DOKEZO Morogoro: Mahashrey na wafanyabiashara wa ufuta wanavyoshirikiana na wafanyakazi wasio waaminifu kuhujumu mfumo wa stakabadhi ghalani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

nokwenumuya

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
810
2,851
Mkoa wa Morogoro ni mmoja wa Mkoa wenye uzalishaji mkubwa wa mazao yakiwemo mazao ya ufuta.

Ni takribani miaka mitatu sasa Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango, na Wizara ya Viwanda na Biashara zimekuwa zikitoa maagizo kuwa Ufuta wa Morogoro uuzwe kupitia Stakabadhi za Ghala Ili Mkulima aweze kupata bei yenye tija na aweze kujikwamua kiuchumi.

Lakini kila mwaka kumekuwa na vijisababu kuwa bado Elimu haijawafikia wakulima kuhusu zoezi Hilo.

Mwaka jana wakati wakulima tayari wakiwa wamepeleka ufuta ghalani, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Bwana Shigela aliamua kutoa amri kuwa kasimamisha mfumo huo hadi mwaka 2023. Inasemekana alifika bei kwa wahindi.

Mwaka huu pia katika baadhi ya Wilaya za Morogoro kama Malinyi na Morogoro DC tayari wameanza mfumo, Cha ajabu ni pale baadhi ya Viongozi haswa wanasiasa na baadhi ya Watendaji kuingilia zoezi na ni kwa rushwa za wanunuzi ambao hufaidika na mfumo holela huku wakulima wakiendelea kuumia.

JINSI WAFANYABISHARA WAWAIBIAVYO WAKULIMA.

Mfanyabiashara anayenufaika sana na kilimo Cha ufuta wa Morogoro ni MAHASHREY, mfanyabiashara huyu hapendi mfumo wa stakabadhi kuogopa ushindani wa WAFANYABISHARA wengine wanaoweza kutoa bei kubwa zaidi yake.

Na mara nyingi akienda kununua huenda na mizani iliyochezewa. Katika kila kilo 100 anazopima ameseti mzani wake kuiba kilo 15.
Hivyo hata akionyesha ananunua kwa bei kubwa huwa kamuibia mkulima.

Pia huwa wanadanganya katika mageti ya ushuru na hivyo kutolipa ushuru halali wa Serikali.

KWANINI WAKULIMA WA MOROGORO WAENDELEE KUHUJUMIWA?

Tunamuomba Mh. Waziri Mkuu aingilie kati Ili Ufuta wa Morogoro umfaidishe mkulima wa Morogoro kama ilivyo kwao Lindi, Mtwara, Pwani, Ruvuma, Songwe. N.k.

Naomba kuwasilisha.
 
Tunamshukuru Mh. Kigoma Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesimama kidete kuhakikisha mfumo unasimama Imara.

Wanaoyumba na kuruhusu Ufuta utoke kiholela katika Wilaya zao ni Wakuu wa Wilaya ambazo mfumo huu unatekelezwa.
 
Mkoa wa Morogoro ni mmoja wa Mkoa wenye uzalishaji mkubwa wa mazao yakiwemo mazao ya ufuta.

Ni takribani miaka mitatu sasa Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango, na Wizara ya Viwanda na Biashara zimekuwa zikitoa maagizo kuwa Ufuta wa Morogoro uuzwe kupitia Stakabadhi za Ghala Ili Mkulima aweze kupata bei yenye tija na aweze kujikwamua kiuchumi.

Lakini kila mwaka kumekuwa na vijisababu kuwa bado Elimu haijawafikia wakulima kuhusu zoezi Hilo.

Mwaka jana wakati wakulima tayari wakiwa wamepeleka ufuta ghalani, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Bwana Shigela aliamua kutoa amri kuwa kasimamisha mfumo huo hadi mwaka 2023. Inasemekana alifika bei kwa wahindi.

Mwaka huu pia katika baadhi ya Wilaya za Morogoro kama Malinyi na Morogoro DC tayari wameanza mfumo, Cha ajabu ni pale baadhi ya Viongozi haswa wanasiasa na baadhi ya Watendaji kuingilia zoezi na ni kwa rushwa za wanunuzi ambao hufaidika na mfumo holela huku wakulima wakiendelea kuumia.

JINSI WAFANYABISHARA WAWAIBIAVYO WAKULIMA.

Mfanyabiashara anayenufaika sana na kilimo Cha ufuta wa Morogoro ni MAHASHREY, mfanyabiashara huyu hapendi mfumo wa stakabadhi kuogopa ushindani wa WAFANYABISHARA wengine wanaoweza kutoa bei kubwa zaidi yake.

Na mara nyingi akienda kununua huenda na mizani iliyochezewa. Katika kila kilo 100 anazopima ameseti mzani wake kuiba kilo 15.
Hivyo hata akionyesha ananunua kwa bei kubwa huwa kamuibia mkulima.

Pia huwa wanadanganya katika mageti ya ushuru na hivyo kutolipa ushuru halali wa Serikali.

KWANINI WAKULIMA WA MOROGORO WAENDELEE KUHUJUMIWA?

Tunamuomba Mh. Waziri Mkuu aingilie kati Ili Ufuta wa Morogoro umfaidishe mkulima wa Morogoro kama ilivyo kwao Lindi, Mtwara, Pwani, Ruvuma, Songwe. N.k.

Naomba kuwasilisha.
Asante kwa jinsi mlivyoliweka
 
Back
Top Bottom