Mr. II aibuka dhidi ya Zinduka!

Madai ya MR II yanafunua kwa upana zaidi yaliyokuwa yamejificha katika tamasha lile..

Nilijiulizaa sana iweje tamasha la kuhamasisha na kuelimisha kuhusu janga la malaria baadhi ya watu waingie kwa kiingilio??? Je VIP group ilikuwa ina umuhimu gani katika Tamasha la aina ilee???

Kama Taifa shughuli yenye kumhusisha mkuu wa nchi kama mgeni Rasmi na kuhudhuriwa na halaiki ya umma lazima iwe na masilahi ya Taifa mbele na sio kikundi cha watu!! hapa kuna protokali inayotakiwa kulitambua hili na kulisimamiaa..halikufanyika.

Wale wote wanaofanya kazi IKULU kwa nafasi yeyote ile katika kumsaidia Mh Raisi utekelezaji wa majukumu yake wasitumie nafasi hizo kujinufaisha au kujipatiaa umaarufuu binafsi.. Natumai kama kuna kanuni za kazi IKULU huenda hili limebainishwa na kama halipo liangaliwee upya!!

Ni aibu kama Taifa kuwepo kwa madai kama haya katika tukio ambalo Mkuu wa Nchi aliongozaa ufanyikaji wake..Mh Raisi uwe unajiridhisha zaidi katika kushiriki masuala mbali mbali yenye masilahi ya kitaifa kwa kudadisii maudhui na mwelekeo wa tukio zima..Zana unazo ni kuzitumia tuu ukitaka!
 
Hata mimi ningekuwa MR. II ningekwenda mahakamani, huu ni wizi wa fikra za watu.
 
Ukishangaa ya Mussa utayaona ya Firauni,

Kikwete kuingizwa mikenge si ndio zake, kwani umesahau sakata la hotel Arusha, Kivuko kule Mto Ruvuma.... huyu amejizungushia kina Sheikh Yahya Hussein, hawezi kuyaona mambo katika mstari wake.

Sugu moto chini, asante kwa kuendelea na vita hii.
 
Ina maana rais hana Usalama wa Taifa wanaopaswa kugundua mambo feki kama haya ili yasimtie aibu?Walishindwa kweli kujua kama hili ni famba tu? Kama itakuwa ndo hivi si atakuja kudhurika siku moja?
 
Uzinduzi wa Kampeni dhidi ya Malaria ulitakiwa ufanyike kwenye viwanja vya Jangwani mchana kweupe na si gizani huko leaders club na wananchi kutakiwa kutoa viingilio! Kitu kingine kinachoshangaza ni kwamba hivyo vyandarua vya bure kutoka US vinauzwa Kariakoo mtaa wa Congo mchana kweupe ndani ya magari kwa bei ya Sh. 6,000 kila chandarua. Hao akina mama wajawazito tangu wanaanza clinic wanapewa ahadi tu za kupatiwa vyandarua lakini mpaka mtoto anazaliwa hakuna chandarua chochote wanachopata.

It is a shame really! Bush anajua vyandarua vinatolewa bure kumbe vinauzwa tena vikiwa vimeandikwa FREE NETS!
 
Ukishangaa ya Mussa utayaona ya Firauni,

Kikwete kuingizwa mikenge si ndio zake, kwani umesahau sakata la hotel Arusha, Kivuko kule Mto Ruvuma.... huyu amejizungushia kina Sheikh Yahya Hussein, hawezi kuyaona mambo katika mstari wake.

Sugu moto chini, asante kwa kuendelea na vita hii.
uuuuh!!!
am tired and confused totally and completely!!!
ujanja ujanja wa kipumbafu, wizi wizi, ubinafsi!!!
daaaaaaaaamn!!!
 
