Msaada: Jinsi kutengeneza Mandazi

Babu M ............nna wasi wasi hukijui unachokitafuta. maandazi ya kubonyea ndio hayo hapo kwenye linki pamoja na picha na recipe na namna ya kutengeneza.................unless wewe unataka kufundishwa kaimati

(au ramadhani inakuja umekumbuka kaimati? maana hichi chakula sana kinapikwa wakati huo)
 
nakubaliana na wewe Gaijin, maanadazi ya kumimina!!! na kila kilichowekwa hapa sio!
 
Mkongwe chemsha viazi vitamu au magimbi ndy simpo kuliko vyote, halafu kiasili zaidi. Kama vp wasiliana na wadau wakutumie...au ndy uko Australia kwenye masharti kibao kuingiza MANUMBU? Kule Tabora wangekutumia MATOBORWA au Shinyanga wangekutumia Maparage na Michembe!! Ukikosa kabisa kunywa uji wa ulezi!
 
Babu M ............nna wasi wasi hukijui unachokitafuta. maandazi ya kubonyea ndio hayo hapo kwenye linki pamoja na picha na recipe na namna ya kutengeneza.................unless wewe unataka kufundishwa kaimati

(au ramadhani inakuja umekumbuka kaimati? maana hichi chakula sana kinapikwa wakati huo)

Huyo mi nimemsoma kitambo, anataka BAGIA
 
Mkuu X-PASTER hakuna mapishi ya kalimati katika ukumbi huo, kama unafahamu jinsi ya kuzikorofisha basi naomba uweke details
Kaimati

Vipimo:

Unga ---------------------2 vikombe vya chai
Hamira ---------------------1 ½ Kijiko cha chai
Samli ---------------------1 Kijiko cha Supu
Maji ---------------------1 ½ kikombe cha chai (kiasi)
Mafuta ya kukaangia --------------------- kiasi
Shira ---------------------1 kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Changanya unga Hamira, Samli, maji, kisha vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
2. Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
3. Ziepue na zichuje mafuta.
4. Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia Shira zikiwa tayari.

Shira:
Sukari --------------------- 2 vikombe
Maji --------------------- 1 kikombe
Zaafarani ---------------------1 kijiko cha chai
Hiliki --------------------- ¼ kijiko cha chai
Arki (rose flavour) --------------------- 3-4 matone
 
Asante kwa msaada wako.Huko tunafikaje bila kugonga hapa? nimejaribu kutafuta "Groups" lakini sijapata.
Gonga kwenye profile yangu, kisha scroll kwa chini utaona ilo group la mambo ya mahakuli, nawe unaweza kujiunga kwenye group kama utapendezwa nalo.

Karibu sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom