Mjadala: Nini chanzo na tiba ya tatizo la upele kuota kwenye uume?

denis fourplux

JF-Expert Member
Aug 17, 2017
1,049
1,378
Habari zenu wana JF, samahani sana kwa usumbufu kama vile tujuavyo misemo ya wahenga kuwa mficha uchi hazai.

Since mwezi wa nne nasumbuliwa na hili tatizo nimetumia dawa nyingi sana ant fungus kama zote za tube mpaka za kopo ila bado tatizo linanisumbua.

Ninawashwa sana mwilini na vijipele vimetokea mkononi na sehemu za siri, nimepima hospital kama BURHAN, Regency wanasema siumwi kitu ila hali yangu mimi naona inazidi kua mbaya.

Majuzi nimepima hospitali ya mtaani wakasema na syphilis nimeanza matibabu ya sindano zile nne za mwezi mpaka sasa nishachoma sindano 2 ila bado hali iko vile vile tena ndio inazidi kabisa.

Mwenye msaada naomba anisaidie nawashwa sana mwili.

IMG_0697.JPG
IMG_0690.JPG
IMG_0689.JPG


UFAFANUZI WA JUMLA TATIZO HILI KUTOKA KWA MTAALAMU

MASUNDOSUNDO, MALENGELENGE, VINGWARU NA VIPELE LAINI NA VIDOGO SEHEMU ZA SIRI
Ukiwa mzima mshukuru Mungu mara mia mia, sisemi ukiwa sio mzima usimshukuru Mungu la hasha ila ninataka kuonyesha msisitizo ya kwamba kuna watu wanateseka na mardhi ya kila aina ile hali wewe mzima kabisa wala huoni sababu ya kumshukutu Mola wako.

Leo ningependa kuongelea habari ya #masundosundo, #vipele laini na #malengelenge sehemu za siri, ni vitu vidogo lakini mara nyingi vinaleta usumbufu hadi wengine kuanza kudhania wameathirika, kumbe sio. Kumbuka ili kujua umeathirika na #VVU lazima uwe umepima. Tabia ya kujipima wenyewe haifai na ni hatari sana. Kuna watu wanaota vinyama laini vidogovidogo kwenye sehemu za siri yaani nfano kichwa cha uume, mashavu ya uke, ndani kwenye mirija ya mkojo, maeneo yanayozunguka haja kubwa, kwenye makoo na mdomoni. Aidha wengine wanaota vipele vidogo vidogo sehemu mbalimbali za siri vinavyopasuka na kuacha maji mnato ivi na kisha kuunda kidonda cha wastani. Usikae na ugonjwa onana na madaktari au washauri wa afya ili uweze kuanza safari ya matibabu.

MAAMBUKIZI NA CHANZO CHA MAGONJWA HAYA ni ukosefu wa kinga imara ya mwili, kujamiiana hovyo kwa njia ambazo sio za asili na kuvaa nguo za ndani chafu. Magonjwa haya ni ya kuambukiza na pia ya kujitakia. Wadudu jamii ya virusi,bacteria na fangasi hupata nafasi kutokana na tabia hizoo na kuanza kushambulia maeneo haya niliyoyataja kirahisi sana.

DALILI ZAKE
  • Kuna vinavyoonekana kwa macho lakini vingine huwa havionekani kabisa utasikia muwasho mkali kama wa kuunguza na moto kwa mbali, iwapo utakuna unaweza tokea michubuko inayochelewa kupona. Iwapo vinaonekana basi ni kama unavyoona katika picha hapo chini.
  • Maeneo yaliyozungukwa na masundosundo saa ingine yanapata ganzi
  • Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri kama ugonjwa upo kwa ndani.
  • Kutokwa na damu ukeni hasa baada ya kufanya tendo la ndoa, ile hali hauko bleed.

UBAYA WA MAGONJWA HAYA
  • Usumbufu wa kujikuna kuna sehemu za siri kila wakati wakati mwingine utajisahau hata mbele ya wakwe
  • Maumivu
  • Ukosefu wa uhuru
  • Kuchochea magonjwa mengine
  • Kukosa uhuru wa tendo la ndoa