Ina maana rais hana Usalama wa Taifa wanaopaswa kugundua mambo feki kama haya ili yasimtie aibu?Walishindwa kweli kujua kama hili ni famba tu? Kama itakuwa ndo hivi si atakuja kudhurika siku moja?
Usalama wa Taifa wa taifa hili ni watu wa hatari sana, wao wapo kulinda usalama wa chama Tawala, na ukitaka kujua ni Genge la watu waajabu ebu leo ibuka na ufichue wezi wa mali za umma, kweli watakukamata, watakutesa, watakuandama ile mbaya.

Sasa kwasababu wako busy na mambo yasiyo na maana, wako busy kutaka kujua CCJ ni kina nani...

Pamoja na lawama hizo dhidi ya UWT, lakini turudi katika uwezo wakuona mambo wa JK, kama kweli anaona UWT wanamtia fedheha kwanini mpaka leo hamuwajibishi mkurugenzi wao, ama watendaji wengine ili mambo yaende sawa..... ila mimi kuna jambo nahisi, anamsikiliza sana Sheik Yahya, huenda ndie anaemshauri....Tanzania bana.
 
Hao CLOUDS wamezoea kuwaibia wasanii na ukikataa wanagoma kupiga nyimbo zako walishafanya hivyo kwa TID,Dudubaya,Sugu,Kikosi cha Mizinga na wasanii wengine.

Mr II wasaidie hao wasanii waweze hata kudai haki zao
 
i) Je ni kweli nyimbo za Mr II huwa hazipigwi Cloud FM?

HAZI-PI-GWI-GWI KABISA...... Hahaaa...yaani bifu la kufa mtu

....................................
Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
MM usisahau kuwa January Makamba anasema ametumwa na mkulu kwenda kumn'goa Shulukindo huko Bumbuli kwahiyo hiyo dili inawezekana ikawa ndio katika kuchangisha pesa za kugombea ubunge; January asingeweza kupata mshiko kama dili ingepitia kwa Mr.11 kwahiyo akaipitisha kwa Ruge!! Na hao wakina January ndio sampuli ya vijana watawala wanataka kuwarithisha nchi!!!

Imeshasemwa kuwa "adui wa adui yako ni rafiki".

Nafikiri kama kuna mtu hii kesi angelifurahia kuwa Mr.II anashinda ni Shelukindo.

Sifahamu hata kama anafahamu juu la hili. Hii ni nafasi pekee ya kumdhoofisha mpinzani wake ambaye anakuja kwa kutumia mgogo wa MTANDAO.

Kama hii iliyosemwa hapa ni kweli kuhusu huyu mtani wangu January Makamba na hayo aliyotufunulia MMkjj kuhusu dada mtu ............. wa Msingi wa Voda na uje ujumlishe na tabia ya baba mtu, hii familia lazima nikiri IMEJALIWA.
 
imejaaliwa wasanii wenye vipaji maalum. (am wondering who is the mama)
 
Hao CLOUDS wamezoea kuwaibia wasanii na ukikataa wanagoma kupiga nyimbo zako walishafanya hivyo kwa TID,Dudubaya,Sugu,Kikosi cha Mizinga na wasanii wengine.

Mr II wasaidie hao wasanii waweze hata kudai haki zao

Hivi ilikuwa busara pia kwenye ile Red Alert longolongo kuwalazimisha wasanii wachangie vinginevyo nyimbo zao hazitapigwa??? (am just curious)
 
Pasco,

Mie ni mpenzi na mfuatiaji sana wa miziki. Nimesoma na kusikiliza historia nyingi sana ya miziki na hasa unapokuja ugomvi kati ya wanamuziki na hawa Producer/promotors.

Nafikiri moja ya producer wakorofi alikuwa Dodi Cox ambaye aliwatengenezea album ya kwanza akina Bob Marley, Peter MacnTOSH na Bunny Wailer. Jamaa walifanya kazi mwaka mzima na imefika X-mas wanataka warudi nyumbani, jamaa akawapa pesa kidogo kiasi kwamba walimrushia usoni na wakaondoka na milele hawakurudi tena. Lakini hapohapo wakakutana na Chris Blackwell wa Islands Rec. (now under Def Jam) ambaye wameshirikiana naye kwa miaka mingi na hadi leo kama sikosei familia yake bado wanashirikiana naye na huyu jamaa anaheshima sana kwa watu wa kawaidia kwani alikuwa akiuma ndiyo ila anajua kupuliza.

Kuna kesi ya Marion Suge Knight ambaye ubabe wake ulimkimbiza kabisa kwenye muziki mwimbaji kama Vanilla Ice. Alikuja kuwafanyia mbaya zaidi akina Snoop na Dr. Dre na wengine wanasema ndiye aliwatanguliza 2Pac na BIG. Snoop na Dre kabla ya hapo walikuwa kwa mjinga mwingine aitwaye Easy E. Huyu jamaa na yeye alikuwa anawatreat kama wao ni MALI YAKE.
Kiboko cha yote ilikuwa kipindi wametangaza kuwa TLC wamefilisika wakati dunia nzima wananunua CD zao. Hapo ndipo ikabidi sasa USA kufanyike sheria kali sana kuwatetea wanamuziki. Hadi leo kama sikosei ni MJJ ndiye alikuwa anachukua hela nyingi kwa kila produced CD yaani $1. Wengine kama sikosei ilikuwa andikwa kuwa Min. wachukue $0.30 kwa CD na si chini ya hapo.

Ukirudi kwa Tanzania, kusema kuwa JD kafanikiwa, ni sawa na kusema wakati MJJ yuko juu sana akiwa chini ya SONY ya shemeji Motola, wanamuzi kama George Michael alikuwa na ugomvi mkubwa sana na Sony na hadi akagoma kuzalisha mziki.

Ukweli ni kuwa ni biashara ngumu sana na wanatumia hela nyingi katika kuzalisha, kusambaza, kuuza na kutanga miziki, ila upande mwingine ni lazima nchi iunde sheria kuwalinda wanamuziki. Kama hii ya kugomea kupiga mziki wa mtu, naona ni utoto wa hali ya juu. Mbona hatuoni MTV wakimgomea Taahira Kanye West? Na jamaa kashawaaibisha/ kajiaibisha si mara moja na kuwapa maneno yao LIVE.

Wanamuziki/Wasanii wa Tanzania lazima waungane na watafute wanasheria wa kuwalinda. Nafahamu kuna wengine wataona hilo wao haliwahusu kwani wana majina tayari ila hao watakaoungana, wataweza kuwa na sauti kwa mfano kuiambia Clouds kuwa kama hupigi miziki ya mtu fulani basi sisi wote tunaondoa miziki yetu. Hii ikifanywa kwa ushirikiano, wataweza kufanikiwa.

Na hii tunayoiona hapa Tanzania ni cha mchezo tu na wenzentu walishapitia huko zamani sana na walishauwana sana tu na hadi leo hii kuna wengine wanaogopa kabisa kushika Mic kwani mabwana zao watakuja hapohapo na kudai kipato chao chote. Kama hii isipotulizwa mapema, basi tusishangae tukafika huko very soon kwenye kutishiana maisha au kuuwana.
 
...Nadhani tatizo hapa ni kwa wasanii kutojua haki zao na pia kutofahamu mantiki nzima ya hatimiliki.

Mr II alitakiwa kusainiana makubaliano na wahusika kabla ya kuanza kujadili mpango. Makubaliano haya yangewafunga wahusika kutojadili, kuanzisha mpango unaofanana na huo kwa njia yoyote ile kwa kipindi cha muda fulani.

Kama hakufanya hivyo, itakuwa ngumu sana kupata haki mahakamani.
 
imejaaliwa wasanii wenye vipaji maalum. (am wondering who is the mama)

Siyo vipaji. Maana labda angelitokea mmoja awe tofauti basi tungelisema ni vipaji.

