 sio Jambo Dogo, hivyo lazima ulitolee Jasho.
Wakaondoka watatu tukabaki watatu.
Ingawaje majina Yao walioondoka tuliona yawepo tuu.
Shida ilikuja kuwa wale wenzangu walikuwa na familia na Hawana Pesa, hivyo Mimi ndio ilinibidi niwe natoa Pesa Kutoka kwenye kibiashara changu kumlipa Wakili kila atakapopanda.

Tulimtumia Barua ya wito kupitia Sanduku la posta la Ile kampuni yake, hakutokea siku ilipotajwa,
Mahakama ikatuomba tumpelekee tena Barua nyingine ya Wito, lakini safari Hii tuipeleke Kwa mkono(Physically)
Tukaenda, nikashauri tupitie serikali za mitaa ya anapoishi kisha mwenyekiti au mtendaji ndio atupeleke, tukafika ofisi za serikali za mtaa, tukamsihi mtendaji tuambatane naye, lakini akatupa msaada wa mlinzi(mgambo) atupeleke, tukasema sio kesi.

Tumefika, tukasema tusigonge Kwanza tuangalie mazingira tuone yanaonyesha nyumba inamtu au haina, maana lile Geti lake Lina kamera hivyo MTU akiwa ndani anaweza kutuona, na kama atatuona anaweza kukataa Kutoka na Sisi tutaona hayupo, lakini tukagundua mule ndani kuna chumba cha mlinzi.
Tukamuagiza Mfanyakazi mwenzetu wa kike akagonge.
Yule mlinzi akachungulia kwenye sehemu ya Geti iliyowekwa maalumu Kwa kuchungulia, alipomuona ni Mwanamke akafungua MLANGO.
Mdada akajitambulisha, lakini hakusema ukweli kuhusu mambo ya Kazi na madai.
Mlinzi pasipokujua akasema Boss yupo,

Akaombwa amuite, akamuita. boss akashuka Chini Kwa sababu nyumba ni ya ghorofa moja. Akashtuka kutukuta pale.
Kisha mume WA boss naye Kwa bahati nzuri akaja na Gari akitokea mizunguko yake.
Baada ya mazungumzo Yule Mume WA boss akauliza,
Hizi karatasi mmezitoa wapi?
Tukamjibu anachotakiwa kukifanya NI kusaini kuwa ameipokea. Jina la kampuni la sheria lilimtisha.

Kisha akasema,
Hapa Robert ni yupi?
Kwa sababu hakuwahi kunijua Kwa sababu yeye hahusiki zaidi na Ile kampuni tuliyokuwa tunaifanyia kazi.
Alipoonyeshwa Robert ni Mimi akashangaa Sana.

Mume WA boss; Aisee! Mbona ni kijana mdogo Sana.
Unajiamini Sana Bwana Mdogo, kipi kinakufanya ujiamini?

Mimi; swali Hilo hukuwahi kuniuliza wewe wala Mkeo kipindi nikiwa nawafanyia kazi.
Linapokuja swala la Haki na Ukweli ni kawaida Robert Kujiamini.

Mume wa Boss; Vizuri Sana. Ila Hii ni hatari endapo utakutana na watu wabaya na MAKATILI. Huogopi.
(Aliniuliza akiwa anapima kina cha uelewa wangu na ujasiri wangu Kwa Yale ninayoyaamini)
Mimi; Sisemi kuwa siogopi nitakuwa naongopa, Ila pia siogopi kushughulika na wanaoninyima Haki zangu hasa zile kubwakubwa,

Akakataa kuipokea barua Ile ya Wito. Huku akitutaka tuwe wavumilivu ndani ya wiki moja atatulipa fedha zetu. Alituomba na kutusihi Sana.
Lakini nikamwambia Kwa tulipofikia maneno pekee yake hayatasaidia hapa.

Mkewe alikuwa mkimya tofauti na tulivyomzoea.
Nikamwambia "wewe si ulisema hata twende Polisi au Mahakamani hutonipa Pesa yangu.
Sasa nataka nianzie hukohuko uliposema ili nipime ukweli WA maneno yako.
Alafu ikishindikana Huko ndio utajua kuwa zipo Njia elfu elfu za mtu kujipatia Haki zake. Subiri utajionea na kila tunavyopanda kwenye hatua zinazofuata ndio ugumu na madhara yanaongezeka na Wahusika wataongezeka"

Kuifanya Stori kuwa fupi,
Baada ya wiki mbili Nikiwa kwneye kibiashara changu simu yangu ikaita, ilikuwa namba ngeni, nikapokea,
Aliyekuwa anaongea na Mwanamke ambaye ni boss wetu.

Boss; Niweke Pesa kwenye Akaunti yako ya Benki ileile?
Mimi: Unaweka kiasi gani? Maana tayari haya mambo yameshafika Mahakamani na kiwango cha Pesa ulikiona pamoja na Fidia ya usumbufu na gharama za kuendesha kesi.
Boss; Robert nakuomba niwalipe zile mnazonidai, nimepitia kipindi kigumu Sana kifedha hata Mungu anajua, hizi zenyewe nimezikopa sehemu Fulani ili niwalipe nyie.
Bla!blah! blah!"

Aliongea Kwa uchungu, binafsi nilimuelewa, lengo langu halikuwa kumkomoa, lengo langu lilikuwa Kupata Haki yangu, kilichochangu.

Mimi; Waingizie wengine Pesa zao, Mimi niwe wamwisho, maana kama nilivyokuahidi zakwangu utatoa tuu iwe wewe au familia yako.

Boss: Kwa nini unawahangaikia hao, hawatakusaidia kitu chochote. Usipende kuwasaidia Saidia Watu. Watu ni wabaya.

