WENYELE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,415
- 1,379
Wakuu, naomba msaada kupata shule ya wasichana ya Bweni ya bei kawaida Advance, itakua nzuri ikipatikana kanda ya ziwa au sehemu nyingine Tanzania.
Iko hivi, mimi ni mwenyeji wa kanda ya ziwa, jana nilipigiwa simu na binti wa pale kijijini kwetu kamaliza form 4 akapata DIV III ya 25 bahati mbaya combination hazikubalance.
Selection za kwanza zimetoka hajachaguliwa bahati mbaya nyumbani mzee wake ashamtafutia mme na anataka kumuozesha kwa ng'ombe, dogo akanipigia simu jana analia anahitaji msaada. Mimi ninatokea pale kijiji ni mmoja wa tu tuliosoma ktk mazingira magumu ila tukafanikiwa so binti alinitafuta ili nimpe msaada au nimsaidie aende kwa mkurugenzi au mkuu wa wilaya ya Itilima.
Sasa mimi nikaona nikimsomesha sio mbaya sababu nishawahi kufanya hivyo kwa kijana mwingine pale kijijini 2015 japo yeye alikua na DIV IV 26 nilim-sponsor kwa kusaidiana na group langu la WhatsApp la chuo kikuu akapiga advance km private candidate na akafaulu vizuri kwa DIV II ya 12 saiv yupo Mwenge University pale.
Kiuchumi siko vizuri sana ila siwezi kukosa kumsapoti kidogo kidogo hadi anamaliza.
Naomba ushauri wenu wakuu na msaada wa shule au vyuo navyoweza mpeleka akasome ili naye akamilishe ndoto zake.
Natanguliza shukrani