Hawa jamaa WAMEJALIWA KIPAJI. Wote wanacho hicho hicho.
 
mpakaleo nashindwa kujua kama tamasha la 'zinduka' ni biashara au msaada wa kupambana na malaria?

hayo mengine ya madili au nini ni kawaida nchini kwetu sema hapa kidogo wamefika mbali kama lengo lilikuwa msaada wakahamua kufanya biashara.

hile siku kama ilikuwa ni harambee basi walalahoi walijichangia 3000 wasubiri net zao za mbu zinakuja ,kama ilikuwa ni introduction wa msaada wa vyandarua basi sh 3000 zao ni takrima na net za mbu wameenda kuzijaribu VIPs kama zinafaa kabla ya kuwapa walalahoi.
Nasikia hasira ya kuua mtu...:(
 
Wapi tunaelekea kama taifa?

Mwanzoni niliposikia nilidhani majungu maana waosha vinywa huwa hawalali lkn niliposikia kuwa kuna kiingilio kwenye hilo tamasha ambalo Rais alitoa tamko kuwa malaria sasa ni janga la kitaifa haikuniingia akilini kabisa. Nilijiuliza maswali bila kupata majibu kwamba Rais kabla ya kuhudhuria shughuli hiyo alifahamishwa kuwa hilo lilikuwa tamasha la kuonyesha vibaji vya vijana wetu wa bongo fleva na wajasiriamali wanaonatafuta mkate wao wa siku maana kwa shughuli zote zihusuzo uhamasishaji tena wa majanga kwa taifa tumezoea kusikia zikifanyika Mnazi Mmoja bila kiingilio tena watu tutapewa vipeperushi ikibidi na fulana ili kuhamasika zaidi na hao wabongo fleva kutuelimisha kupitia tungo zao.

So kuanzia mwanzo mpangilio mzima wa hiyo shughuli ulikuwa na dosari ambazo sitaki kuamini kama mheshimiwa alikuwa akizifahamu lakini akazifumbia macho ila kilichonishtua na kunitoa kwenye usingizi ni kusikia likitajwa jina la mtoto huyu wa kigogo tena inasemwa kuwa ni mtumishi wa nyummba ile tukufu (ikulu) January Makamba. Sio vibaya kwake kufanya kazi pale kama sifa anazo bali hofu yangu ni kwamba anaitumia vibaya hiyo nafasi nyeti aliyopewa baada kugeuza ikulu kuwa kituo chake cha biashara kwa sababu tu baba yake ni swahiba wa mheshimiwa hivyo anaweza fanya lolote na asitokee mtu wa kumkemea, ni aibu.

Turudi kwa Mr. II au Sugu kwa jina lingine, pole swahiba wangu. Nitakushauri uende mahakamani kama formality tu maana umeonewa kwa mujibu wa kauli yako ila naingiwa nashaka kama kweli utaipata hiyo haki huko unakoifuata maana kama umepingwa ngwala na jamaa wa ikulu tu ambako tunaamini hawawezi kufanya hayo waliyoyafanya basi kuhamia kwenye muhimili mwingine hakutobadilisha kitu maana hao jamaa wana nguvu za kuogofya.

Nisingependa kumtuhumu Ruge moja kwa moja maana kama ni deal basi yeye amepigiwa pande na hao vigogo ambao kwa namna moja ama nyingine ni maswahiba zake. Sugu wewe piga kazi tu nyingine utatoka usijali maana hata kina 50 cent iliwachukua muda sana hadi game kuwalipa.

Labda cha msingi mbadilike (wasaniii) kwa kuendesha mambo yenu kisomi kidogo sio lazima muende wote shule ila jaribuni kuwatumia wataalamu kwenye nyanja za biashara na sheria badala kufanya kazi kishkaji mtatoka tu.
 
Ukishangaa ya Mussa utayaona ya Firauni,

Kikwete kuingizwa mikenge si ndio zake, kwani umesahau sakata la hotel Arusha, Kivuko kule Mto Ruvuma.... huyu amejizungushia kina Sheikh Yahya Hussein, hawezi kuyaona mambo katika mstari wake.

Sugu moto chini, asante kwa kuendelea na vita hii.
Sugu peke yake hantoweza......hii ni vita kubwa siyo nyepesi kiasi hicho!!!
 
Back
Top Bottom