NAMNA GANI UTAJIKINGA
  • CHAKULA NI KINGA YA KWANZA, kama hujapata bado basi hakikisha unakula chakula bora chenye uwingi wa vyakula vyenye kukukinga dhidi ya mardhi na vyenye kujenga nguvu ya mwili na kuzalisha seli kwa wingi. Vyakula hivyo ni pamoja na vyakula vyenye protein kwa wingi, mbogamboga na matunda
  • EPUKA NGONO ZEMBE NA NGONO KIYUME NA MAUMBILE
  • Wanawake wasagaji achana na mchezo huo
  • Kuwa msafi kila wakati (hasa mliopo sehemu za joto kama DSM). Badili nguo za ndani mara kwa mara, wanaume mara nyingi utakuta mtu anavaa jeansi moja wiki nzima, hii siyo sawa.
  • Vaa chupi zilizotengenezwa kwa pamba na usivae nguo nyingi za ndani.
  • Siku za bleed tumia pedi za pamba, zenye uwezo wa kuingiza hewa safi na kutoa hewa chafu na kisha kuuwa wadudu wa aina yeyeto walio na uharibifu kwa mwili wako. Sisi tunapendekeza pedi za #Neplily kama hujawahi zitumia jaribu inaweza kuwa ndio mkombozi wako.
Kama tayari umeshapata na unamagonjwa haya kwa muda mrefu au huwa yanakuja na kutoweka basi wasiliana nasi kwa ushauri zaidi. Ili uweze kupata ushauri kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili, kupata food suppliment ili kuweza kudhibiti wadudu hawa waharibifu na wasumbufu.

USHAURI KWA WADADA – Mapenzi ya kusagana, kunyonyana sehemu za siri na mapenzi kinyume na maumbile hayafai. Tafuta namna ingine ya kumridhisha mwenza wako. Najua wadada wengi ni wasafi lakini wachache ni wachafu kabisa, pia wengi hamtumii pedi salama.

USHAURI KWA WAKAKA – Mara nyingi wakaka hukutwa na malengelenge kwenye uume na vile vipele laini vyenye kutoa maji, masundodundo wengi yanawatokea kwenye haja kubwa. Wengi hubakia kuwa cariers kwa kuendelea kuambukiza wanawake wengine ile hali wao hawana dalili, kama mpenzi wako ana dalili mojawapo kati ya hizo hapo juu basi na wewe lazima upate tiba ili kumaliza tatizo hili kikamilifu.

Achana na tabia mbaya za ngono kinyume na maumbile, kupiga punyeto, kula vyakula visivyokuwa na matunda na mboga, kuvaa nguo chafu muda mrefu bila kufua, kutumia madawa ya kulevya na pombe kali kupindukia. Kama tayari una tatizo hili tafadhali kwa sasa lina ufumbuzi na utatuzi ambapo utatumia


BAADHI YA MAONI NA USHAURI KUTOKA KWA WADAU WA JF
Pole Mkuu kwa tatizo linalokusumbua kwa haraka haraka bila kupepesa utakuwa una ugonjwa unaoitwa Genital Herpes infection ambao husababishwa na Herpes simplex virus type 1 & 2 ila kwa upande wako naona ni type 1 and type 2 ndio zinakusumbua, maana nimejaribu kuangalia na hizo blister hapo katika mwili wako zimekaa kama za herpes plus ukijaribu kuvitumbua najua utakuwa unapata maumivu ya ajabu.

Hivyo basi ningependa uende maeneo ya pale sanitas mikocheni wachukue damu, majimaji kutoka kwenye hivyo viupele, mate, au sehemu kidogo ya ngozi ambayo ina hizo blisters ili waweze kufanya analysis kwa njia ya Polymerase chain reaction (PCR) au hata Serological test (ELISA) ili ku confirm ugonjwa husika.

Kuhusu tiba incase ikagundulika una herpes infection wanatibu dalili husika, ila kwa hapo baadae utapata long life immunity amabyo itakuwezesha kutokupata huo ugonjwa tena.

NB: Ugonjwa huu madaktari wengi huhisi ni ugonjwa wa fangus, bacterial au ugonjwa wowote wa njia ya mkojo ambapo huwa ni uwongo...

Hivyo wahi kwenye hiyo hospitali kama wewe ni mkaaji wa dar es salaam uweze pata tiba kila la kheri boss.
---
Ndio Mkuu, Tahadhari tu angalia usishiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga maana uko katika risk kubwa ya kupata magonjwa hatari hasa HIV.

Na Kwa kuongeza hapo kama nilivyokwisha tangulia kusema hapo mwanzo hakuna tiba ya huo ugonjwa kama ikithibitika unao. Hivyo kuna dawa utapewa ni kama zile za ukimwi mfano Ayclovir (zovirax) , famciclovir (famvir) au valacyclovir (Valtrex), hizi dawa zitakusaidia sana maana huwa zinazuia hao vizuri wasiendelee kuzaliana na pia kuepusha wewe kusambaza vizuri hivyo pale utakapokutana kimwili na mwanamke.

Na mara nyingi baada ya kutumia dawa hizi mgonjwa hupata nafuu na kupona kabisa ila ikitokea baada ya kutumia dawa hivyo viupele vikatokea tena basi utaendelea na dawa mpaka pale vitakavyokoma.

