Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli katika kusimamia kikamilifu uwajibikaji, kupambana na ufisadi na vitendo vya rushwa, umezidi kurejesha imani kwa baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani wakiwemo wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilayani Mvomero, Morogoro
Hatua hiyo imewafanya wanachama sita wa Chadema wilayani Mvomero akiwemo aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Mvomero, Mchungaji Oswald Mlay juzi kutangaza kukihama chama cha Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mlay alisema alishindwa kuitumikia Chadema kutokana na kukosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa chama hicho,
Mbali na hilo, pia uwepo wa matabaka ndani ya chama na viongozi kushindwa kufuata Katiba, ni moja ya sababu iliyomlazimu kuondoka na kujiunga na CCM
Pia alisema jambo la msingi zaidi yeye na wenzake watano kuamua kukihama chama hicho ni kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli
Wanachama hao wa zamani wa Chadema walikabidhiwa kadi za uanachama wa CCM na Kaimu Katibu wa CCM Mkoa, Kulwa Milonge
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kujiunga na CCM, Paulo Michael na Patrick Amri, walidai kuwa ndani ya Chadema kumekuwepo kwa matabaka ikiwa na viongozi wa Chama hicho kushindwa kufuata Katiba, hivyo kulazimika kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM
Wengine waliohama ni Romanus Mtiga, Mussa Abdallah na Michael Hepa
Chanzo : HabariLeo