Mimi: Walipe Kwanza kisha utanipigie kunipa hayo mahubiri. Kwa jinsi ulivyowafanyia ubaya na kunifanyia Mimi sidhani kama unaweza kuwa mshauri wangu WA nini nifanye na kipi nisifanye.

Akawatumia, nikawauliza wakasema wameingiziwa Pesa zao. Kisha nami nikatumiwa pesa yangu.

Baada ya hapo nilitegemea kuwa zilepesa ambazo tulikubaliana kuwa watanilipa Kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa namlipa Wakili, na ishu za usafiri Kwa wale wengine kufuatilia mambo ya kesi ambalo lilikuwa jukumu lao, hawakunilipa

Wala kunipigia simu kunishukuru Kwa jinsi nilivyohangaika kwaajili Yao,
Fikiria MTU analipwa milioni 11 alafu anashindwa kutoa hata elfu 50 tuu ya Ahsante Kwa aliyempigania apate hizo Pesa.

Nikachukua simu, Kwa bahati nzuri huwaga sio mtu wa kunyamazia mambo.
Nikawapigia, baadhi walipokea wengine hawakupokea tangu siku waliyolipwa.
Nikawaambia kwenye Maisha wanapaswa kuwa na Shukrani ili wasiishie Kupata msaada mmoja tuu.

Baadaye, Yule boss wa kike alianzisha kampuuni nyingine 2021 akataka niwe sehemu ya hiyo kampuni, nikakataa Kwa kumueleza kuwa sasa hivi ninashughulika na vijibiashara vyako ingawaje bado ni vidogo.
Alijitahidi kuniweka karibu lakini Imani yangu kwake ilipotea, wengine tunaamini mara moja Ila tunaouwezo WA kupenda zaidi ya mara moja.

Nilichojifunza kuhusu mkasa ule;
I) Kudai haki kunahitaji Subira na ujasiri
ii) Usaliti kwenye Kudai haki ni Jambo la kawaida.
iii) Wazazi wangu hawakuwa tayari niendelee kufuatilia mambo ya makesi walisema nimuachie Mungu.
Nikawaambia Mungu hakufanya kazi aliyefanya kazi ni Mimi.
Nikawaambia wajiandae Kwa lolote.
Nikajifunza kuwa Vijana wengi hupoteza ujasiri na Haki zao Kutokana na Wazazi na watu wao wakaribu.

iv) Ukubwa WA pua sio wingi wa makamasi. Walioondoka wote walikuwa Watu wazima above 40, wao walimuachia Mungu.

v) Tenda Wema bila kutegemea Shukrani.
Binadamu wengi ni wabinafsi.

Jamii ikiwa na kizazi jasiri, dhulma na uonevu vitapungua Sana.

Watu hawaonewi na kudhulumiwa Kwa umaskini wao Bali wanaonewa na kudhulumiwa Kutokana na woga na mtizamo wao Mbaya kuhusu matajiri.

Kizazi cha kuonewa ndicho huunda serikali yenye viongozi waonevu na wenye dhulma.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Sijaona Uchambuzi wowote badala yake nimeona kisa chako na tajiri yako. Mfano wa kisa chako imechukua robo tatu ya andiko lote la kile unachokiita Uchambuzi.

Uchambuzi ungejikita katika kung'amua ukweli wa taarifa iliyowasilishwa. Mwenye makosa na kitu Gani kifanyike ili haki ya Mhusika (Eliudi au Salaah) ipatikane.

Anyway, tunashukuru kwa kisa chako Mkuu.
 
Sijaona Uchambuzi wote badala yake nimeona kisa chako na tajiri yako. Mfano wa kisa chako imechukua robo tatu ya andiko lote la kile unachokiita Uchambuzi.

Uchambuzi ungejikita katika kung'amua ukweli wa taarifa iliyowasilishwa. Mwenye makosa na kitu Gani kifanyike ili haki ya Mhusika (Eliudi au Salaah) ipatikane.

Anyway, tunashukuru kwa kisa chako Mkuu.

Mkuu kisa changu ndio uchambuzi wa kisa cha huyo kilichotokea.
Hakuna atakayetoa uchambazi zaidi ya huo.

Hatua za kuchukua zipo kwenye kisa changu.
Hata hivyo ninahofu kuwa kama tuhuma nyingin zimejikita kwenye shughuli haramu sio rahisi MTU kufikishwa Mahakamani.

Huyo anasema Polisi wamekataa kufungua faili dhidi ya huyo Saalah.
Hivi Kwa MTU aliyekuwa anamiliki zaidi ya mamilioni ya fedha zaidi ya 500M anakosaje Wanasheria?
Anashindwaje kuipeleka kesi yake Kwa Makampuni ya sheria yamejaa kibao hapa mjini. Anashindwa kuwapa kazi hiyo kama kweli kesi yake ni halali?

Ingekuwa kesi imeletwa na MTU ambaye hajawahi kushika hata milioni 5 tungesema labda hana Pesa au connection ya hao wanasheria.

Hiyo ndio shida ya kujihusisha na Michezo michafu inakuwa ni ngumu kufuatilia Haki zako.
Humo humo serikali kuna genge la wahalifu na kuna genge la wapenda Haki.
 
Niliachia kusoma pale eti walilazimika kumpelekea 80m Tsh na 90 m kwa sababu zipi na wapi yaani pesa halal kabisa unaweza kumpelekea mtu kienyeji hivyo huyo jamaa anaweza kuwa mtu mbaya ila huo ubaya wameutengeza hao wanaomchangia mamilioni nyumbani kwake...biashara ya hela nyingi bila wanasheria wala bank inafanyika kienyeji mimi nina uzoefu na Kariakoo kwa hiyo hapo pana miguu bado kaikumbatia mtoa mada wacha tuendelee kutafuna popcorn..
 
