bampami
JF-Expert Member
- Nov 5, 2011
- 5,697
- 4,107
Habari wana JamiiForums,
Nimekuwa nikisikia kuwa kuvaa pete na shela wakati wa harusi ni kutenda dhambi, lakini pia kumekuwa na mafundisho mengi yazungumzayo uhusiano wake na dhambi, pamoja na kusoma mafundisho hayo yote bado nimekuwa mgumu kuelewa, kwani sijaona dhambi hapo, isipokuwa kama bibi harusi kavaa shela lenye kuonyesha maumbile yake ya mwili.
Nimekuja kwenu nikijua kuna wataalam wengi waliosoma biblia, wakailelewa wenye vipaji toka kwa Mungu vya kutafsiri biblia ipasavyo, nitaambatanisha na somo moja wapo ambalo nimelipitia lakini bado moyo wangu unaegamia kuwa siyo dhambi, japokuwa 98% ya marafiki zangu na ndugu zangu wanasema ni dhambi.
Sasa..Je, kuvaa shela na kuvalishwa pete wakati wa harusi ni dhambi mbele za Mungu au?
Kama ni dhambi:
Je, ni vifungu gani katika biblia vinavyosema na kukataza watu wasivae mashela, wala kuvalishana pete wakati wa harusi?
Kama Si Dhambi:
Je, nitasimamia vifungu gani vya biblia ili kujiridhisha kuwa tukio hili takatifu la kuunganisha maisha ya wawili kuwa mwili mmoja yakiambata na mavazi kama vile shela, suit na kuvishana pete si ishara ya kutenda dhambi mbele za Mungu?
Nimeambatanisha na link ya moja ya somo lizungumziayo : http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/12/somo-mavazi-ya-mtu-aliyeokoka-askofu.html