Mpiga debe wa Kichina stendi ya Ubungo

Wabongolala bado tupo usingizini( sina maana ya usingizi wa kufumba macho, bali usingizi wa akili, akili zimelala yaani bongolala). Sasa tuamshe akili zetu tuache longolongo na tufanye kazi kwa bidii.
 
Sheria zetu za Barabarani kuhusu uzito nafikiri zina muskeli kidogo, kuna siku nilipanda Bus la Kilmanjaro la kutokea Arusha kufika mizani ya pale njia panda ya Himo wakasema uzito umezidi, wakati basi halikuwa limejaa abiria wala mizigo. kudadisi Dereva akasema lile bus siku zote huonekana hivyo na ndio sababu hawakujaza abiria wala mizigo mingi ila limejengwa Injini iko nyuma na pia mtambo wa kiyoyozi(AC) uko nyuma pia Tanki la mafuta, hivyo kusababisha likaonekana ni zito zaidi nyuma. inaonekana kuwa vipimo vyetu si sawa maana bus limekuja kutoka kiwandani likiwa na viwango standard, sasa ukianza safari ndefu inakubidi Mafuta ujaze full tank kabla ya kuvuka mizani. sijui ni kigezo gani wanatumia kuweka kiwango vya uzito wa bus.
 
Naomba kutofautiana na wachangiaji wanao support wachina kufanyakazi za upigadebe hapa Tanzania.Ningependa wachina waje kwa wingi hapa Tanzania kufanyakazi za kitaalamu kama ujenzi,utengenezaji wa mitambo na kazi nyingine zinazohusiana na utaalamu.Leo kama tunashangilia wachina kufanyakazi za wapiga debe nadhani tunatakiwa kujiangalia na kujipanga vyema kwasababu hizi kazi za wapiga debe tunazipiga vita si kwa wachina tu bali hata kwa watanzania wazawa sasa iweje leo tunashabikia wachina kufanyakazi ambazo hata watanzania tunawakaza.
Idara yetu ya uhamiaji inatakiwa kuimarishwa ili kukabiliana na wimbi la wageni wa aina zote kufanyakazi ambazo watanzania wangeweza kuzifanya au kazi zisizohitaji mtaji mkubwa kuzianzisha.EAC inakuja muda si mrefu kama uhamiaji itashindwa kuwadhibiti wageni kuto nchi za mbali kama China sijui itakuwaje kwa wageni wanchitulizopakana nazo.

I must say- sipendi attitude ya baadhi ya watu kama wewe ambao wanaamini sisi watanzania tunadeserve kazi ndogondogo kama za upiga debe na umachinga, tena ndani ya nchi yetu wenyewe! Why dont we all be optimistic and positive na tuseme kwa sauti kubwa kwamba kazi za kitaalam zinazohitaji ujuzi na mitaji ndio ziwe za watanzania na kazi ndogondogo na chafu ndio tuwaachie wageni? Hata sisi tulioko ughaibuni tunajua kwamba 9/10 kuna uwezekano kuwa ukiomba kazi 'chafu' utaipata na zile za kitaalamu ni za wazawa!

Pia, kama walivyosema wengi hapa- tatizo letu ni 'attitude'. Mbongo akishajipinda akanunua kabasi basi yeye anaamkia bar kwenye supu na kupiga mbili tatu huku akisubiri hesabu, ataajiri wapiga debe, makonda, madereva- kwa kuwa tu anajiona ameshaukata na hizo kazi sio za type yake. Wakati wenzetu utakuta wanaendesha, wanasanya wenyewe, na hata likiharibika wanatinga overoli na kuzama chini wenyewe, achilia mbali kupiga debe!
 
Haya si maendeleo tunayoyahitaji Tanzania. Hatutaweza kuendelea kwa kuleta wawekezaji hadi wapiga debe! Nilitarajia mwekezaji km huyo atoe ajira kwa wazawa, mfano madereva, makondakta nk. sasa km anakuja na wapiga debe wake hao wazawa watatoa wapi ajira?
 
1) Kms 140/hr against 80kms/hr for buses in TZ

2) Kushushwa kny mizani, why? basi linatakiwa litengenezwa kwa uwiano mzuri wa uzito hata kama engine itakuwa nyuma!

So hawa nao wanavunja sheria za barabarani!

Hakuna basi lisilovunja sheria kwenye kipengele cha speed labda cha kushusha watu na inategemea basi ni la route gani. Sitegemei basi kutoka Morogoro likawa na mizigo mingi kama basi kutoka Mbeya ambalo watu wanajaza viroba vya mchele na maharage.
 
Haya si maendeleo tunayoyahitaji Tanzania. Hatutaweza kuendelea kwa kuleta wawekezaji hadi wapiga debe! Nilitarajia mwekezaji km huyo atoe ajira kwa wazawa, mfano madereva, makondakta nk. sasa km anakuja na wapiga debe wake hao wazawa watatoa wapi ajira?

Aliye kwambia hao wapigadebe ni special from China nani? Kwani mmiliki wa basi hawezi kupiga debe? sasa kwa taarifa yako, wale wa china, yale ni basi yao (ndo wamiliki) so huduma zote wanatoa, kuanzia kutafuta abiria (kupiga debe), kukata tiketi etc. Acha kukariri kwamba mpiga debe ni mbangaizaji tu ndugu yangu! Ref. Post ya Kana -ka - Nsungu for more
 
Hakuna basi lisilovunja sheria kwenye kipengele cha speed labda cha kushusha watu na inategemea basi ni la route gani. Sitegemei basi kutoka Morogoro likawa na mizigo mingi kama basi kutoka Mbeya ambalo watu wanajaza viroba vya mchele na maharage.

Ndo maana nimesema ''hao nao wanavunja sheria'' kwa maana kwamba wapo wazalendo wavunjaji sheria, so I thought initially kwamba hawa ni exceptional!
 
Mbona wadosi tuko nao kitambo, tena afadhali ya wachina wanajiachia wadosi wanajifungia na pesa au mchongo ukingia katika anga zao hakuna mbongo atakae tia mkono. Mie naona watu kutoka nje ndio watakaofanya Bongo iendelee fasta kuliko huu uswahili ambao watu wameung'ang'ania kitambo.

Kama wapiga debe wa kibongo wengi mateja na ndio vibaka, wenye mabasi hawajali namna abiria wao wanavyoteseka kwa kuibiwa na usumbufu miaka nenda miaka rudi kali kuliko yote hao wanaoitwa wazalendo ndio wanaongoza kuchinja abiria wao, sasa kama mchina kaingia front kuonyesha namna nyingine ya kufanya biashara ya mabasi ya mkoa mie nawapa saluti.

Wabongo wengi wanangojea fursa za kupewa na wanasiasa na ndio maana kila mtu anapiga siasa, na waliokuwa bush wanataka kuingia Dar. Nani kakwambia Bongo ndio kwenu na usitoke! mnashindwa hata kuchomokea Burundi, Rwanda au Congo kuna fursa kibao huko.
 
...lakini inapofika mahali 'muwekezaji' huyu anayekuja kwa njia ya globalization anafanya yale yale ya wafanyabiashara wetu wa kibongo e.g mtu umestarehe kwenye reclining seat yako halafu unaambiwa nyanyuka uje mbele ili tupite mizani kwanza kwa maana nyingie kuibia serikali, do we really need this kind of wawekezaji?
 
Kama mlidhani Globalization lelemama basi mlikosea, Cha msingi ni kutafuta namna ya kusurvive na kujiletea maendeleo popote duniani. Mipaka ya kisiasa huko mbeleni itabaki kwenye ramani tu ila wanadamu watajichanganya tu. kwa sababu alichokifanya mchina huyo mpiga debe kinaweza kufanywa na Mzambia, Mganda, Mrundi na tusione ajabu sana lakini kwa sababu Mchina anaonekana na rangi kidogo tofauti na sisi basi tunaona ajabu kweli kweli.

Kiufupi ni kwamba Mchina kupiga debe ni kwa sababu amekuta Watanzania wanapiga debe na biashara zao zinatoka, angekuta Watanzania wanafanya booking online naye bila shaka angeanzia hapo kwa huduma zake. sasa iweje Mtanzania kupiga debe iwe sawa lakini mchina kupiga debe si sawa wakati wote wanagombania wateja walewale?.