Mtu aliyezizoea milioni 100 anashindwaje Kutumia Makampuni ya sheria yaliyojaa nchi nzima?

Tatizo ni yeye aliyeanza kumdhulumu mwenzake Kwa kisingizio cha Pesa zimeibiwa,
Sasa mwenzake kachukua mpaka riba.
 
Mie nasema huyo Eliud angekutana na mimi angenichukia yeye, watoto wake na vizazi vingine viwili.

Huwezi poteza hela kiasi hicho recklessly kabisa.

Waarabu wanaendelea kwa sababu wako strict na principle zao kwenye biashara. Nenda uarabuni utaona makampuni mengi ni yao lkn hawaendeshi wao, ila wanaowasaidia kuyaendesha wanajua kabisa jamaa hawataki mchezo na mali zao. Sasa wabongo badala ya kuiga hio mentality tunakuja kujivika unyonge kutafuta haki za kipuuzi baada ya kufanya upuuzi. Kama uliiba jipange kulipa hela au pumbu zako zifanyishe mazoezi mapema
 
Kwema Wakuu!

Nilikuwa nafuatilia mkasa uliokuwa umeletwa siku tatu nyuma na ndugu nokwenumuya, akiwasilisha malalamiko yake kuhusu uonevu na dhulma inayofanywa na tajiri mmoja aliyemtambulisha Kwa jina la Saalah Dhidi ya Eliud.
Nikaona nitoe uchambuzi Kwa uchache ili kama taifa tuwezi kujifunza na kujua ni vipi tunatoka.
Haya tusipoteze muda;

I) Ukiona sehemu yoyote au nchi yoyote inadhulma au uonevu basi kosa sio la hao wadhulumaji Bali kosa ni la viongozi na watendaji WA serikali.
Ni ngumu na nadra Sana kukuta dhulma au uonevu kwenye taifa linaloongozwa na viongozi wenye kupenda Haki.

Matajiri na watu mashuhuri ukiona wanauthubutu wa kukudhulumu na kukuonea wala usiwalaumu wao, wakulaumiwa na viongozi na watendaji wanaoongoza,

ii) Watanzania wengi wanapenda kutia wenzao hasara alafu wakiambiwa walipie hiyo hasara wanaona wanaonewa na kudhulumiwa.
Watanzania wengi ni Wezi, wanatabia za udokozi dokozi, alafu siku ukimshika ukimuambia Lipa anaona tabu, ukitumia mabavu anasema unamuonea na kumdhulumu.
Na Kwa vile yeye ni mnyonge basi wenye Akili kama zake ambao ndio wengi watamuonea huruma na kukuchukulia wewe unaroho Mbaya Kwa kudhulumu Watu.

iii) Watanzania wengi ni Wanafiki, watasema mambo mabaya ya MTU Baada ya kugombana lakini Kabla hamjagombana naye anakuwa sehemu ya ushiriki WA hayo mabaya.
Mtanzania unaweza shiriki naye madili Fulani haramu akakaa kimya Kwa sababu naye anapatamo kitu lakini siku mkipishana na kutofautiana Kwa vile hapati chochote na yupo nje ya mfumo ndio atajifanya anayasema mabaya ya eneo Fulani.

Watu wa namna hiyo Mimi kama Taikon huwaga siwasikilizi na wala kuwatetea Kwa chochote kile, zaidi ningekuwa serikalini ningewatia ndani, Kwa sababu wanatabia ya unafiki na usaliti.

Hata kwenye viongozi wanatabia Hii, akiwa Waziri au sehemu ya uongozi, anakaa kimya mabaya yakifanyika iwe hadharani au Kwa Siri, alafu likiondolewa unakuta linaanza kupiga Kelele.
Unafiki na usaliti ni tabia ya Watu wahalifu na waovu.

Kwa kesi ya Saalah na Eliud, huyo Eliud miaka yote ameshiriki kufanya uhalifu na Hilo genge analolituhumu lakini alikaa kimya, Leo Baada ya kupishana na naye kufikikiwa na michezo hiyo michafu ndio anapiga mayowe.

Taikon huwaga nasemaga, Usisaidie Maskini iwe Maskini wa Kifikra, kiuchumi au whatever, Kwa sababu Tabia nyingi za Maskini wengi ni Mbaya.

iv) Wanaoonewa na kudhulumiwa ni Watu wasiojasiri.
Kimsingi Mimi Pesa yangu huwezi kuila kienyeji, tena kimabavu ndio kabisa haiwezekaniki. Iwe Kwa damu au roho jua au Mvua hilo halitowezekana Dunia ingalipo.
Hutoweza kunidhulumu Kwa sababu sitokudhulumi na siwezi dhulumu cha MTU. Hivyo endapo utanidhulumu tena kimabavu Kwa kisingizio chochote kile labda ATI umenizidi uwezo wa kifedha, kihashi na kicheo au kimamlaka basi jua kuwa umeingia kwenye vita nzuri Sana.

Sisi ni Watu ambao hatumuachii Mungu,

Acha niwape kisa kimoja kilichotokea miaka ya 2019 kinanihusu Mimi mwenyewe;

Watanzania wengi ni Watu waoga waoga Sana. Niliwahi kufanya kazi sehemu Fulani hapa Dar, ndio nikagundua Watanzania wengi ni Watu waoga kudai Haki zao nafikiri ni Kwa sababu wengi sio waaminifu.

Mimi ninaamka na ninakuja Kwa wakati kazini, ninakufanyia kazi zao vizuri, matunda ya Kazi yanaonekana, hujawahi nilalamikia Kwa chochote, kama nimekuwa mwaminifu kwako Kwa kiwango cha 100% basi elewa kuwa utakapo nizingua nitakuwa mwaminifu Kwa asilimia zilezile 100% kukulipa unayonifanyia bila kujali Matokeo.

