MOROGORO : Mchungaji aliyegombea ubunge Chadema ahamia CCM

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli katika kusimamia kikamilifu uwajibikaji, kupambana na ufisadi na vitendo vya rushwa, umezidi kurejesha imani kwa baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani wakiwemo wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilayani Mvomero, Morogoro

Hatua hiyo imewafanya wanachama sita wa Chadema wilayani Mvomero akiwemo aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Mvomero, Mchungaji Oswald Mlay juzi kutangaza kukihama chama cha Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Mlay alisema alishindwa kuitumikia Chadema kutokana na kukosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa chama hicho,
Mbali na hilo, pia uwepo wa matabaka ndani ya chama na viongozi kushindwa kufuata Katiba, ni moja ya sababu iliyomlazimu kuondoka na kujiunga na CCM

Pia alisema jambo la msingi zaidi yeye na wenzake watano kuamua kukihama chama hicho ni kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli

Wanachama hao wa zamani wa Chadema walikabidhiwa kadi za uanachama wa CCM na Kaimu Katibu wa CCM Mkoa, Kulwa Milonge

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kujiunga na CCM, Paulo Michael na Patrick Amri, walidai kuwa ndani ya Chadema kumekuwepo kwa matabaka ikiwa na viongozi wa Chama hicho kushindwa kufuata Katiba, hivyo kulazimika kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM

Wengine waliohama ni Romanus Mtiga, Mussa Abdallah na Michael Hepa

Chanzo : HabariLeo
 
Mchungaji alikuwa CCM, MWEZI WA PILI 2015 AKAHAMIA CHADEMA LENGO LAKE LILIKUWA NI KUUTAFUTA UBUNGE BAADA YA KUIKOSA FURSA HIYO CCM KWAMAANA ALIAMINI ASINGEWEZA KUMUANGUSHA MAKALA WALA MURADI MBUNGE WA SASA, ALIPOUKOSA UBUNGE KWA KUSHINDWA NA MURADI AKAPEWA DILI NA MKULU KUUVURUGA UKUTA KUPITIA MIJADALA YAKE YA KIDINI. MKULU HAKUJUA KAMA JAMAA ALIKUWA CDM,HIVYO IMEMLAZIMU MBAULA KURUDI TENA CCM.
 
Anasema njaa imemkimbiza upinzani, kumbe tatizo lake yeye ni njaa sio kuwatetea watanzania.
 
Mimi naishi mvomero na nilikuwepo kwenye mkutano wake wa kurudi ccm,aliufanyia kijiji cha kidudwe kata ya mtibwa. Yule ni YUDA ESCARIOTE, hana Msimamo. Alikuwa CCM akakimbia akaja chadema amekimbia amerudi nyumbani kwa baba
 
Romanus Mtiga na Musa Abdallah ni watoto wa mkiti wa CCM wa Wilaya hiyo ya mvomero Mh Abdullah Mtiga
 
Mimi naishi mvomero na nilikuwepo kwenye mkutano wake wa kurudi ccm,aliufanyia kijiji cha kidudwe kata ya mtibwa. Yule ni YUDA ESCARIOTE, hana Msimamo. Alikuwa CCM akakimbia akaja chadema amekimbia amerudi nyumbani kwa baba
Inamaana akitokea Kiongozi mwingine akimridhisha tu atahama chama.. hoja dhaifu sana
 
MCHUNGAJI mpenda fedha huyo.
Kutokana na tamaa yake namtumia ujumbe huu :
Waebrania 10:38(Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa Imani ,naye akisitasita roho yangu haina furaha naye.)
 
Back
Top Bottom