Na pia kuhusiana na hivyo vipele ni vyema ukawa unaosha kwa kusugua na maji ya uvuguuvugu yakiwa na chumvi ndani yake kipimo ni chukua kijiko cha chai weka chumvi nusu changanya na maji nusu lita sugua kwa kuosha na kwa maumivu amadogo madogo unaweza tumia dawa kama aspirin au acetaminophen utakuwa sawa mkuu..
---
Kiongozi umenena vyema.

Mimi nashauri umuone Dr. Bingwa wa magonjwa ya ngozi. Usiende kwa madokta wa kawaida. Ulizia Dr. Bingwa wa magonjwa ya ngozi. Kwa muhimbili wanapatikana muda wowote, ila kwa hospitali binafsi wanapatikana jioni.

Ushauri. Kuna ugonjwa unaitwa scabies, na madokta wengi huwa wanakosea diagnosis yake kwa sababu ya kutokuwa na dalili hizo hizo kila wakati.

Mimi japo sio Dr. Lakini ningesema kwenye kichwa chako cha uume ni scabies, lakini scabies huwa haina blisters mwili mzima. Sehemu ambazo parasites waliingilia ndiyo huwa panawasha, na usiku muwasho unakuwa mkali sana, na hizo sehemu zenye muwasho huwa zina viuvimbe kwa sababu ya burrows za wale parasites.

Fanya hima ufanyiwe test. Lakini pia check tena VDRL kuncofirm kama kweli una Sypillis. Katika moja ya hospitali nzuri kwenye vipimo na maabara ni Regency. Kama walifanya kipimo cha Sypillis na hawakuona, basi nasita kusema ni Sypillis. Labda kama hukupimwa huo ugonjwa.
---
Pole boss, kwa muonekano wa hivo vijipele naona ni kama vile vya Herpes simplex virus Genital sores na mara nyingi huambatana na vipele vya mdomoni na kama vimetokea sehemu ya ubavu yaweza kuwa relapse ya previous HSV infection.

Maambukizi.Ugonjwa huo huenezwa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mtu mwingine kukutana kwa majimaji ya mwili kama mate, maji ya ukeni au shahawa.

Vihatarishi/Risk factors : ni kuwa na ngono zembe mara kwa mara, kuwahi kuumwa magonjwa ya zinaa au maambukizi ya VVU.
Matibabu: Unaweza ukaandikiwa dawa kama acyclovir (Zovirax), famciclovir (Famvir) au AntiVirals nyingine.

Ushauri: Ni vema ukamwona daktari kwa uchunguzi zaidi, na ufikirie kupima maambukizi ya HIV/AIDS ili ufahamu afya yako na ujijengee mikakati kama Other STIs umeshapima.
---
Mkuu huo sio ugonjwa wa zinaa na wala hauhusishwi kabsa na mambo ya ngono,,,, chanzo cha huo ugonjwa ni UCHAFU KUZIDI MWILINI,, na sio kama najiropokea bro naongea kutokana na experience niliyokua nayo, nakumbuka nikiwa nakaa hostel huu ugonjwa ulinipata na sio mm tu pamoja na masela zangu!

Tiba hasa ya huo ugonjwa ni dawa flani hivi ni kimiminika na inarangi ya pink (samahani jina nimesahau) na imetengenezwa hapahapa nchini mkoa wa mwanza, changamoto ya hio dawa ni inaunguza mapumbu kinoma bro na kama umepaka bila kuoga utafrahia show,

Unatakiwa ukishapaka ukae sehemu ambapo kuna upepo mwanana lacvyo unaweza kuunguza hio mali!!! Sina la zaidi bro na polee sana coz huo ugonjwa naujua balaa lake zito
 
Pole Mkuu kwa tatizo linalokusumbua kwa haraka haraka bila kupepesa utakuwa una ugonjwa unaoitwa Genital Herpes infection ambao husababishwa na Herpes simplex virus type 1 & 2 ila kwa upande wako naona ni type 1 and type 2 ndio zinakusumbua, maana nimejaribu kuangalia na hizo blister hapo katika mwili wako zimekaa kama za herpes plus ukijaribu kuvitumbua najua utakuwa unapata maumivu ya ajabu.

Hivyo basi ningependa uende maeneo ya pale Sanitas mikocheni wachukue damu, majimaji kutoka kwenye hivyo viupele, mate, au sehemu kidogo ya ngozi ambayo ina hizo blisters ili waweze kufanya analysis kwa njia ya Polymerase chain reaction (PCR) au hata Serological test (ELISA) ili kuconfirm ugonjwa husika.

Kuhusu tiba incase ikagundulika una herpes infection wanatibu dalili husika, ila kwa hapo baadae utapata long life immunity ambayo itakuwezesha kutokupata huo ugonjwa tena.