Yule Tajiri akapata Crisis ya kiuchumi ila hakutuambia Sisi wafanyakazi wake, hivyo akawa analipa baadhi ya wafanyakazi ikiwemo Mimi Ila wengine akawa anashindwa kuwalipa, wale ambao hawakulipwa walifikisha miezi mitatu na ndipo nami akashindwa kunilipa. Mpaka taasisi inafungwa Mimi sikulipwa Kwa miezi mitatu, huku wenzangu wakiwa hawajalipwa miezi sita.

Nilikuwa ninabiashara zingine hivyo sikuwa naitegemea Sana Ile Pesa.
Akatupiga Kalenda wee, Mimi nikawa namuelewa, tulikuwa tunaishi kwenye compound ya Kampuni, tukashangaa siku moja wamekuja Mapolisi Wawili wakiwa na Sare, wakatuambia kuwa ATI kuna kitu kimeibiwa kwenye Ile Compound ya Kampuni, na washukiwa WA wizi huo ni Sisi.

Mimi; Wewe unajua Sisi humu ndani tupo wangapi na ni kina Nani? Maana ninyi mmesema ni Polisi.
Polisi: hatujui ninyi ni kina Nani
Mimi:. Kama hamjui Sisi ni kina Nani, bila Shaka pia hamjui Kwa nini tupo ndani ya eneo hili, si ndio?,
Polisi: wewe mbona unajifanya Mjuaji, Sisi hatutaki tutumie nguvu,
Mimi: Kutumia nguvu ya nini, mnaweza onyesha uhalali WA ninyi kuwa hapa?

Polisi: unasikia wee, usijiingize kwenye matatizo (akaongea Polisi wa pili)
Mimi: Kwa hiyo Mwenye kampuni ndio amewatuma ili mje kututisha? Yeye tunayemdai hatujampeleka Polisi wala serikali kwani tulichukulia Hii ishu itaisha Kwa Amani lakini yeye kawaita ninyi polisi(nikacheka)
Mimi: Mlivyopita pale getini hamkuona Mlinzi? Yeye kazi yake ni kulinda Mali zilizomo humu, yeye ndio wakuulizwa vitu vilivyopotea. Sisi sio walinzi WA eneo hili.

Hapo tukaanza kujibishana hovyohovyo. Huku wafanyakazi wenzangu walionizidi wakinizuia nisijibishane nao kwani nitajipata kwenye matatizo.
Nikawaambia huwaga sioni Shida kujipata kwenye matatizo nikiwa napigania Haki zangu. Ikiwezekana hata Kufa au kuuana hiyo kwangu sio Shida.

Sasa ukiongea maneno haya lazima Watu wakutazame Kwa Makini alafu walinganishe maneno yako na vile unavyoonekana😂😂. Sasa muonekano wangu ulikuwa mbali Mno na maneno yangu. Walikuwa wakiniona kama kijana mpole mwenye uso mtulivu na pengine barubaru. Lakini walisahau kuwa Sura sio Roho.

Nikachukua simu nikampigia Yule Tajiri, akapokea,
Mimi: Shikamoo Boss, Kwa kweli leo umefanya Jambo la ajabu Sana. Sisi tunayekudai hatujakuletea polisi, hatujaenda hata serikali za mitaa, wala hatujaenda hata Mahakama za usuluhishi kukushtaki, tumekuvumilia Kwa sababu tunaroho ya Mungu juu yetu, wewe mwenyewe ndio ulituambia tubaki humuhumu ndani ya compound yako mpaka utakapotulipa pesa zetu, ukasema ndani ya miezi miwili utafanikisha Hilo, huu ni mwezi wa tatu hujafanya hivyo, lakini tumekuwa Wema kwako, hatujakutukana wala kusema neno lolote baya juu yako"

" Wala kukushtakia popote pale hata Kwa Mungu hatujasema neno lolote zaidi ya yote tunakuombea ili mambo yako yafanikiwe ili utulipe Pesa zetu ili tusiachane Kwa kinyongo. Leo hii unatuletea polisi!! Sisi Leo tumekuwa Wezi? Baada ya kukutumikia Kwa uaminifu wote leo hii Sisi tumegeuka Wezi? (Nikacheka)"

"Nimewapa Leo na kesho tuu muondoke hapo, nataka kufanya shughuli zingine. Pesa zenu mtapewa"
Yule Tajiri Mwanamke akasema,

Mimi: sasa kama ulikuwa unataka tuondoke si ungetuambia tuu. Ulifikiri kila MTU anaogopa Polisi? Ulidhani tutatishika?
Haujafanya Fair kabisa,
Boss hivi unawafukuza Watu ndani ya siku Mbili wawe wameondoka, hivi haujui humu kuna wanaume na familia zao wameziacha mkoani, wengine Mwanza, wengine Musoma, na wengine Dodoma.
Hawa wote wanafamilia, Nauli Watatoa wapi? Na wakifika majumbani mwao mikono mitupu ilhali walikufanyia kazi unafikiri hiyo imekaaje?

Kwa udhalimu ulioufanya ninauhakika utaulipia tuu kivyovyote vile"

Hapo akakasirika Sana, akaanza kunijia juu huku akionyesha kiburi chake;
Tajiri Mwanamke: Nisikilize Robert, Kwa vile unajifanya Mjuaji Pesa zako sitakupa, nitawapa wenzako Ila wewe sitakupa, wewe si unajifanya mjuaji, tuone Nani ataumia, nenda polisi, nenda Mahakamani, nenda popote lakini Pesa yako sitakupa, alafu tuone utafanya nini.

