Msaada kuhusu mikopo ya wanafunzi elimu ya juu

Terminator

Member
May 27, 2009
32
10
Wakuu nahisi naingizwa mjini na ndugu yangu ambaye nilijitolea kumsomesha Tumaini, alijiunga na kuniletea joining instruction ikinionyesha kiasi cha ada na mahitaji mengine, ila baadae nimekuja kugundua kuwa ali-apply mkopo HESLB na kupata na wala hakunipa taarifa, kwahiyo nikawa natoa ada kama kawaida na hela za matumizi,huu ni mwaka wake wa pili katika masomo na kinachonitia uchungu ni huyu ndugu ni mtoto wa kaka yangu ambae ni marehemu, nilifuatilia kwa wanafunzi wenzake pia wakanijibu ni kweli amepewa mkopo na jina lake lipo kwenye notice board likionyesha meal and accommodation allowance na stationery. ila kiasi alichopewa kwa ajili ya ada ndio sijui na nimeshindwa ku-access kwenye mtandao. ila tayari kanipigia akidai ada tena ya semester hii, nikamweleza kuhusu huo mkopo akashtuka na kuwa na majibu lukuki, basi nikamuomba anieleze kiasi cha ada alichopewa ameanzaa kunichanganyia habari mara amepewa laki sita ambayo italipia ada kwa kila semester laki tatu kwa hiyo niongeze ziada. kwa maana hiyo wakuu naomba kujua mkopo kama mkopo huwa unatolewa kwa semester au unagawanywa kulipia semester mbili kwa mujibu wa maelezo yake, pia naomba kujua jinsi ya kuingia katika mtandao maana pamoja na yote aliyonifanyia kiasi halisi cha ada bado anakanganya,
 
vijana hao kama una uwezo wa kumlipia hiyo senti wewe mlipie tu mungu atakupa dhawabu
 
Back
Top Bottom