Bhujegwe
Senior Member
- Nov 23, 2013
- 135
- 191
Ninawiwa kusaidiwa kujua ni muda upi kisheria ambao mtu aliyeshindwa kesi ya madai Mahakama Kuu-Ardhi atakuwa ndani ya muda kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa.
Swali langu linajengwa na case ground ifuatayo japo kwa ufupi sana. Mnamo mwaka 2014,Jamaa yangu Mjasiriamali aliomba na kupewa mkopo tshs.10m kutoka benki ya Posta Tanzania tawi fulani huko jijin Mwanza. Ambapo aliweka nyumba yake ya makaz km dhamana ya mkopo huo (ambayo ktk mkataba wao na benki walikubaliana na kusainiana kuwa ilikuwa na thaman ya tshs 50m),kwa mkataba wa marejesho ya mwaka mmoja.
Hata hivyo baada ya miez 3 tokea kupata huo mkopo, jamaa alivamiwa dukani na majambaz dukan na kunyang'anywa kias kikubwa cha fedha. Lilikuwa tukio la waz na liliripotiwa Polis station-Nyakato ambao walifika dakika 15 baada ya wizi huo kutendeka.
Licha ya ugumu wa kibiashara,jamaa aliendelea kujikongoja kupeleka marejesho kidogo kidogo ingawa anakiri kwa sehemu hakuweza kwenda sawa tena na makubaliano ya kimkataba.
Kwa maelezo yake benki waliuza nyumba yake miezi 4 kabla ya Mkataba wao kuisha kwa tshs 9.9m na ni ktk wakati ambao deni lilikuwa limebakia tshs. 7.5m tu. Kwenye mauzo hayo hakupewa pesa yoyote iliyozid!
Hiyo ni nyumba ya vyumba 4 vya kulala huku masterbedroom ikiwa ni self,ikiwa na dinning,kitchen na sitting room,tiles,ceilling bord,umeme na maji ndani choo na bafu kwa nje na kiwanja kikiwa na nyumba nyingine ya vyumba 2 pembeni.
Licha ya kuwa amehangaikia kuanzia baraza la ardhi na nyumba la Nyamagana had Mahakama Kuu-Ardhi bado amejikuta akiangukia pua.
Binafs nimehis hukumu za kushindwa kwake ni matokeo ya yeye kutopata Mawakili wenye nguvu za Kisheria ili kumsaidia kutetea haki yake na hasa nikizingatia kuwa aliyeichukua hiyo nyumba ni kigogo mmoja wa CCM (Nasikia alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda wakati huo). Na ndiyo maana ilitumika nguvu kubwa ya kumtoa nje pasipo kibali cha mahakama.
Niko kutafuta namna ya kumsaidia huyu jamaa ili ajarib kuitafuta haki ikiwa bado mlango wa kisheria utaruhusu. Kwa maelezo yake,aliandika barua ya malalamiko ofisi ya TAKUKURU kuomba msaada lakini akajibiwa kuwa suala lake linapaswa kushughulikiwa ktk mfumo wa kimahakama ilimradi lilishapelekwa huko. Lakini hata wao walikiri anazo sababu za msingi kwenye shauri lake.
Hukumu ya Mahakama Kuu-Ardhi ilisomwa mwaka jana mwezi June.
Je,kungali kuna mlango wa kisheria kulifuatilia na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa?
Naombeni hekima,busara na huruma zenu ili tumsaidie,kwa vile tu yeye alikwama pale Mawakili walipompa hesabu ya zaidi ya tshs.5m km gharama za kesi!
Huyu ni mtu anahangaika na nyumba za kupanga na kwa familia yake ya wategemezi 15 anapitia wakati mgumu huku mtu mwingine kwa kutumia cheo chake tu akifaidi nyumba aliyoijenga kwa jasho na damu akitumia vihela vya kudunduliza.
Msaada wenu wa Mawazo ndugu zangu!!!