Rukwa na Morogoro polisi wamelala

jupiter001

Member
May 25, 2023
44
72
Report ya utapeli mitandaoni iliyotolewa na TCRA inaonyesha Rukwa na Morogoro wana matapeli wengi sana wa mitandaoni.

Inakuaje mkoa ambao una watu wachache kuliko DSM unakua na matapeli wengi namna hio, na sio mara ya kwanza kumekua na report hata za nyuma zinaonyesha matapeli ni wengi sana morogoro na Rukwa.

Polisi wa vitengo vya cyber wa maeneo hayo wanafanya kazi gani? Wanasubiri kuzuia maandamano tu?

Kamati za ulinzi na usalama za maeneo hayo zinafanya kazi gani? Au haya maeneo yanaongozwa na wale tulioambiwa ni wakimbizi waliopata nafasi serikalini na teuzi?

Mama zetu na watanzania wa hali za chini wanaumizwa na matapeli polisi wapo tu ,wanasubiri kuzuia maandamano shame on you polisi wa mitandaoni.

Kila siku nyie kazi yenu kuhangaika na wanasiasa wa upinzani tu, mambo ya msingi hamfanyi!


report
 

Attachments

  • TCRA Communications Statistics for Q2 2023 - 2024_1705933797.pdf
    26.6 MB · Views: 1
Back
Top Bottom