Mimi: (Nikacheka) unafikiri kila mtu anamawazo kama yako, Mimi jasho langu halijawahi kuliwa popote pale. Pesa yangu lazima uitoe, simu hii nimekupigia ili uwalipe hawa wenzangu pesa Yao maana yangu ninauhakika 100% utaitoa tuu.
Kama nilivyokuwa mwaminifu kukufanyia kazi na hata wewe ni shahidi vivyohivyo nitakuwa mwaminifu kuhakikisha utailipa Pesa yangu, utaamua mwenyewe uilipe Kwa namna gani Kwa nguvu au Kwa hiyari, Kwa jasho au Kwa damu, wewe au Watoto wako. Kwa sababu mchuma janga hula na wakao. Kwa vile wewe umekuwa dhalimu na hiyo Pesa ninauhakika umekula na familia yako, hivyo lazima nao wahusike"

Kufikia hapo akakata simu,
Wale Polisi wakawa wananitazama, na wafanyakazi wenzangu wakawa wananishangaa.

Polisi: Sasa Ndugu huoni hiyo inaweza kuwa shida kwako kama wakiamua kukupeleka Mahakamani? Fuatilia mambo haya polepole yanaweza kukuletea matatizo
Mimi: ninyi polisi ni Vijana wadogo Kwa mnavyoonekana, nafikiri tupo rika Sawa.
Msipende kuingilia mambo yasiyowahusu hasa yanayohusu jasho la Watu... Huo ni ushauri tuu nawapa, mnahiyari ya kuupokea au kuukataa.

Mara simu yangu inaita Kwa namba ngeni. Napokeo simu,
Mimi: Hello
Unknown; Hello, naongea na Mr. Robert
Mimi; Ndio, Nani mwenzangu?
(Anajitambulisha)
Mimi: Ndio Mume wa Boss,
Mume wa Boss: Tafadhali nakuomba usiingize familia kwenye mambo yenu.
Vinginevyo nitakufanya kitu kibaya hutokuja kusahau.

Mimi: sasa Kaka mkubwa, Mimi nikifikiri Kwa kuwa wewe NI mwanaume utakuwa na hekima angalau kidogo lakini kumbe wewe ndiye mpumbavu Kabisa.
(Ananikatisha lakini NAMI nakazana) sikiliza... Sikia.... Sikiliza...( Anaamua kutilia)

Mimi: nilitegemea ungeniambia, Bwana Mdogo huna haja ya kupaniki, tunajua tumechelewa kuwalipa Kwa wakati hivyo tunaomba Radhi, lakini tutawalipa ndani ya muda mfupi, jukumu hilo nitalifuatilia mwenyewe kuhakikisha mnalipwa Pesa zenu. Huna haja ya kufikia kuingiza wasiohusika kama Familia.

Mimi: Hivyo tuu ningekuona unaakili. Lakini Kwa vile ni mjinga unadhani Vitisho vyako ndio Suluhu ya Jambo hili. Nisikilize (nataja jina lake) katika Jambo hilo ninakuhakikishia hakuna atakayekusaidia, labda sio Mimi. Kama unafikiri kuna msaada nakuhakikishia hautaupata.

Mume wa Boss: utanifanya nini wewe kapuku? Kwani hamna kwenu, ondokeni hapo, usitake nikufanye kitu mbaya.

Mimi: Kitu kibaya zaidi ya kunicheleweshea Pesa yangu sidhani kama unazaidi.
Watoto wa WENZENU wanapata shida Kwa sababu Baba zao hamuwapi pesa, huyu mmoja MKE wake alijifungua kidhalili na Kwa kusikitisha kisa udhalimu wenu, lakini ninyi hamtaki familia zenu ziumizwe Kwa Makosa yenu, Watoto wenu wacheke, wafurahie Maisha, wasome shule nzuri kisa na mkasa ninyi ni maboss, kipimo mlichotupimia ndicho hichohicho nitakachokitumia. Kwa Njia ipi subirini mtaona"

Nikakata Simu.
Akapiga, nikakata, akapiga nikakata tena.
Kisha simu ya polisi mmoja ikaita, akapokea, Yule polisi akaambiwa maneno Fulani ambayo nilikuja kuyaelewa kuwa ameambiwa anipe simu.

Mimi: Nini?
Polisi: Ongea naye
Mimi: Nani?
Polisi: Boss wako.
Mimi: wewe si ulisemwa haukutumwa na Boss, huyo boss amepata wapi namba zako? Kwa hiyo wewe haukutumwa na mkuu wako WA kituo? (Nikawa nasoma Kwa Sauti namba na jina lilikuwa kwenye Beji ya kwenye Shati lake)
Polisi: Amekataa, ngoja tuwaachie mambo yenu.

Wale Polisi wakaondoka, lakini tayari nilikuwa nimechukua namba na majina Yao. Nikayafuatilia majina Yao. Nikagundua Yule polisi aliyekuwa anaongea na kufokafoka Sana alikuwa ni mdogo wake na Mume WA Boss wetu(yaani shemeji wa Boss).

Wenzangu (walikuwa watano) wakaingiwa na hofu. Wakaazimia kuondoka kesho yake.
Kwa upande wangu sikutaka kujihakikishia najiamini Sana, sikutaka kupuuzia vitisho nilivyopewa. Nilijua ninatakiwa kuchukua hatua kadhaa,
Nikachukua Dairy yangu nikaandika tukio la siku Ile Kwa ufupi mambo muhimu kama Siku, Tarehe, masaa, mazingira, Wahusika na majina Yao, baadhi ya maneno, kisha Ile Record nikaiweka kwenye Memory card yangu ya akiba ambayo huwaga naiwekaga sehemu maalumu.

