Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,701
- 9,779
Usiku ule ulikuwa ni wa kutisha sana. Binafsi niliwaza sana na kumwambia mke wangu, sijui kama patakucha nikiwa hai.
Basi bhana, maumivu ya kichwa yasiyo na kifani, maumivu ya misuli na mifupa, njaa kali, kichefu chefu, sensitivity ya ngozi kuongezeka, kukosa nguvu kabisa viliutawala mwili wangu. Palipokucha tu nikazama duka la dawa kuchukua Dawa tatu. Hadi kufikia saa kumi na mbili jioni, hali ilikuwa imetaradadi. Nikaona wacha nikapate vipimo. Baada ya kumuelezea yule daktari wa kike mwenye kihospitali chake cha mchongo, akanijibu eti tupime Malaria.
Nikajaribu kumfafanulia kuwa siku tatu zilizopita nilitumia dozi ya Malafin lakini aliishia kuniuliza "Unabishana na daktari?"
Basi bhana, akapima malaria, majibu yakatoka kuwa nina malaria wadudu watatu, kisha akatoa ushauri kuwa kwa kiwango cha malaria nilichonacho itabidi nitumie Mseto na Panadol nyingi zaidi iwezekanavyo. "Ndugu mgonjwa, kula chuma hicho," ni maneno ya mwisho ya yule daktari.
Usiku wa juzi nilianza rasmi matumizi ya vidonge hivyo vya mseto. Ngozi yote ilikufa ganzi, kichwa kikawaka kuliko maelezo, nikajihisi kutapika na nisitapike, maumivu ya misuli ya macho na homa juu, kushindwa kutembea, kuona mazigazi n.k
Nimesitisha dozi kwa kweli. Nifanye nini kuondokana na hizi reactions? Msaada tafadhari!