Msaada: Shule ya wasichana Advanced Level inahitajika haraka

WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,415
1,379
Wakuu, naomba msaada kupata shule ya wasichana ya Bweni ya bei kawaida Advance, itakua nzuri ikipatikana kanda ya ziwa au sehemu nyingine Tanzania.

Iko hivi, mimi ni mwenyeji wa kanda ya ziwa, jana nilipigiwa simu na binti wa pale kijijini kwetu kamaliza form 4 akapata DIV III ya 25 bahati mbaya combination hazikubalance.

Selection za kwanza zimetoka hajachaguliwa bahati mbaya nyumbani mzee wake ashamtafutia mme na anataka kumuozesha kwa ng'ombe, dogo akanipigia simu jana analia anahitaji msaada. Mimi ninatokea pale kijiji ni mmoja wa tu tuliosoma ktk mazingira magumu ila tukafanikiwa so binti alinitafuta ili nimpe msaada au nimsaidie aende kwa mkurugenzi au mkuu wa wilaya ya Itilima.

Sasa mimi nikaona nikimsomesha sio mbaya sababu nishawahi kufanya hivyo kwa kijana mwingine pale kijijini 2015 japo yeye alikua na DIV IV 26 nilim-sponsor kwa kusaidiana na group langu la WhatsApp la chuo kikuu akapiga advance km private candidate na akafaulu vizuri kwa DIV II ya 12 saiv yupo Mwenge University pale.

Kiuchumi siko vizuri sana ila siwezi kukosa kumsapoti kidogo kidogo hadi anamaliza.

Naomba ushauri wenu wakuu na msaada wa shule au vyuo navyoweza mpeleka akasome ili naye akamilishe ndoto zake.

Natanguliza shukrani
 
Aisee Mungu akubariki sana kwa haya uyafanyayo....

Kwa kuangalia matokeo yake ungeweka kwanza angalau kombi iliyokaa vozuri then watu wakashauri shule ya kumpeleka
 
Asante mkuu
Ana
KISWAHILI-C
HISTORY-C
CIVICS-C
GEOGRAPHY-D
ENGLISH-D
na masomo mengine ana D
 
Morogoro Maeneo Ya Nane Nane Kuna Shule Ya Father Pekupeku Nadhani Wana Ada Nafuu
 
Hii naifahamu inaitwa Alpha, kijana wa kanza niliyemsapoti alisoma pale ila iko mbali na kwao kwa kuwa huyu ni wa kike anaweza sumbuka
 
Sawa
Kama Unaijua
Ni Mchanganyiko Pia Ipo Nyingine Mtoni Morogoro Secondary School.
 
Wakuu, naomba msaada kupata shule ya wasichana ya Bweni ya bei kawaida Advance, itakua nzuri ikipatikana kanda ya ziwa au sehemu nyingine Tanzania.

Iko hivi, mimi ni mwenyeji wa kanda ya ziwa, jana nilipigiwa simu na binti wa pale kijijini kwetu kamaliza form 4 akapata DIV III ya 25 bahati mbaya combination hazikubalance.

Selection za kwanza zimetoka hajachaguliwa bahati mbaya nyumbani mzee wake ashamtafutia mme na anataka kumuozesha kwa ng'ombe, dogo akanipigia simu jana analia anahitaji msaada. Mimi ninatokea pale kijiji ni mmoja wa tu tuliosoma ktk mazingira magumu ila tukafanikiwa so binti alinitafuta ili nimpe msaada au nimsaidie aende kwa mkurugenzi au mkuu wa wilaya ya Itilima.

Sasa mimi nikaona nikimsomesha sio mbaya sababu nishawahi kufanya hivyo kwa kijana mwingine pale kijijini 2015 japo yeye alikua na DIV IV 26 nilim-sponsor kwa kusaidiana na group langu la WhatsApp la chuo kikuu akapiga advance km private candidate na akafaulu vizuri kwa DIV II ya 12 saiv yupo Mwenge University pale.

Kiuchumi siko vizuri sana ila siwezi kukosa kumsapoti kidogo kidogo hadi anamaliza.

Naomba ushauri wenu wakuu na msaada wa shule au vyuo navyoweza mpeleka akasome ili naye akamilishe ndoto zake.

Natanguliza shukrani
Kibaha ipo Gili girls ,ada Ni 4m na Ni boarding,Hakuna pocket money wala nini.Ukimleta ukamfikisha basi hakuna gharama,chakula kizuri na kila kitu Safi ni kusoma tu.
 
Back
Top Bottom