Mrisho Gambo: Ninao ushahidi wa watu waliotapeliwa Magari na Godbless Lema

Siasa za Arusha tuachie sisi wenyewe wapiga kura wa Arusha mjini.
Huyo Gambo asubirie kuteuliwa viti maalumu.
Tunasubiri uchaguzi kwa hamu kubwa tumuoneshe hasira zetu.
Issue ya mtu kuacha familia yake ughaibuni ni mambo binafsi.
Suala la Lema kiwa na kazi au kutokuwa na kazi mimi hakinisaidii kitu maana sijawahi kumlisha Lema wala hajawahi kuniomba kitu.
Suala la kudhulumu magari hao wenye ushahidi waende mahakamani Lema ashtakiwe.
Mengine ni propaganda za kindezi tu.
Umemaliza mkuu,
Ni aibu kubwa sana kiongozi kuongea majungu badala ya kuongelea mikakati ya maendeleo ya wananchi wake.
Kweli ccm ni janga la Taifa, Mungu tunusuru na hili janga.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katika mahojiano yaliyofanywa kati ya mwanahabari Odemba na Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Mrisho Gambo ameeleza mambo mengi sana kuhusu mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini. ambapo ameeleza bila kusita wala hofu kuwa anao ushahidi wa kutosha wa watu waliotapeliwa Magari na Godbless lema,amesema hata leo hii anaweza kuutoa ushahidi huo ikiwa utahitajika, amesema hata sasa anahofia kuwa pengine Lema anaweza kuwa ameirudia kazi yake hiyo ya zamani maana kwa sasa hana kazi ya aina yoyote ile anayoifanya hapa nchini na hata ukimuuliza anafanya kazi gani hawezi kukwambia.

Ameeleza zaidi pia kuwa mbunge huyo anapenda sana dezo na mteremko ,na ndio maana ameshindwa hata kuilea familia yake na kuamua kuitelekeza nje ya nchi ambako inalelewa huko na watu.amesema kuwa anashangaa na kumshangaa kuwa Lema ni mchaga wa aina gani ambaye anashindwa hata kulea tu familia yake, maana wachaga wamezoea upambanaji tofauti na yeye lema anayependa dezo na mteremko kwa kila kitu.anasema alikimbia kwa visingizio lakini Rais Samia alipoingia madarakani akasema njooni nchini tujenge nchi yetu, lakini kwa kuwa Lema anapenda mteremko ameona familia yake ibaki huko huko inakolelewa bure.

Amesema mbona watu kama Mbowe au John Heche Wana familia zao hapa hapa nchini? Amesema kwani kuna tatizo lipi nchini kwa sasa? Amesema ni kutanga tanga na kuhangaika na kukosa kazi za kufanya kwa Lema ndiko kunakomfanya aogope hata kuleta familia yake nchini maana anajuwa watamdai mahitaji kama vile ada za shule na mahitaji mengine ndio maana anaamua aiche huko huko wanakomsaidia kulea.

Amesema kwa sasa Lema hata jimbo tu la kugombea haelewi agombee lipi maana anatanga tanga kwa kusema mara anataka kugombea hai ,mara atafute jimbo Dar .anasema anatanga tanga kwa kuwa hana kazi za kufanya na anaona Ubunge ndio ponea yake ya kuendeshea maisha yake .

Mimi mwenyewe namuunga mkono Mheshimiwa Mrisho Gambo kwa sababu haiingii akilini mtu alisema amekimbia nchi kwa sababu anawindwa na kukimbilia huko nje ya nchi nakuomba kusaidiwa kulishwa na mahitaji mbalimbali yeye na familia yake.lakini Dkt Samia alipoingia madarakani akasema njooni tujenge nchi yetu ,lakini cha ajabu baada ya kunogewa na mteremko wa kupewa msaada na matunzo na mahitaji yote kutoka kwa wazungu amegoma kabisa kuirejesha familia yake na badala yake karejea mwenyewe nchini nakuja kuwaporomoshea matusi watanzania kuwa kazi wanazofanya ni za laana na za kimaskini.

Kwa hakika ni jambo ambalo wana Arusha hawata kaa wasahau matusi haya waliyotukanwa na Lema ambaye walimchangiaga mia mia zao mpaka akapata ubunge na kwenda kula pesa bungeni, bila kuwatumikia wala kuwapelekea maendeleo ya aina yoyote ile zaidi ya kufanya mivurugu kuanzia Bungeni mpaka mitaani. Kwa hakika wana Arusha walikuwa sahihi kabisa kumfurusha Arusha mjini kwa kumnyima kura za ndio.kwa sasa akatafute kwa kugombea maana Arusha hakuna wa kumpatia kura maana alishawaambia kuwa wao ni maskini na wanafanya kazi za kimaskini ,ilihali alikuwa mbunge kwa miaka kumi na hakuwasaidia kwa chochote zaidi ya kuja kuwatukana tu baada ya kurejea kutoka kwa wazungu alikokuwa akilishwa na kuhudumiwa kwa kila kitu kama kuku wa kisasa wasio weza jitafutia chakula chao au Makinda ya ndege.

