Msaada: Biashara yangu inapata Mauzo hafifu

Decency13

Member
Jun 2, 2023
14
20
Waheshimiwa nahitaji msaada kwenye hili, hivi inakuwaje mtu hauuzi kabisa dukani kwako kwa siku karibia 20 yani kila siku patupu tatizo linakua ni nini?

Binafsi nimefungua frame nauza mitumba ya kike(gauni) lakini niliuza siku 5 za kwanza tu ila sasa hivi mambo magumu mzigo ni kama umechacha sijafikia hata nusu ya gharama za mzigo.
 
Acha Mkuu ,. Nilishawahi experience kitu kama chako, Na biashara inaenda Kwa hasara kubwa

Binafsi nilibadili location, at least nilipo Namshukuru Mungu
Waheshimiwa nahitaji msaada kwenye hili, hivi inakuwaje mtu hauuzi kabisa dukani kwako kwa siku karibia 20 yani kila siku patupu tatizo linakua ni nini?

Binafsi nimefungua frame nauza mitumba ya kike(gauni) lakini niliuza siku 5 za kwanza tu ila sasa hivi mambo magumu mzigo ni kama umechacha sijafikia hata nusu ya gharama za mzigo.
 
Waheshimiwa nahitaji msaada kwenye hili, hivi inakuwaje mtu hauuzi kabisa dukani kwako kwa siku karibia 20 yani kila siku patupu tatizo linakua ni nini?

Binafsi nimefungua frame nauza mitumba ya kike(gauni) lakini niliuza siku 5 za kwanza tu ila sasa hivi mambo magumu mzigo ni kama umechacha sijafikia hata nusu ya gharama za mzigo.
Soma ushauri wa watu ila ukitaka mtaalam kuna mtu namfahamu uzuri
 
jaribu kuweka na uwakala wa simu pesa hapo kwenye fremu weka na bango linaloonyesha hiyo huduma inapatikana, pia changanya bidhaa, tafuta midoli ivalishe nguo weka nje fanya biashara ionekane zaidi,kauli nzuri kwa wateja, kama eneo si la mzunguko wa watu wengi hama apo mapema
 
biashara ya nguo siku hizi ni MTANDAONII NDUGU YANGUUU kama una ofisi ondoa shaka jiongezee funguaa account insta...fb uwe unapiga picha unapost yani utawapata tu wakitaka kuja ofisini unawaelekeza ila usiuzee mironyooo sanaa..!! na uwe muaminifu tu kwa wateja...kule sinza frame kubwa huoni mteja akiingia hata masaa matatu pamepoaa balaaa ila boda wanaenda kupeleka delivery za kutosha. JIONGOZE USIKIMBIE FRAME
 
Mkuu hama hapo kwanza yalishatukuta hayo nilifungua frem Tabata nilikuwa napata hasara mwanzo mwisho. Hapo uondoke ofisi inatakiwa in nature iwe inajitegemea wateja wawepo hiyo ndo faida ya frem.

Than ndo unatumia nguvu za ziada kidogo unaongeza mapato kama kutangaza mtandaoni, mambo yetu yale mvuto kalumanzila au maombi. Hama mkuu ushakosea Location.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom