Msaada: Gari langu lina tatizo la kushtuka stuka nikiwa barabarani

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,789
2,383
Habari wana JF.

Naombeni ushauri kwa mafundi au yeyote anayeweza kujua tatizo la gari langu.

Nina gari aina ya Hirrier vijana wanaita (matako ya nyani). Gari hili nimenunua mwishoni mwa mwaka 2018.
Takribani miezi mitatu, gari lilianza tatizo la kushtuka stuka (inakita) ukiwa mwenye mwendo. . Nilimleta fundi (niliambiwa ni mzuri) akaitazama na akasema tatizo ni control box. Suala la control box ikafanyiwa kazi.

Tatizo halikuisha. Fundi wa pili akaja akasema tatizo ni valve chaser nayo tukarekebisha. Tatizo halijaisha. Mbaya zaidi sasa hivi nikiweka reverse gear, gali halirudi mpaka nikanyage mafuta.

Fundi wa tatu ananiambia nibadilishe engine. Sasa kabla sijaendelea kupoteza fedha zingine, nimeona nije humu JF naweza kupata ushauri wa kitaalam.

Aksanteni
 
Yale yale ya Daktari kupasua mtu kichwa kumbe mtu anaumwa kiuno... Tafuta mafundi professional au garage professional wenye kuiscan gari kwa vifaa maalum sio mafundi ambao wanakadilia tu
Aksante chief. Tafadhali unaweza kushare angalau gareji nzuri nikawaone? Nipo Dar es Salaam.
 
Nenda kwa Dr. toyota...pale sinza ama kariakoo....mtafute kwenye social media.
 
Habari wana JF.

Naombeni ushauri kwa mafundi au yeyote anayeweza kujua tatizo la gari langu.

Nina gari aina ya Hirrier vijana wanaita (matako ya nyani). Gari hili nimenunua mwishoni mwa mwaka 2018.
Takribani miezi mitatu, gari lilianza tatizo la kushtuka stuka (inakita) ukiwa mwenye mwendo. . Nilimleta fundi (niliambiwa ni mzuri) akaitazama na akasema tatizo ni control box. Suala la control box ikafanyiwa kazi.

Tatizo halikuisha. Fundi wa pili akaja akasema tatizo ni valve chaser nayo tukarekebisha. Tatizo halijaisha. Mbaya zaidi sasa hivi nikiweka reverse gear, gali halirudi mpaka nikanyage mafuta.

Fundi wa tatu ananiambia nibadilishe engine. Sasa kabla sijaendelea kupoteza fedha zingine, nimeona nije humu JF naweza kupata ushauri wa kitaalam.

Aksanteni
Mtumba noma ulitakiwa ushushe engine waipange upya
 
Gari yangu ilikuwa na shida kama Hy, fatilia acceleration cable ikaguliwe unaweza kuta ina kitu, pia check front diffu may be ina cheza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom