Gamba,Kama mlidhani Globalization lelemama basi mlikosea, Cha msingi ni kutafuta namna ya kusurvive na kujiletea maendeleo popote duniani. Mipaka ya kisiasa huko mbeleni itabaki kwenye ramani tu ila wanadamu watajichanganya tu. kwa sababu alichokifanya mchina huyo mpiga debe kinaweza kufanywa na Mzambia, Mganda, Mrundi na tusione ajabu sana lakini kwa sababu Mchina anaonekana na rangi kidogo tofauti na sisi basi tunaona ajabu kweli kweli.
Kiufupi ni kwamba Mchina kupiga debe ni kwa sababu amekuta Watanzania wanapiga debe na biashara zao zinatoka, angekuta Watanzania wanafanya booking online naye bila shaka angeanzia hapo kwa huduma zake. sasa iweje Mtanzania kupiga debe iwe sawa lakini mchina kupiga debe si sawa wakati wote wanagombania wateja walewale?.
Leo asubuhi nilikuwa nasindikiza wageni kuelekea bara (mkoani). Nikiwa ndani ya stendi ya mabasi ya Ubungo kiasi cha saa 11:15 (kumi na moja na robo alfajiri) nilikumbana na mpiga debe wa kichina akiniaambia 'lipo basi la Obama hapa linakwenda Mbeya hadi Tunduma" (lafudhi ya kihuuhii). Sikuamini ilibidi nisimame nihakikishe anayoyasema. Baada ya kudadisi nikaambia hao wachina (walikuwa watatu) unaowaona wanamiliki hilo basi (pembeni yetu) lenye rangi za bendera ya USA linalofanya safari zake Dar-Tunduma.
Jamani, hivi kweli mchina ananunua basi na anaajiri mpiga debe mchina, mkata tiketi mchina, vibari vya kufanya uhuni huu wanapata wapi?
Kweli mtanzania unaweza kwenda nchi za watu ukafanya hivi?
Hawa wako Ubungo, si muda mrefu tutawaona kwenye ofisi za ATCL, manake wako katika mazungumzo na Serikali ili wawekeze, watamiliki hisa 49% na Serikali 51%.
Tatizo si hawa jamaa kufanya biashara ya basi lao. Lakini jee tuna sera gani kulinda ajira za wazawa?, tunapoangalia Utandawazi (Globalization) lazima pia tuwe na sheria za kumlinda raia wa kawaida, ikumbukwe kama hatutakuwa na sheria za kutulinda, wenzetu wana mitaji hivyo wanaweza kuja kufanya ama kuchukua kila kitu.
Hakuna ubaya mgeni yeyote kufanya biashara TZ kama amefuata sheria za nji hii, na analipa kodi, hata kama wanauza mchicha, wachina wako safi kuliko hata jirani zetu wababaishaji. Ni changamoto na kichocheo kwa sisi wabongo ambao bado tumelala fofofo. Wabongo kazi yetu ni kukwepa kodi na uvivu tu,na kualalamika kila kukicha, uharibifu unaofanywa na waTZ ni mkubwa kuliko wanaofanya wageni.
Chief naomba utufahamishe yafuatayo maana wewe umesha onja hiyo huduma yao:--
1. Nauli (kutoka DAR -MBY-TND) ukilinganisha na mabasi mengine (ya kiswahili - aka wazawa)
2. Mwendo wa Mabasi haya (ya wachina - aka wawekezaji)
3. Huduma (kuanzia, kupiga debe, kukata ticket, ndani ya basi, mizigo, kusimamisha abiria nk nk)
4. Vp yakifika kwenye mizani kuna abiria wanashushwa?
5. Je wanafuata ratiba waliyopangiwa ya kusafiri? (mda uliopangwa DAR-TDM unatumika vilivyo)
6. Vp kuhusu wateja....wanapata au wanapelaka basi tupu?
Baada ya kuyafahamu hayo basi tufanye kulinganisha na huduma za mabasi ya wawekezaji wazawa ambayo tunayajua vizuri. Baada ya hapo sasa tuendelee na kudiscuss je uwepo wao una manufaa?
Asante.
Sasa kama sisi Watz tumelala- je wao wafanyeje?
Hapana aisee, hatujalala. Tumekuwa sidelined na serikali yetu tuliyoiweka madarakani kulinda maslahi yetu. Jambo hilo limeendelea siku nyingi na wasiwasi wangu ni kuwa linaweza kutufanya siku zijazo tugeuke kuwa kama Somalia.
Leo asubuhi nilikuwa nasindikiza wageni kuelekea bara (mkoani). Nikiwa ndani ya stendi ya mabasi ya Ubungo kiasi cha saa 11:15 (kumi na moja na robo alfajiri) nilikumbana na mpiga debe wa kichina akiniaambia 'lipo basi la Obama hapa linakwenda Mbeya hadi Tunduma" (lafudhi ya kihuuhii). Sikuamini ilibidi nisimame nihakikishe anayoyasema. Baada ya kudadisi nikaambia hao wachina (walikuwa watatu) unaowaona wanamiliki hilo basi (pembeni yetu) lenye rangi za bendera ya USA linalofanya safari zake Dar-Tunduma.
Jamani, hivi kweli mchina ananunua basi na anaajiri mpiga debe mchina, mkata tiketi mchina, vibari vya kufanya uhuni huu wanapata wapi?
Kweli mtanzania unaweza kwenda nchi za watu ukafanya hivi?
Mkuu ndo raha ya utandawazi hiyo.Wabongo wangapi wapo south wanapiga kiwi?
Wabongo wangapi wapo USA wanabeba box?Mbona wao hawalalamiki waache waje tu imradi hawavunji sheria za nchi tena mabus yao very luxury mazuri sana.
Basi hilo ni zuri sana. Nilipanda kwenda Mbeya majuzi. Ni fully airconditioned (inafanya kazi), reclining seats (2X2) na toilet ndani.
1. Nauli = Nililipa Shs 30,000
2. Mwendo = Yako fast kwa kweli ingawaje huwezi ku-feel. Nilikaa mbele na maximum speed as per the speedometer ni kms 140 kwa saa na jamaa alikuwa anafikisha hapo. Scania bus hazifui dafu kwenye tambarare. Engine: Ni Cummins kutoka USA. Drawback: Zina air suspension hivyo kwenye mashimo kidogo inabidi aende mwendo wa wastani kwani zinanepa sana.
3. Huduma = Nzuri. Reclining seats. Wanatoa free soft drinks. Hakuna kusimama. Kuna toilet ndani. Nilimtuma mtu kukata tiketi hivyo sijui huko kituoni.
4. Kuna kushushwa kwenye mizani/abiria kuletwa mbele ya basi kwani ina engine nyuma. Nafikiri huchukua mizigo mingi kweye buti.5. Siwezi kusema kuhusu ratiba kwani sijui wanatakiwa kufika saaa ngapi.
6. Wateja = Nadhani wanapata ingawaje competition ni kubwa sana kwa mabasi ya Mbeya/Tunduma na ndio kwanza wameingia kwenye biashara. Angalau tulikuwa tumejaa kwenye basi.