Kilichofuata, ni kuchukua Daftari jingine na kuunda Mpango mkakati wa kukabiliana na tukio lililokuwa linaendelea,
I) tukio lilipoanzia, sehemu lilipo na upi mwelekeo.
ii) Rasilimali zipi nilizonazo naweza kuzitumia kukabiliana na ishu hii;
a) kiasi cha fedha nilichonacho,
Nilikuwa na kiasi kidogo cha fedha kama milioni tano tuu😀😀
b) Rasilimali Watu.
Ni Wahusika gani waingie katika tukio Hili, kila mhusika na Role yake, hapa bila Shaka kuna Wazazi, baadhi ya Ndugu, na wanasheria pamoja na nguvu zisizoonekana.

iii) Mkakati wa kutimiza ushindi katika tukio.
a) Mpaka naandika, tukio lile tulikuwa tumefika hatua ya pili, hivyo iliyokuwa inasubiriwa ni hatua ya tatu.
Hatua ya Kwanza ilikuwa kudai Hali yetu Kwa hiyari na Amani pasipo kutumia nguvu, hatua ya pili ni kuongeza shinikizo Kwa tajiri Kwa kumpa Alert kuwa Uvumilivu wetu umefika mwisho, hatua ya tatu ni kufuata sheria za kibinadamu kadiri ya zilivyowekwa na mawazo ya kibinadamu Hii itahusisha kuchukua Maoni na mawazo ya Watu wa karibu kuhusiana na tukio lenyewe, pili kuunda kamati ya kushughulikia Jambo Hilo, kisha kamati itatafuta Kampuni nzuri ya Wanasheria na mawakili watakaohakikisha kila kitu kinaenda Sawa. Hapo tayari Bajeti ishapangwa na Kamati.

b) Kuwa na ulinzi na tahadhari Kwa namna yoyote Ile.
Tayari nimeshatishwa hivyo sipaswi ku-relax na kuishi kama awali. Ingawaje muda wote ni mtu wa tahadhari.

Ikiwa Njia ya sheria na Mahakama ingeshindikana nini kitafanyika?
Tayari majibu yalikuwa kwenye Kamati,
Kamati ilihusisha Wahusika wenye uwezo katika Nyanja muhimu, kama Sheria na mambo ya Mahakama,
Pili, ulinzi na usalama wangu binafsi
Tatu, Njia mbadala endapo Njia za kawaida zitashindikana.

Kwenye ulinzi na usalama, tukakubalina ninatakiwa niondoke kwenye eneo lake, hata wanasheria walinitaka nifanye hivyo.
Pili, nimpe angalau mwezi mmoja wa mwisho ili anilipe Pesa yangu na kama hatalipa hatua zingine ziendelee,
Nikafanya hivyo, Wakati huo nimeshaondoka eneo lake la kazi.

Wakati huo wenzangu walishakata tamaa kabisa, na walishamuachia Mungu.
Kuna Baba mmoja tuliyekuwa tunafanya kazi wote, umri wake ni kama miaka 44 hivi yeye alinishangaza aliponiambia ATI yeye kazoea kudhulumiwa.

Mimi nikamuambia, siwezi kukubali kazi hizi za mwanzomwanzo kudhulumiwa nisije jipa mkosi wa Maisha. Mimi bado ni kijana mdogo, nikianza na kudhulumiwa ni kujiharibia CV na Falsafa ya Maisha.
Nikamuambia wewe kama umezoea kusamehe Jasho lako Mimi sitoweza kujidharau. Ndio maana ninakuwa mwaminifu ninapopewa kazi ya MTU.

Nikawaambia nimetafuta kampuni la sheria litakaloshughulikia Jambo letu. Kwa sababu kampuni hilo ni ndugu zangu wamesema watatusaidia Kwa gharama nafuu. Hivyo ninyi mtakachokifanya ni kutoa Pesa ya Wakili kila kesi itakapotajwa. Nikawatajia kiwango, tukaenda Posta kwenye Ofisi ya Kampuni Ile, kisha tukakubalina.
Shida ikaja kuwa wafanyakazi wengine wakawa wameona tunapoteza nguvu na Pesa Bure kwani Kwa uzoefu wao na umri wao waliwahi kufanya hivyo wakashindwa.

Nikawaambia mlishindwa Kwa sababu hamkutaka kushinda. Mngekaza kivyovyote vile. Kupokea milioni 10 sio Jambo Dogo, hivyo lazima ulitolee Jasho.
Wakaondoka watatu tukabaki watatu.
Ingawaje majina Yao walioondoka tuliona yawepo tuu.
Shida ilikuja kuwa wale wenzangu walikuwa na familia na Hawana Pesa, hivyo Mimi ndio ilinibidi niwe natoa Pesa Kutoka kwenye kibiashara changu kumlipa Wakili kila atakapopanda.

Tulimtumia Barua ya wito kupitia Sanduku la posta la Ile kampuni yake, hakutokea siku ilipotajwa,
Mahakama ikatuomba tumpelekee tena Barua nyingine ya Wito, lakini safari Hii tuipeleke Kwa mkono(Physically)
Tukaenda, nikashauri tupitie serikali za mitaa ya anapoishi kisha mwenyekiti au mtendaji ndio atupeleke, tukafika ofisi za serikali za mtaa, tukamsihi mtendaji tuambatane naye, lakini akatupa msaada wa mlinzi(mgambo) atupeleke, tukasema sio kesi.

Tumefika, tukasema tusigonge Kwanza tuangalie mazingira tuone yanaonyesha nyumba inamtu au haina, maana lile Geti lake Lina kamera hivyo MTU akiwa ndani anaweza kutuona, na kama atatuona anaweza kukataa Kutoka na Sisi tutaona hayupo, lakini tukagundua mule ndani kuna chumba cha mlinzi.
Tukamuagiza Mfanyakazi mwenzetu wa kike akagonge.
Yule mlinzi akachungulia kwenye sehemu ya Geti iliyowekwa maalumu Kwa kuchungulia, alipomuona ni Mwanamke akafungua MLANGO.
Mdada akajitambulisha, lakini hakusema ukweli kuhusu mambo ya Kazi na madai.
Mlinzi pasipokujua akasema Boss yupo,

Akaombwa amuite, akamuita. boss akashuka Chini Kwa sababu nyumba ni ya ghorofa moja. Akashtuka kutukuta pale.
Kisha mume WA boss naye Kwa bahati nzuri akaja na Gari akitokea mizunguko yake.
Baada ya mazungumzo Yule Mume WA boss akauliza,
Hizi karatasi mmezitoa wapi?
Tukamjibu anachotakiwa kukifanya NI kusaini kuwa ameipokea. Jina la kampuni la sheria lilimtisha.

Kisha akasema,
Hapa Robert ni yupi?
Kwa sababu hakuwahi kunijua Kwa sababu yeye hahusiki zaidi na Ile kampuni tuliyokuwa tunaifanyia kazi.
Alipoonyeshwa Robert ni Mimi akashangaa Sana.

Mume WA boss; Aisee! Mbona ni kijana mdogo Sana.
Unajiamini Sana Bwana Mdogo, kipi kinakufanya ujiamini?

Mimi; swali Hilo hukuwahi kuniuliza wewe wala Mkeo kipindi nikiwa nawafanyia kazi.
Linapokuja swala la Haki na Ukweli ni kawaida Robert Kujiamini.

Mume wa Boss; Vizuri Sana. Ila Hii ni hatari endapo utakutana na watu wabaya na MAKATILI. Huogopi.
(Aliniuliza akiwa anapima kina cha uelewa wangu na ujasiri wangu Kwa Yale ninayoyaamini)
Mimi; Sisemi kuwa siogopi nitakuwa naongopa, Ila pia siogopi kushughulika na wanaoninyima Haki zangu hasa zile kubwakubwa,

Akakataa kuipokea barua Ile ya Wito. Huku akitutaka tuwe wavumilivu ndani ya wiki moja atatulipa fedha zetu. Alituomba na kutusihi Sana.
Lakini nikamwambia Kwa tulipofikia maneno pekee yake hayatasaidia hapa.

Mkewe alikuwa mkimya tofauti na tulivyomzoea.
Nikamwambia "wewe si ulisema hata twende Polisi au Mahakamani hutonipa Pesa yangu.
Sasa nataka nianzie hukohuko uliposema ili nipime ukweli WA maneno yako.
Alafu ikishindikana Huko ndio utajua kuwa zipo Njia elfu elfu za mtu kujipatia Haki zake. Subiri utajionea na kila tunavyopanda kwenye hatua zinazofuata ndio ugumu na madhara yanaongezeka na Wahusika wataongezeka"

Kuifanya Stori kuwa fupi,
Baada ya wiki mbili Nikiwa kwneye kibiashara changu simu yangu ikaita, ilikuwa namba ngeni, nikapokea,
Aliyekuwa anaongea na Mwanamke ambaye ni boss wetu.

Boss; Niweke Pesa kwenye Akaunti yako ya Benki ileile?
Mimi: Unaweka kiasi gani? Maana tayari haya mambo yameshafika Mahakamani na kiwango cha Pesa ulikiona pamoja na Fidia ya usumbufu na gharama za kuendesha kesi.
Boss; Robert nakuomba niwalipe zile mnazonidai, nimepitia kipindi kigumu Sana kifedha hata Mungu anajua, hizi zenyewe nimezikopa sehemu Fulani ili niwalipe nyie.
Bla!blah! blah!"

Aliongea Kwa uchungu, binafsi nilimuelewa, lengo langu halikuwa kumkomoa, lengo langu lilikuwa Kupata Haki yangu, kilichochangu.

Mimi; Waingizie wengine Pesa zao, Mimi niwe wamwisho, maana kama nilivyokuahidi zakwangu utatoa tuu iwe wewe au familia yako.

Boss: Kwa nini unawahangaikia hao, hawatakusaidia kitu chochote. Usipende kuwasaidia Saidia Watu. Watu ni wabaya.

Mimi: Walipe Kwanza kisha utanipigie kunipa hayo mahubiri. Kwa jinsi ulivyowafanyia ubaya na kunifanyia Mimi sidhani kama unaweza kuwa mshauri wangu WA nini nifanye na kipi nisifanye.

Akawatumia, nikawauliza wakasema wameingiziwa Pesa zao. Kisha nami nikatumiwa pesa yangu.

Baada ya hapo nilitegemea kuwa zilepesa ambazo tulikubaliana kuwa watanilipa Kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa namlipa Wakili, na ishu za usafiri Kwa wale wengine kufuatilia mambo ya kesi ambalo lilikuwa jukumu lao, hawakunilipa

Wala kunipigia simu kunishukuru Kwa jinsi nilivyohangaika kwaajili Yao,
Fikiria MTU analipwa milioni 11 alafu anashindwa kutoa hata elfu 50 tuu ya Ahsante Kwa aliyempigania apate hizo Pesa.

Nikachukua simu, Kwa bahati nzuri huwaga sio mtu wa kunyamazia mambo.
Nikawapigia, baadhi walipokea wengine hawakupokea tangu siku waliyolipwa.
Nikawaambia kwenye Maisha wanapaswa kuwa na Shukrani ili wasiishie Kupata msaada mmoja tuu.

