Morogoro: Viongozi wa CHADEMA wakamatwa na polisi, vurugu zaibuka!

Hii serikali dhaifu imepoteza heshima na uhalali wa kuongoza nchi hii. Muda ni kutumia nguvu na vitisho, navyo sasa vimefika ukingoni. So Mr. Kikwete what is left with you then?
 
Kuna gari 4 za FFU likiwemo la Maji ya kuwasha nimepishana nayo hapa Airport, yanaelekea upande wa Tazara. Inaweza ikawa na uhusiano na vurugu hizi? Kwamba yanaelekea Moro kuongeza nguvu? Au kuna tifu jingine somewhere?
 
Habari za uhakika ni kua polisi wameua mtu maeneo ya Msamvu bila sababu ya msingi,kisa ni kua walikua tu wanajaribu kuzuia maandamano ya Cdm na kijana huyo aliyekua akiuza magazeti aliwaonyesha alama ya V ndipo walipomlipua! My take: ni wazi jeshi la police chini ya IGP Mwema limeshindwa kuwalinda raia na mali zake,na kuwachukulia hatua wezi wakubwa na wahujumu nchini,bali jeshi la polisi limegeuka kua la mauaji kwa raia wasio na hatia kwa jinsi watakavyo! Source: mimi mwenyewe nipo kwenye mkutano hapa Morogoro
 
haki haizuwiwi kwa mtutu na mabomu ya machozi au ya moto,watu wa moro msirudi nyuma songeni mbele kulikomboa taifa
 
ITV imetangaza habari mpasuko hivi punde kuwa mtu mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi ya kisogoni na Polisi wa Morogoro kwenye maandamano .Je wama JF mlioko huko hembu tupasheni ukweli uko vipi huko Mji kasoro bahari hivi sasa.
 
Orio Lilio;4509699]haki haizuwiwi kwa mtutu na mabomu ya machozi au ya moto,watu wa moro msirudi nyuma songeni mbele kulikomboa taifa
 
Jeshi la polisi mkoani Morogoro latumia mabomu ya machozi kukabiliana na wafuasi wa chama cha CHADEMA, wanaoshinikiza kuandamana kuelekea kwenye mkutano wao unaofanyika Uwanja wa Ndege.

Source:
www.ippmedia.com
 
...[/QUOTE]

Viongozi wa CDM waendelee kuweka data base nzuri ya haya matukio ili muda muafaka utakapofika lazima wasimame mbele ya mahakama ya kimataifa kujibu tuhuma hizi, matukio na picha msisahau kila mauaji yanapotokea nasiku ya mazishi tuwe na ushahidi wa kutosha.

Tukio la lao lina mhusu Shilogile IGP mwama na WENZAKE.Hata Kenya hawakutegemea kama wengefika kwa OCAMPO
.
 
......inasikitisha na inatia machungu sana; huu unyama kwa watu wasiokuwa na hatia kwakweli umekithiri.
 
Wanatekeleza maelekezo ya mwigulu nchemba kweli hatuna polisi !!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kweli hatari hii yani mpaka watu wapigwe mabomu ya machozi ndo wanaelewa kwa kitu kidogo tu kuto kitii sheria bila shuruti hivi kwani bila hayo maandamano mkutano usinge fanyika? Tuwe makini vijana wa kitanzania tusitumiwe na wanasiasi..
 



Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema

Askari waliokuwa katika eneo la tukio kabla ya kuanza kwa maandamano hayo

Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya chadema leo mjini morogoro




Gari la chadema lililokuwa likiongoza maandamano hayo

Mmoja wa kiongozi wa chadema akiwa amekamatwa akiwa ndani ya gari la polisi

Wafuasi wa chadema wakiwa na maandamao hayo mjini morogoro


 
Back
Top Bottom