Moses Phiri hajagusa mpira kwa dakika 16

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,154
7,926
Juzi hapa nilifanya marudio ya mechi ya Simba vs ASEC Mimosas ili nijiridhishe baadhi ya vitu.

Moja ya jambo nililogundua na kunishangaza katika marudio ni kugundua kuwa Moses Phiri aliingia dakika ya 59 ya mchezo na alikuja kugusa mpira wake wa kwanza dakika ya 76. Imenikumbusha mechi ya kwanza dhidi ya Power Dynamos kule Zambia ambapo Moses Phiri hakuonekana kuwa na impact kwa timu kwa sababu hakuwa anachezeshwa kabisa na ikawapa maneno wale ambao kwa sababu zao hawamkubali huyu mwamba wakasema mbona amepangwa ila hakufanya lolote.

Pia sielewi kwa nini Chama hachezeshwi pamoja na Phiri. Simba imekuwa na shida ya kujua jinsi sahihi ya kuwatumia wachezaji wake. Sakho alikuwa na impact zaidi uwanjani akiingia kama sub badala ya kuanza ila hilo walishindwa kugundua pamoja na kwamba uwanjani tofauti zilionekana akianza na akiingia lakini bado wakawa wanang'ang'ania kumuanzisha. Naona Saidoo ni mchezaji wa namna hiyo pia.

Weka pale mbele Phiri, Chama na Miquissone wacheze pamoja. Hawa watatu wana maelewano ya karibu ndani na nje ya uwanja na wanapenda kucheza pamoja na kuona mwenzake anafanya vitu vikubwa uwanjani. Ni sawa na beki ya Yanga ya kina Job/Mwamnyeto/Kibabage/Shomari. Utumie huo utatu badala ya kufanya bahati nasibu katika upangaji wa kikosi. Kuhusu Baleke wengine tulisema toka mwanzo ni mchezaji mwenye uwezo wa kumalizia ila siyo mshambuliaji mwenye uwezo wa kukokota mipira kama Mayele. Mfumo wa sasa hivi wa kumtaka arudi kati kutafuta mipira haumfai.

Kama kinyago tumekitengeneza wenyewe hatuna budi kukifuta vumbi kivutie.
 
Mkuu hiyo inatokea sana,nilishangaa haya mechi ya Belouizdad vs Yanga, Aziz K alipotezwa mechi nzima hakuonekana , ni meno tu tulikuwa tunaona

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Max kuna wakati nilikuja kushangaa bado yuko uwanjani nilidhani alishatoka maana alipotea mazima ila sidhani kama ni kwa sababu hawakuchezeshwa ila impact yao ilikuwa ndogo kulinganisha na ambavyo tumewazoea.
 
Back
Top Bottom