Msaada wa kisheria katika Jimbo la Arumeru Mashariki

Ni lazima si unajua sio yeye anaendeshwa na waliomweka
qinp1.jpg

qinp2.jpg

qinp3.jpg
 
Naombeni wana JF mnisaidie katika jambo hili.Hivi kama jimbo limemchagua mbunge na bado hajaapishwa,sheria inasemaje katika hilo?
Hapa Arumeru Mashariki mbunge aliyechaguliwa anaumwa hata kabla ya kampeni za mwaka jana.Lakini kutokana na upumbavu wa wanaArumeru wachache wakampa ubunge eti kwa kuwa ni mzee na tene niwa CCM.
Huyu mzee naambiwa amelazwa mpaka leo na hajaapishwa.Vipi ni mbunge halali kweli?
Aliwahi kuwa naibu waziri wa Fedha 2005/10.

Kwanza tulisikia alihonga dakika za mwisho alikuwa ameisha bwagwa huyo. Hao wameru huwa siwaelewagi kabisa ni kama kwetu huku wazinza ni kama wameru kabisa wana kuwa na mambo ya ajabu ajabu sana na mihasira ya kufa mtu.

My Take;

Speaker wa bunge mpaka sasa haja liona hilo au ni kuta kujiongezea kiti (CCM) ndani ya bunge??
 
Watazania tambueni hili .....''Haki huinua Taifa bali Dhambi ni aibu ya watu wote''.......Dogo SUMARI ndo angetakiwa awe mbunge wa lile Jimbo (ARUMERU MASH) lakini kutokana na HILA,UFISADI,UWEZO WA FEDHA,MAZOEA,MKUMBO,UNAFIKI WA KISIASA,KUJIPENDEKEZA,KUKOSA FOCUS(UPEO),Ndgu zangu wa damu WAMERU walijichakachua wenyewe...kuna huu msemo CHAKACHUA ,UCHAKACHULIWE...Imekula kwetu..miaka 5 itaisha hivihivi.

Ee MUNGU haki ya mtu haipotei ndgo SUMARI Usikate tamaa jipe moyo kuna siku....Nawasilisha.
 
Vuteni subra' kama muda wote huo bado anaumwa mapenzi ya Mungu yatatimizwa mtafanya uchaguzi mwingine mda si mrefu!
 
Jaji Makame (Mwenyekiti) na Ibrahim Kiravo (mkurugenzi) hawaoni jinsi haki ya kuwakilishwa ya wanajimbo wa Arumeru Mashariki inapotezwa? The mzee (Sumary) is said to be mentally incapable of carrying out his own daily affairs. He is mentally sick.
 
Kweli yule mbunge ni kuhurumia kuna siku tulikutana mahali amekonda sana hata kutembea anatembea kwa shida.
Inabidi tu wameru wavumilie kwa mad usiojulikana kuna siku tulikuwa na jamaa fulani akasema chadema tunasubiri kuchukua jimbo letu tulilochakachuliwa na ccm.
 
" Huyu mzee naambiwa amelazwa mpaka leo na hajaapishwa" The guy is in DAR busy working kamaa kawaida, who told you amelazwa?
 


Kwanza tulisikia alihonga dakika za mwisho alikuwa ameisha bwagwa huyo. Hao wameru huwa siwaelewagi kabisa ni kama kwetu huku wazinza ni kama wameru kabisa wana kuwa na mambo ya ajabu ajabu sana na mihasira ya kufa mtu.

My Take;

Speaker wa bunge mpaka sasa haja liona hilo au ni kuta kujiongezea kiti (CCM) ndani ya bunge??
Wewe unadhani Arumeru na Arusha mjini ni wapi CDM wametawala?...hebu nipe namba ya madiwani wa meru ambao ni CDM na madiwani wa Arusha ambao ni cdm.Halafu labda ndio nitafahamu wapi CCMwana jimbo na wapi CDM wana jimbo.
 
Inatakiwa Spika aiandikie tume ya uchaguzi kwamba Jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi, ili tume itoe taarifa kwa vyama vya siasa kugombania. inashangaza na kusikitisha kwamba mwaka unaisha jimbo halina mbunge na serikali legelege iko kimya!
 
Mpumbavu ni wewe na siyo wana Arumeru. Wao wametumia haki yao ya kikatiba ya kumchagua mtu wanayemtaka.

Ndg yangu Mwitw hili ni kosa kubwa sana ambalo wameru tumefanyiwa na Serikali, huyu ndg hawezituwakilisha, sijapenda sana jina la wameru kuitwa wapumbavu, ila neno lenyewe lina ukweli ndani yake. tunahitaji uchaguzi urudiwe tumpate mbunge mzima wa afya, wewe fikiri kama mtu amekosa nguvu ya kuapishwa ataweza kuhudhuria vikao licha ya kuwawakilishia wananchi matatizo yao?
 
Sumari ameapishwa. Anashiriki vikao vya Bunge ingawa sio vyote. Juzi nimemwona mjini atembea mwenyewe na anaongea vizuri. Naomba tuweke usahihi wa Jambo hili.
 
hii katiba inabidi iseme ni kwa muda gani mbunge anapaswa kusuburuwa akiwa mgonjwa. Na isiwe zaid ya miezi 12 Ngoma iwekwe kati kipenga kipulizwe upya
 
Back
Top Bottom