Maneno mazito sana haya mkuu!

Kama huyo mchina angeenda US au UK..sidhani kama angepiga debe! Angeanza kufanya mambo online! Salute mkuu!

Harafu kama wengine walivyosema, globalization siyo lelemama! NA HATA KAMA WANAFOJI VIBALI NA KUINGIA KIHOLELA Nchini mwetu, MTU WA KULAUMIWA YUPO NA SIYO HAO WACHINA!

watanzania wenzangu, we are in for a very long duel. Inabidi tuzoee hii hali. Globalization imefikia point of no return.
 
Maneno mazito sana haya mkuu!

Kama huyo mchina angeenda US au UK..sidhani kama angepiga debe! Angeanza kufanya mambo online! Salute mkuu!

Harafu kama wengine walivyosema, globalization siyo lelemama! NA HATA KAMA WANAFOJI VIBALI NA KUINGIA KIHOLELA Nchini mwetu, MTU WA KULAUMIWA YUPO NA SIYO HAO WACHINA!

watanzania wenzangu, we are in for a very long duel. Inabidi tuzoee hii hali. Globalization imefikia point of no return.

Kadri ya mazingira ya kufanya biashara yatakavyoimarika, wageni wengi ndiyo watakavyozidi kuingia Tanzania, na hakuna serikali wala nani wakuweza kuzuia jambo hili. Angalia, leo hii ni watu wa mataifa mangapi wanapigana vikumbo huko China, kwa taarifa Ulimwengu mzima umeelekea China na wachina sasa wanapata fursa ya kutoka kwenda kuwekeza zaid nje ya china. Kwa kadri uchumi wa China unavyokuwa basi na investments zao nje ya china zitaendelea kukuwa. Tutarajie kuwaona wachina wengi tu wakiingia bongo na sehemu zingine mbalimbali duniani.
 
Naungana na wachangiaji mbalimbali ambao wamekuwa wazi kuwakubali hao mabwana kufanya kazi ya 'kupiga debe'. Hoja yangu hasa ni kipengele cha usawa katika utandawazi. Ikiwa wewe ukienda nchi za wengine unapewa kazi kwa nini mchina au raia wa nchi nyingine akija Tanzania asipewe? Na tumeelezwa kuwa hao mabwana ni wawekezaji hivyo wana haki ya kuwa 'marketing strategy' yoyote ilimradi hawavunji sheria za nchi. Kwa wale waliowahi kuishi ama wanaishi nchi za ughaibuni wataielewa vizuri hoja hii. Na kwa wale ambao wapo Tanzania siku zote wajue dunia yetu imekuwa kama mtaa mmoja - tunakufa na kuzikana, na tunaombana chumvi.
 

Kwa kuongezea...na ATCL wanachukua Wachina...hebu ngoja nianze kujifunza kichina mie!!!!

wachina noma bwana.
tuna mengi ya kujifunza kutoka kwao.
mojawapo ni uchapaj kaz. kuna jamaa aliniambia yeye alipokuwa USA ilikuwa kama wao (mablack) ni kama washindan wa wachina kufanya kaz kama za kubeba boksi. lakin akaniambia wachina walikuwa wanawashinda weus. wanafanya kaz zaid na haraka na hata kwa hela ndogo kaz inafanywa.

na serikali ya marekan yenyewe imekopa dola kibao kutoka china. china wanakuja na wako juu.

na kuna ka nchi huko karibu na bonden nasikia wachina wako mpaka vijijin wanalima na kuuza mboga. masupermarket mengi ni ya kwao. wenyeji wamebak wateja na wanalialia na kushangaa kwamba sijui itakuwaje siku za mbele. business nyingi zimeshikwa au zinaelekea kushikwa na wagen (wachina).

kuna uwekezaj mwingine unafaa kufanywa na wageni, kama vile kufungua viwanda na nk. ambavyo vitalipa kodi na kuajiri watz.
lakin angalia, inavyoelekea wachina wengine wanaweza kuja na kuanzisha biashara ya teks. kwa kuwa anamtaj biashara itakuwa kubwa na teks za wabongo zitakosa soko na hivyo zitapaki. kipato cha mbongo kitapungua.

baada ya muda wachina wengine wanaweza kuja na biashara ingine na kutokana na uwezo mzur katka business wanaweza kufanya wabongo biashara zao zisimame.

yap. tutafanyaje katka hali kama hiyo?
cha kwanza lazima tuwababe. kama wanaanzisha kampun wasiite wachina wenzao kuja kufanya kaz kama za udereva, utingo. kaz ambazo wapo watz wanaoweza kuzifanya.

lakin rushwa imejaa, tunahandle vip wagen wanaokuja kuomba uraia? USA wanafanyaje? kenya wanafanyaje? uchina wanafanyaje? ni vigumu au ni rahis kias gani kupata uraia wa tz?
na mgeni ni ruksa kufanya biashara yeyote? na ya mtaj wowote?

tuna sheria na taratibu zetu. ni muhimu kuziheshimu. na sheria ni muhimu zikienda na wakat. lakin pia sheria na taratibu tulizonazo huenda hazifai
 
He he he..

Hawa wadanganyika wanaowa-support hawa wachina na kuwapigia chapuo sidhani kama wana tofauti saana na akina Sultan Mangungu of Msovero..!

Ukweli ni kwamba;

1. ELIMU NA UWEZESHWAJI WA KIFIKRA
Hii mada ilivyo mkao wake ni kama ule wa thread kuhusu serikali kufacilitate upatikanaji wa elimu ya juu kwa wananchi wake. Serikali ambayo haipo critical kuhakikisha wananchi wake wanakuwa-fit 'upstairs' ni kwamba systematically inakaribisha 'wachina' zaidi kuja kuchukua kazi zetu na kutuacha masikini zaidi na zaidi. Ukweli ni kuwa waTz wengi kama si wote, hatuna ilmu na skills za kibiashara. Ktk kuhakikisha watu wanaamka ni dhima ya serikali kuangalia fursa na methodology ipi itumike na wapi mzizi wa tatizo uanze kukatwa. Nadhani ndio kazi ya wanataaluma ktk Wizara ya Biashara na Uchumi na sio kujibu maswali ya bunge!.

2. UWEZESHWAJI WA NGUVU ZA KIBIASHARA
Ni dhahiri kuwa kwa hali ya sasa, mTz wa kawaida kumilliki biashara ya maana ambayo inaweza kuelezewa kuwa its fairly sustainable, seuze kiasi cha kuvuka mipaka (Transboundary business) ni ndoto. Hii inatokana na kukosekana na mfumo mzuri wa uratibu biashara pamoja na bureaucratic system, ikiwemo ya kuwawezesha mitaji bila masharti ambayo ni suicidal. Mitaji mingi imekaa kuwanufaisha watu ambao wanaotoa hiyo mitaji, hususan mabenki.


3. LONGOLONGO NA POLITIKI
Kuna watu wapo very theoretical na kudhani kuwa mambo yatabadilika waTZ 'tukiamka' na 'kuacha uvivu', and all over sudden tutakuwa taifa tajiri, HELL NO!. Hawasemi ‘kuamka’ na ‘kuacha uvivu’ huo ni kupi? Wala methodology ya ‘kuacha’ huo ‘uvivu’ na jinsi ya ‘kuamka’.

Najua kuna vijana wengi huwa tunakamatwa eti kwa kosa la 'uzembe' & 'uzururaji'. Lakini huwa najiuliza, serikali huwa inapata wapi nguvu ya kumshtaki mtu kwa kosa la UZEMBE huku hujampa KAZI? Kazi unawapa 'wachina' halafu kosa la uzembe unanipa mimi uliyeninyima fursa ya ajira au kujiajiri. Hii ni haq?

