Monaban asomeshwa namba, anyang'anywa kiwanda cha unga

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,476
215,295
Hakika CCM haina rafiki , huyu jamaa pamoja na kutumika kujaribu kuokoa CCM Arusha lakini ameporwa kiwanda baada ya serikali chini ya Mafuru kuingiza bodi yao.

========

Serikali imetengua umiliki wa Kinu cha kusagisha nafaka cha (NMC) kilichoko mkoani Arusha.

Serikali imetengua umiliki wa Kinu cha kusagisha nafaka cha (NMC) kilichoko mkoani Arusha kutoka kwa mwekezaji wa kampuni ya Monaban Trading na kukiweka chini ya uangalizi wa bodi ya mazao mchanganyiko.

Akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya Kinu hicho msajili wa hazina Taifa Bw. Laurance Mafuru amesema lengo la hatua hiyo ni kukiwezesha Kinu hicho kutumika kwa tija na kwa masilahi mapana zaidi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla, na kwamba mwekezaji ataendelea na shughuli zake kama kawaida chini ya bodi ya mazao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya mazao mchanganyiko Bw. John Maige amesema pia shughuli zote za uendeshaji zitaratibiwa na bodi hiyo na kwamba watanzania wategemee kunufaika zaidi tofauti na hapo awali.

Nae mwekezaji aliyewekeza kwenye kiwanda hicho Bw. Philimon Millel amesema ataendelea kushirikiana na bodi hiyo kwani maamuzi yaliyofikiwa
yanalenga kuongeza tija na ameendelea kuikumbusha serikali ombi lake la kupewa umiliki wa kudumu wa kinu hicho kama ilivyofanya kwa wawekezajiwengine.

Chanzo: ITV
 
1469646555990.jpg
 
Monaban anaanza kuisoma huu utawala wa Arusha ni Chadema siyo kubebana kama ilivyokuwa kwa CCM tena
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom