Msaada: Mahesabu ya kodi ya kuingiza gari

Sniper

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,915
709
Wadau wa JF naomba mnisaidie kwa hili, kuna gari nataka niagize toka Japan, nilikuwa nataka kujua makadirio ya kodi ili nijipange vizuri kwa hilo. Nimefungua ile website ya Welcome to GariYangu.com - GariYangu.Com, kuna calculator pale, lakini nimekuta wameweka tangazo kuwa ile calculator ni kwa viwango vya zamani. Kwa viwango vipya vya kodi wameweka link ya TRA, ambayo nimefungua inaonesha mahesabu ambayo kwa kweli nimeshindwa kuyaelewa.
Naomba msaada wa kujua kodi ya hii gari nitakayoagiza au kama kuna link ya calculator mpya. Asanteni

Details za gari:
Make: Mercedes Benz
Model: C Class (C200 KOMPRESSOR)
Model Code: 203045
Year: 2002
Displacement: 2000
FOB Price: 4950 USD
 
Naona nimekosa msaada humu, au nimeposti kwenye jukwaa si sahihi?
 
Freight/Insurance ni kiasi gani? Customs value sio chini ya USD 7,537 (i.e. kama CIF utakayo declare itakuwa kubwa, then hiyo ndiyo itakayotumika) na kodi sio chini ya USD 4,136

[basis: current retail price USD 48,637 (tra), depreceiation 70%]
 
Mkuu nimeku PM
 
kama gari yako imetumika zaidi ya miaka kumi,kodi itakuwa asilimia 83 ya CIF na kama haijatumika zaidi ya miaka kumi kodi ni asilimia 63 ya CIF,hizo asilimia zimejumlishwa kodi zote,import,excise etc!kama nitakuwa nimekosea ni kiasi kidogo kwa ni muda sasa sijaagiza.
 
VEHICLE COSTINGS
usd
Exch rate
Tshs.
cummulative total
1
Total invoice value
FOB
4,950
2
Freight
2,000
3
Insurance
500
4
Customs Value
CIF Dsm
7,450
1,700.00
12,665,000.00
12,665,000.00
5
Import Duty
25%
3,166,250.00
15,831,250.00
6
Excise Duty
5%
791,562.50
16,622,812.50
7
VAT
18%
2,992,106.25
19,614,918.75
8
Registration&clearing ????
Tukijua freight and insurance then tutakupa jibu la uhakika, hizo nilizoweka ni imaginery
Customs value ni Cost Insurance and Freght (CIF Dsm)
Import duty ni 25% ya CIF
Excise duty ni 5% ya (CIF+Import duty)
Vat ni 18% ya (CIF+Import duty+Excise duty).

GUIDELINE SUBJECT TO VERIFICATION
Current Retail Selling Price
$48,637
Depreciation
70%
Freight
$2,500
Extra Depreciation
0%
Customs value
$7,537
FOB Value
$5,037
Import Duty 25%
$1,884
Excise Base
$9,421
Excise Duty 5%
$471
VAT Base
$9,892
VAT 18%
$1,781
Total Taxes
$4,136
Total Taxes in TSHs
-

Mahesabu hapo juu ni kulingana na TRA Car Tax Calculator.

Below are taxes computed using my own calculator which gives you the same answer.

View attachment benz.doc
 
Back
Top Bottom