Sasa mwakani Ubunge hapati wala nini ili arudi huko huko kwa wazungu.maana hakuna wa kumpatia kura ili aje kuwalipa kwa matusi na kuwadhalilisha kama alivyokwisha kufanya baada ya kuwa amevimbiwa na kuzidiwa na shibe na kusahau alikotokea kisiasa na kimaisha.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
halafu ungeacha kutumia neno ndugu zangu watanzania...aisee sisi hatuna undugu na watu wa caliber yako....
 
Gambo ajikite kwenye hoja za maana watu wa arusha watamwelewa akianza namna hii asahau kupata ubunge hapo A town mwakani. Hilo jimbo halinaga mwenyewe atambuwe hilo.
Arusha haina mwenyewe!! Ila ccm ilishakataliwa arusha tokea enzi ya chama kimoja,kumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi arusha mjini lilikuwa jimbo pekee lililokuwa na vurugu nyingi ccm wakizuia upinzani usichaguliwe,hawakuweza makongoro nyerere akashinda kwa tiketi ya nccr.
 
Yeye kaeleza UKWELI ulio wa wazi. Naomba nikuulize maswali madogo tu ,yaliyoulizwa na Mheshimiwa mbunge kuwa kwanini lema hajaja na familia yake Nchini? Anafanya kazi gani nchini unayoifahamu wewe binafsi. Nje na siasa ya kupiga mdomo na porojo za uongo na kutukana watu ana kazi gani nyingine ya kulipa hata kodi serikalini.
Achen ujinga, mambo ya ndani ya familia ya mtu kuihoji ni utoto na ujinga. Leo kuna watu wanaishi Dodoma kikaz na familia zao zinaishi Dar, hii inatofauti gan na issue ya Lema. Acha kujadili personalities jadili issues. Gambo unasumbuliwa na ugonjwa wa kisiasa (election fever)

Anayo matatizo makubwa sana na CCM yake kuliko huyo anayemchokoza. Gambo aeleze alichokifanya sio mshindan wake wa kisiasa.

Kwanza inawezekana hata CCM yake isimpitishe kutokana na utoto na ujinga mwingi alionao. Siasa za Gambo cku zote ni kununua uhasama. Alianza na DED wa Arusha mjini na watu wengine. Kila cku kwake ni Drama na watu. Lema kajituliza yeye anaangaika tu. Ni mtu hopeless kabisa
 
Kwanini huyo Gambo asikutanishwe na Lema siku moja hapo studioni?
Naona kama mwandishi nae hawezi kuseti mahojiano vizuri
 
Hata pasipo kukutanishwa .Lema anaifahamu vyema sana tabia hiyo na kazi hiyo aliyokuwa akiifanya awali kabla ya kuwa Mbunge.
 
Hatumtaki huyo gambo mbwa kabisa nimempigia simu zaidi ya mara 10 anazingua kujibu KERO za hapa sinoni

Matak* kabisa
Kwa hiyo mtu akiwa bungeni apokee simu yako mbele ya bunge? Au ulikuwa na mambo yako? Mheshimiwa Mrisho Gambo ndio Mbunge wako ajaye kwa awamu nyingine tena. Wana Arusha hawapo tayari tena kuongozwa na tapeli.
 
Yeye kaeleza UKWELI ulio wa wazi. Naomba nikuulize maswali madogo tu ,yaliyoulizwa na Mheshimiwa mbunge kuwa kwanini lema hajaja na familia yake Nchini? Anafanya kazi gani nchini unayoifahamu wewe binafsi. Nje na siasa ya kupiga mdomo na porojo za uongo na kutukana watu ana kazi gani nyingine ya kulipa hata kodi serikalini.
Wewe familia ya Lema inakuhusu nini? ya kwako tunaijua?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katika mahojiano yaliyofanywa kati ya mwanahabari Odemba na Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Mrisho Gambo ameeleza mambo mengi sana kuhusu mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini. ambapo ameeleza bila kusita wala hofu kuwa anao ushahidi wa kutosha wa watu waliotapeliwa Magari na Godbless lema,amesema hata leo hii anaweza kuutoa ushahidi huo ikiwa utahitajika, amesema hata sasa anahofia kuwa pengine Lema anaweza kuwa ameirudia kazi yake hiyo ya zamani maana kwa sasa hana kazi ya aina yoyote ile anayoifanya hapa nchini na hata ukimuuliza anafanya kazi gani hawezi kukwambia.

