Monaban asomeshwa namba, anyang'anywa kiwanda cha unga

Jamani ukweli ni kwamba monaban hakuwa mmiliki alikuwa muendeshaji kwa niaba ya serikali through consolidated holding cooperation ambayo haipo for now, so kwa sasa nmc itasimamiwa na bodi ya nafaka na uendeshaji wake unaendelea kuwa chini ya monaban mpaka 2022 mkataba wake utakapofika mwisho but anaweza akaongezewa na Bodi ya nafaka mkataba mwingine.
 
jamaa yaonesha bwana mvii humuelewi kabisa mpaka una Xray maalumu.
Sijui kama umenielewa ndugu yangu ,Monaban hata angeshinda ubunge Arusha mjini kupitia CCM na Lowasa kuwa Ukawa ,Monaban angekua loyal kwa Lowasa na sio Ccm ,
 
Hakika CCM haina rafiki , huyu jamaa pamoja na kutumika kujaribu kuokoa CCM Arusha lakini ameporwa kiwanda baada ya serikali chini ya Mafuru kuingiza bodi yao.

========

Serikali imetengua umiliki wa Kinu cha kusagisha nafaka cha (NMC) kilichoko mkoani Arusha.

Serikali imetengua umiliki wa Kinu cha kusagisha nafaka cha (NMC) kilichoko mkoani Arusha kutoka kwa mwekezaji wa kampuni ya Monaban Trading na kukiweka chini ya uangalizi wa bodi ya mazao mchanganyiko.

Akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya Kinu hicho msajili wa hazina Taifa Bw. Laurance Mafuru amesema lengo la hatua hiyo ni kukiwezesha Kinu hicho kutumika kwa tija na kwa masilahi mapana zaidi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla, na kwamba mwekezaji ataendelea na shughuli zake kama kawaida chini ya bodi ya mazao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya mazao mchanganyiko Bw. John Maige amesema pia shughuli zote za uendeshaji zitaratibiwa na bodi hiyo na kwamba watanzania wategemee kunufaika zaidi tofauti na hapo awali.

Nae mwekezaji aliyewekeza kwenye kiwanda hicho Bw. Philimon Millel amesema ataendelea kushirikiana na bodi hiyo kwani maamuzi yaliyofikiwa
yanalenga kuongeza tija na ameendelea kuikumbusha serikali ombi lake la kupewa umiliki wa kudumu wa kinu hicho kama ilivyofanya kwa wawekezajiwengine.

Chanzo: ITV

Ubunge ukose na kiwanda unayang'anywe! Wacha tu isome nambaaa heeeeeee
 
Jamani ukweli ni kwamba monaban hakuwa mmiliki alikuwa muendeshaji kwa niaba ya serikali through consolidated holding cooperation ambayo haipo for now, so kwa sasa nmc itasimamiwa na bodi ya nafaka na uendeshaji wake unaendelea kuwa chini ya monaban mpaka 2022 mkataba wake utakapofika mwisho but anaweza akaongezewa na Bodi ya nafaka mkataba mwingine.
Mpaka 2022.
 
Back
Top Bottom