4. ROLE YA SERIKALI
Mwingine anasema tusibweteke na kuisubiri serikali. Hii ni kauli potofu. Sisi wananchi ndio waajiri wa hiyo entity inayojiita ‘serikali’. Na tumeiweka madarakani ifanye kazi ambazo sisi waTz mmoja-mmoja tusingeweza kuifanya. Hivyo basi, kama serikali inashindwa ku-live up to the expectation, sidhani kama kuna ulazima wa hii serikali kuendelea kuishi kwa migongo yetu wakati haitusaidii chochote. Nilitegemea ktk mazingira ya kisasa ya utandawazi, kuwe basi at least information ktk state websites kuhusu upatikanaji wa mitaji, taarifa za masoko ya ndani na nje, wapi uende unapohitaji hiki au kile kuhusu biashara yako.n.k. Pia ningelitegemea kiasi fulani ktk bajeti kiwe kinatengwa kila mwaka kwenda moja kwa moja kwenye field na vikundi vya mfano vya wajasiriamali ktk mikoa yote na sio kutoa ‘asante kwa kumuwezesha kuingia Ikulu’ mtu, kwa staili ya ‘mabilioni ya JK’.

5. TAKWIMU
Ktk nchi ambazo serikali zao zinawajibika ipasavyo, ukusanyaji wa takwimu unapewa kipaumbele. Taarifa kuhusu nguvukazi, hali ya ukosefu wa ajira, fursa zilizopo kwa sasa, upungufu uliopo n.k. Ktk hali kama hii ndio unaweza ku-justify hii hadith ya ‘mchina’ kupiga debe au la. Nchi za wenzetu takwimu kama hizi zipo readily available, na wakati mwingine ambapo kunakuwa na deficit ya nguvukazi wa taaluma Fulani, serikali haikai tu ikishangaa, bali hujaribu hata kuchochea wataalamu kutoka nchi nyingine kuja kuziba pengo kwa kurahisisha masharti ya visa n.k. Kwa hiyo mtu anayesema serikali isilaumiwe haelewi kuwa kinachoelea kimeundwa hikidondoki kama mana jangwani.

6. KULINDA WAZAWA
Ktk nchi ambazo serikali zao zinawajibika ipasavyo kwa wananchi wake, hufanya affirmative actions kadhaa kuhakikisha wananchi wanamiliki uchumi wao. Hizi mbinu zinatofautiana na zina range kuanzia kuwapa tax grace period wawekezaji wazawa, kuwapa heavy tax wawekezaji wa kigeni n.k.

Ukiona serikali inayojua kabisa kuwa wananchi wake ni masikini halafu inawa-expose wawekezaji wazawa kwenye very competitive challenges na wale wa nje, ujue tu kuwa serikali hiyo haipo kwa maslahi ya taifa.


Was’alam
 
Leo asubuhi nilikuwa nasindikiza wageni kuelekea bara (mkoani). Nikiwa ndani ya stendi ya mabasi ya Ubungo kiasi cha saa 11:15 (kumi na moja na robo alfajiri) nilikumbana na mpiga debe wa kichina akiniaambia 'lipo basi la Obama hapa linakwenda Mbeya hadi Tunduma" (lafudhi ya kihuuhii). Sikuamini ilibidi nisimame nihakikishe anayoyasema. Baada ya kudadisi nikaambia hao wachina (walikuwa watatu) unaowaona wanamiliki hilo basi (pembeni yetu) lenye rangi za bendera ya USA linalofanya safari zake Dar-Tunduma.

Jamani, hivi kweli mchina ananunua basi na anaajiri mpiga debe mchina, mkata tiketi mchina, vibari vya kufanya uhuni huu wanapata wapi?

Kweli mtanzania unaweza kwenda nchi za watu ukafanya hivi?

Kama basi lilikuwa la Mbeya hadi Tunduma, inawezekana kuwa hawa si raia wa China. Ni Watanzania wenzetu wenye damu za Kichina ambao ni matunda ya ujenzi wa TAZARA. Nasikia kipande hiyo wapo wengi tu. Jamaa alinihadithia kuwa kuna kijiji mpakani mwa Zambia kwenye miaka ya 70 - 80 kilikuwa kama Hong Kong. Kilikuwa na vijana na wasichana wengi wenye sura za Kichina.
 
Back
Top Bottom