Ameeleza zaidi pia kuwa mbunge huyo anapenda sana dezo na mteremko ,na ndio maana ameshindwa hata kuilea familia yake na kuamua kuitelekeza nje ya nchi ambako inalelewa huko na watu.amesema kuwa anashangaa na kumshangaa kuwa Lema ni mchaga wa aina gani ambaye anashindwa hata kulea tu familia yake, maana wachaga wamezoea upambanaji tofauti na yeye lema anayependa dezo na mteremko kwa kila kitu.anasema alikimbia kwa visingizio lakini Rais Samia alipoingia madarakani akasema njooni nchini tujenge nchi yetu, lakini kwa kuwa Lema anapenda mteremko ameona familia yake ibaki huko huko inakolelewa bure.

Amesema mbona watu kama Mbowe au John Heche Wana familia zao hapa hapa nchini? Amesema kwani kuna tatizo lipi nchini kwa sasa? Amesema ni kutanga tanga na kuhangaika na kukosa kazi za kufanya kwa Lema ndiko kunakomfanya aogope hata kuleta familia yake nchini maana anajuwa watamdai mahitaji kama vile ada za shule na mahitaji mengine ndio maana anaamua aiche huko huko wanakomsaidia kulea.

Amesema kwa sasa Lema hata jimbo tu la kugombea haelewi agombee lipi maana anatanga tanga kwa kusema mara anataka kugombea hai ,mara atafute jimbo Dar .anasema anatanga tanga kwa kuwa hana kazi za kufanya na anaona Ubunge ndio ponea yake ya kuendeshea maisha yake .

Mimi mwenyewe namuunga mkono Mheshimiwa Mrisho Gambo kwa sababu haiingii akilini mtu alisema amekimbia nchi kwa sababu anawindwa na kukimbilia huko nje ya nchi nakuomba kusaidiwa kulishwa na mahitaji mbalimbali yeye na familia yake.lakini Dkt Samia alipoingia madarakani akasema njooni tujenge nchi yetu ,lakini cha ajabu baada ya kunogewa na mteremko wa kupewa msaada na matunzo na mahitaji yote kutoka kwa wazungu amegoma kabisa kuirejesha familia yake na badala yake karejea mwenyewe nchini nakuja kuwaporomoshea matusi watanzania kuwa kazi wanazofanya ni za laana na za kimaskini.

Kwa hakika ni jambo ambalo wana Arusha hawata kaa wasahau matusi haya waliyotukanwa na Lema ambaye walimchangiaga mia mia zao mpaka akapata ubunge na kwenda kula pesa bungeni, bila kuwatumikia wala kuwapelekea maendeleo ya aina yoyote ile zaidi ya kufanya mivurugu kuanzia Bungeni mpaka mitaani. Kwa hakika wana Arusha walikuwa sahihi kabisa kumfurusha Arusha mjini kwa kumnyima kura za ndio.kwa sasa akatafute kwa kugombea maana Arusha hakuna wa kumpatia kura maana alishawaambia kuwa wao ni maskini na wanafanya kazi za kimaskini ,ilihali alikuwa mbunge kwa miaka kumi na hakuwasaidia kwa chochote zaidi ya kuja kuwatukana tu baada ya kurejea kutoka kwa wazungu alikokuwa akilishwa na kuhudumiwa kwa kila kitu kama kuku wa kisasa wasio weza jitafutia chakula chao au Makinda ya ndege.

Sasa mwakani Ubunge hapati wala nini ili arudi huko huko kwa wazungu.maana hakuna wa kumpatia kura ili aje kuwalipa kwa matusi na kuwadhalilisha kama alivyokwisha kufanya baada ya kuwa amevimbiwa na kuzidiwa na shibe na kusahau alikotokea kisiasa na kimaisha.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

=====

“Godbless Lema anatanga tanga hayupo Duniani hata ahera hayupo, ni mtu anayependa mteremko, Lema anapenda dezo, hana mvuto, amewatapeli watu Magari Arusha na ushahidi ninao, hana kazi ya kufanya amekuwa kama jina lake… Godbless - Jobless” MRISHO GAMBO

Gambo amemrahi lema ahache kuwatesa watoto wake kwa kukaa Nchi za watu kwa sababu zake za kisiasa, arudishe watoto Nyumbani kwani Arusha hakuna shida yoyote, hayo mambo anayoyafanya ni aibu kwa kabila lake la wachaga, “wachaga si watu wa kulelewa, sijui hiyo tabia Lema ameitoa wapi” ….?

Ikifika hatua ya mtu kutoa kafara familia yake kwa maslai ya kisiasa huyo mtu anapaswa kuombewa, Odemba kama Lema ni rafiki yako mwambie Arudishe watoto wakamsalimie Babu yao..! Gambo.
View attachment 2940724
Anawewesekaaa peke yake
 
Back
Top Bottom