NB: Ugonjwa huu madaktari wengi huhisi ni ugonjwa wa fangus, bacterial au ugonjwa wowote wa njia ya mkojo ambapo huwa ni uongo...

Hivyo wahi kwenye hiyo hospitali kama wewe ni mkaaji wa Dar es Salaam uweze pata tiba, kila la kheri boss.
 
Pole Mkuu kwa tatizo linalokusumbua kwa haraka haraka bila kupepesa utakuwa una ugonjwa unaoitwa Genital Herpes infection ambao husababishwa na Herpes simplex virus type 1 & 2 ila kwa upande wako naona ni type 2 ndio inakusumbua, maana nimejaribu kuangalia na hizo blister hapo katika mwili wako zimekaa kama za herpes plus ukijaribu kuvitumbua najua utakuwa unapata maumivu ya ajabu...

Asante sana kaka, ubarikiwe
 
Pole Mkuu kwa tatizo linalokusumbua kwa haraka haraka bila kupepesa utakuwa una ugonjwa unaoitwa Genital Herpes infection ambao husababishwa na Herpes simplex virus type 1 & 2 ila kwa upande wako naona ni type 2 ndio inakusumbua, maana nimejaribu kuangalia na hizo blister hapo katika mwili wako zimekaa kama za herpes plus ukijaribu kuvitumbua najua utakuwa unapata maumivu ya ajabu..

Wanatumia bima hawa watu kaka?
 
Wanatumia bima awa watu kaka?
Ndio Mkuu, Tahadhari tu angalia usishiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga maana uko katika risk kubwa ya kupata magonjwa hatari hasa HIV.

Na Kwa kuongeza hapo kama nilivyokwisha tangulia kusema hapo mwanzo hakuna tiba ya huo ugonjwa kama ikithibitika unao. Hivyo kuna dawa utapewa ni kama zile za Ukimwi mfano Ayclovir (zovirax), famciclovir (famvir) au valacyclovir (Valtrex), hizi dawa zitakusaidia sana maana huwa zinazuia hao vizuri wasiendelee kuzaliana na pia kuepusha wewe kusambaza vizuri hivyo pale utakapokutana kimwili na mwanamke.

Na mara nyingi baada ya kutumia dawa hizi mgonjwa hupata nafuu na kupona kabisa ila ikitokea baada ya kutumia dawa hivyo viupele vikatokea tena basi utaendelea na dawa mpaka pale vitakavyokoma.

Na pia kuhusiana na hivyo vipele ni vyema ukawa unaosha kwa kusugua na maji ya uvuguuvugu yakiwa na chumvi ndani yake kipimo ni chukua kijiko cha chai weka chumvi nusu changanya na maji nusu lita sugua kwa kuosha na kwa maumivu madogo madogo unaweza tumia dawa kama aspirin au acetaminophen utakuwa sawa mkuu..
 
Pole Mkuu kwa tatizo linalokusumbua kwa haraka haraka bila kupepesa utakuwa una ugonjwa unaoitwa Genital Herpes infection ambao husababishwa na Herpes simplex virus type 1 & 2 ila kwa upande wako naona ni type 2 ndio inakusumbua, maana nimejaribu kuangalia na hizo blister hapo katika mwili wako zimekaa kama za herpes plus ukijaribu kuvitumbua najua utakuwa unapata maumivu ya ajabu....
Kiongozi umenena vyema.

Mimi nashauri umuone Dr. Bingwa wa magonjwa ya ngozi. Usiende kwa madokta wa kawaida. Ulizia Dr. Bingwa wa magonjwa ya ngozi. Kwa Muhimbili wanapatikana muda wowote, ila kwa hospitali binafsi wanapatikana jioni.

Ushauri. Kuna ugonjwa unaitwa scabies na madokta wengi huwa wanakosea diagnosis yake kwa sababu ya kutokuwa na dalili hizo hizo kila wakati.

Mimi japo sio Dr. Lakini ningesema kwenye kichwa chako cha uume ni scabies, lakini scabies huwa haina blisters mwili mzima. Sehemu ambazo parasites waliingilia ndiyo huwa panawasha na usiku muwasho unakuwa mkali sana na hizo sehemu zenye muwasho huwa zina viuvimbe kwa sababu ya burrows za wale parasites.

Fanya hima ufanyiwe test. Lakini pia check tena VDRL kuncofirm kama kweli una Sypillis. Katika moja ya hospitali nzuri kwenye vipimo na maabara ni Regency. Kama walifanya kipimo cha Sypillis na hawakuona, basi nasita kusema ni Sypillis. Labda kama hukupimwa huo ugonjwa.
 
Back
Top Bottom