Baadaye, Yule boss wa kike alianzisha kampuuni nyingine 2021 akataka niwe sehemu ya hiyo kampuni, nikakataa Kwa kumueleza kuwa sasa hivi ninashughulika na vijibiashara vyako ingawaje bado ni vidogo.
Alijitahidi kuniweka karibu lakini Imani yangu kwake ilipotea, wengine tunaamini mara moja Ila tunaouwezo WA kupenda zaidi ya mara moja.

Nilichojifunza kuhusu mkasa ule;
I) Kudai haki kunahitaji Subira na ujasiri
ii) Usaliti kwenye Kudai haki ni Jambo la kawaida.
iii) Wazazi wangu hawakuwa tayari niendelee kufuatilia mambo ya makesi walisema nimuachie Mungu.
Nikawaambia Mungu hakufanya kazi aliyefanya kazi ni Mimi.
Nikawaambia wajiandae Kwa lolote.
Nikajifunza kuwa Vijana wengi hupoteza ujasiri na Haki zao Kutokana na Wazazi na watu wao wakaribu.

iv) Ukubwa WA pua sio wingi wa makamasi. Walioondoka wote walikuwa Watu wazima above 40, wao walimuachia Mungu.

v) Tenda Wema bila kutegemea Shukrani.
Binadamu wengi ni wabinafsi.

Jamii ikiwa na kizazi jasiri, dhulma na uonevu vitapungua Sana.

Watu hawaonewi na kudhulumiwa Kwa umaskini wao Bali wanaonewa na kudhulumiwa Kutokana na woga na mtizamo wao Mbaya kuhusu matajiri.

Kizazi cha kuonewa ndicho huunda serikali yenye viongozi waonevu na wenye dhulma.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Nimejifunza sana
 
Mtu aliyezizoea milioni 100 anashindwaje Kutumia Makampuni ya sheria yaliyojaa nchi nzima?

Tatizo ni yeye aliyeanza kumdhulumu mwenzake Kwa kisingizio cha Pesa zimeibiwa,
Sasa mwenzake kachukua mpaka riba.
Wapo watu walichukua simu za mkopo Hong Kong na China ilikua ukienda ukinunua za usd 10,000 miaka ya 2007-2010 mfano wanakupa zingine za Ten elfu usd au zaidi niliwaambia hizi hela sio rahisi kihivi walidhani wanaweza kuwadhurumu Wachina baadae walifatwa walichukuliwa vitu vyao kimya kimya wengine waliyakimbia maduka yao Agrey hapo na Msimbazi kwa mtu atakaekuja kuangalia story ya mwisho ataona huyu mswahili anaonewa kumbe pana vitu vingi vilipita...
 
Mie nasema huyo Eliud angekutana na mimi angenichukia yeye, watoto wake na vizazi vingine viwili.

Huwezi poteza hela kiasi hicho recklessly kabisa.

Waarabu wanaendelea kwa sababu wako strict na principle zao kwenye biashara. Nenda uarabuni utaona makampuni mengi ni wao lkn hawaendeshi wao, ila wanaowasaidia kuyaendesha wanajua jamaa hawataki mchezo na mali zao. Sasa wabongo baada ya kuiga hio mentality tunakuja kujivika unyonge kutafuta haki za kipuuzi baada ya kufanya upuuzi. Kama uliiba jipange kulipa hela au pumbu zako zifanyishe mazoezi mapema

Mbaya zaidi, Wakati unafanya uhalifu unakuwa kimya, serikali inakosa Kodi, hao wanaodhulimiwa au kutekwa hujawahi kushtaki au kulisema popote.
Basi kama unaogopa kusema basi Acha kushirikiana na wahalifu pia HAUTAKI Kwa sababu ya kuendekeza tunbo na ubinafsi.

Yakija kukukuta unailaumu Polisi sijui Mahakama utadhani wewe kuna kitu umefanya.

Watanzania tuelewe kuwa kadiri tunavyonyamaza tunapoona uhalifu au uovu usiotugusa ndivyo Watu watakavyo nyamaza watakapoona tukionewa na kufanyiwa uovu
 
Binafsi kwenye ule uzi, niliishia tu kuguna na kusema no comments. Maana ukichunguza kwa kina, utagundua wahusika wote wana makosa., lakini pia ni Waarabu wa Pemba.
 
Wapo watu walichukua simu za mkopo Hong Kong na China ilikua ukienda ukinunua za usd 10,000 miaka ya 2007-2010 mfano wanakupa zingine za Ten elfu usd au zaidi niliwaambia hizi hela sio rahisi kihivi walidhani wanaweza kuwadhurumu Wachina baadae walifatwa walichukuliwa vitu vyao kimya kimya wengine waliyakimbia maduka yao Agrey hapo na Msimbazi kwa mtu atakaekuja kuangalia story ya mwisho ataona huyu mswahili anaonewa kumbe pana vitu vingi vilipita...

Alafu kikawaida muovu hupendelea kumuonea muovu mdogo.
Yaani ukitumwa au ukiyafumbia maovu Mbele ya muovu Ipo siku atakufanyia uovu na wewe.

Mfano, umeajiriwa na kampuni Fulani lakini Boss wako ni muonevu, usipoweza kumwambia jua Ipo siku atakuonea wewe.
Lakini ukiwa unamuambia kama, Ila boss hivyo unavyofanya sio poa, hiyo ni dhulma na dhulma sio nzuri Kabisa.
Ninakuhakikishia boss huyo hatakuwa na ujasiri wa kukudhulumu.

Lakini maboss wengi wameshajihakikisha kuwa wanaowafanyia dhulma wenyewe ni wadhulumaji kama wao, sema ni vile nafasi zinatofautiana
 
Back
Top Bottom