Lengo la kuvaa pete ya ndoa ni nini wakati ndoa ni yako binafsi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,022
144,380
Ni utamduni uliozoeleka na bila shaka ni wa kimagharibi zaidi ingawa uko dunia nzima.

Swali ni je, kwanini uonyeshe kuwa umeoa au umeolewa?

Kuna mahala watu hatambulika kwa ndoa?

Kama ni kulinda ndoa, ndio iwe kwa kuvaa pete?

Je, hii si mbinu ya kulazimisha watu kuheshimu ndoa?

Mfungwa atambulike kwa mavazi na mwenye ndoa kwa kuvaa pete, hii ni sawa?

Je, hawa wote sio wafungwa katika mazingira tofauti?

Tukumbuke wanawake mpaka pete ya uchumba.

Na je, vitabu vya dini vinaelekeza watu kuvaa pete za ndoa au kujitangaza kuwa nimeoa au nimeolewa?

Sipati majibu kabisa!
 
Binafsi nikimuona mwanamke kavaa pete huwa kunakaheshima flani hivi kwake,..na hatakama nimevutiwa nae huwa napita kushoto.
 
Pete ni utamaduni wa kishamba wazungu.
Ndoa haihitaji ishara, inahitaji Mwanamume ampende kwa dhati mke wake na mke awe mtii bila gubu kwa mumewe.
 
Ni utamduni uliozoeleka na bila shaka ni wa kimagharibi zaidi ingawa uko dunia nzima.

Swali ni je, kwanini uonyeshe kuwa umeoa au umeolewa?

Kuna mahala watu hatambulika kwa ndoa?

Kama ni kulinda ndoa, ndio iwe kwa kuvaa pete?

Je, hii si mbinu ya kulazimisha watu kuheshimu ndoa?

Mfungwa atambulike kwa mavazi na mwenye ndoa kwa kuvaa pete, hii ni sawa?

Je, hawa wote sio wafungwa katika mazingira tofauti?

Tukumbuke wanawake mpaka pete ya uchumba.

Na je, vitabu vya dini vinaelekeza watu kuvaa pete za ndoa au kujitangaza kuwa nimeoa au nimeolewa?

Sipati majibu kabisa!
Lengo la wewe kuvaa nguo ni lipi, wakati mwili ni wako binafsi?

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Mtu akifunga ndoa, anatoa ishara kwa umma wote ili waelewe kabisa kwambaa;

Baninga eeh, nasi na bali..... Botika ngofinela amiso go na nzela. NASI MOBAYE NA BALI (kwaherufi kubwa)

Ndiyo badala ashike kipaza sauti kutangaza, basi avaa pete, au pambo fulani kutoa ujumbe huo subtly, kichinichini.

Faida yake ni inasaidia jamii ili mtu mwingine asitumie nguvu nyingi kuflirt naye kumbe tayari sio fungu lake.

Kwa tunaopenda jamii ya kistaarabu tunaona ni utaratibu mzuri na wa kistaarabu kuliko iwe kila unayepishana naye njiani anakuuliza 'Umeoa?Umeolewa? Aaaaargh!
Sipati majibu kabisa
 
Wee unaonekn mtaalamu wa music ya kongo......
 
Kuna shida gani kwani, Kama haupendi usivae haulazimishwi, kwamba ukifunga ndoa lazima uvae. Waislamu hawavai, wasabato na mashahidi wa Jehova hawavai
 
Back
Top Bottom