Mombasa Republican Council wanataka nchi yao...

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Nimefuatilia harakati za hawa jamaa kwa muda mrefu, pamoja na mkwara mzito wa serikali ya Kenya kulipiga marufuku kundi hili na kuliita 'kundi haramu',
bado jamaa hawarudi nyuma. Bado wanasisitiza kuwa Pwani ya Kenya si sehemu ya taifa la kenya.
Pamoja na viongozi wao kufikishwa mahakamani kwa makkosa ya uhaini, jamaa hawaja-give up.
Moja ya madai yao ni kukithiri kwa umasikini katika maeneo ya Pwani wakati kuna rasilimali za kutosha.
Sasa hivi harakati zao zimehamia mtandaoni.

Profile Pictures | Facebook
 
hawana tofauti na wazenji hawa.
watu wa pwani wamefundishwa tabia mbaya ya kudeka deka na waarabu zaidi hata ya watoto.
kwa serikali ya kenya naamini itawa-pin down mmoja mmoja

Lakini madai yao ni ya msingi...
Kwanza,
Wamekuja na sababu za kihistoria, mambo ya Sultanate sijui na nini,
Pili,
Wana sababu za kimazingira, wanadai kuwa Pwani ni masikini sana pamoja na utajiri wa rasilimali uliopo kwao.
Tatizo lipo kwenye namna ya harakati zao na jinsi wanavyoziendesha. Zimekaa kisharishari sana!
 
sijui kama watafanikiwa kwenye hili swala lao
 
hawana tofauti na wazenji hawa.
watu wa pwani wamefundishwa tabia mbaya ya kudeka deka na waarabu zaidi hata ya watoto.
kwa serikali ya kenya naamini itawa-pin down mmoja mmoja

Kikubwa na kizuri zaidi wanadai nchi yao (Pwani ya Kenya including Mombasa) ni sehemu ya Zanzibar....:A S-coffee:
 
Nimefuatilia harakati za hawa jamaa kwa muda mrefu, pamoja na mkwara mzito wa serikali ya Kenya kulipiga marufuku kundi hili na kuliita 'kundi haramu',
bado jamaa hawarudi nyuma. Bado wanasisitiza kuwa Pwani ya Kenya si sehemu ya taifa la kenya.
Pamoja na viongozi wao kufikishwa mahakamani kwa makkosa ya uhaini, jamaa hawaja-give up.
Moja ya madai yao ni kukithiri kwa umasikini katika maeneo ya Pwani wakati kuna rasilimali za kutosha.
Sasa hivi harakati zao zimehamia mtandaoni.

Profile Pictures | Facebook

hata wakipewa hiyo republic they ll still be poor coz of their behaviour! Watajitenga after 5yrs watataka kuungana na kenya kwa kuwa umaskin utaongezeka na si kupungua!
 
Kikubwa na kizuri zaidi wanadai nchi yao (Pwani ya Kenya including Mombasa) ni sehemu ya Zanzibar....:A S-coffee:
wanafata ramani flani ya zamani,ambapo wakiwezeshwa watakuja dai hadi mikoa ya pwani kama tanga,dsm na ukanda wote wa bahari ya hindi,si watu wazuri hawa
 
Kwa hiyo watu wa Sudani ya Kusini wana haki ya kudai uhuru na watu wa Mombasa hawana.
 
Kikubwa na kizuri zaidi wanadai nchi yao (Pwani ya Kenya including Mombasa) ni sehemu ya Zanzibar....:A S-coffee:

hata mimi ndo wasiwasi wangu.
Kwamba wakipewa pwani ya Kenya, Zanzibar will be next.
Nimeona kwenye sehemu ya article zao wakiitaja Zanzibar...
 
hata wakipewa hiyo republic they ll still be poor coz of their behaviour! Watajitenga after 5yrs watataka kuungana na kenya kwa kuwa umaskin utaongezeka na si kupungua!

mkuu hujatoa fact za kujustify madai yako.
Kwanini umasikini uongezeke huko Pwani ya Kenya baada ya jamaa kuchukua Jamhuri yao?
Mimi nina wasiwasi kwa vile jamaa wanasukumwa na hisia kuliko facts, nimejaribu kuwaelimisha kule kwenye page yao, nimeambulia matusi.
 
hata wakipewa hiyo republic they ll still be poor coz of their behaviour! Watajitenga after 5yrs watataka kuungana na kenya kwa kuwa umaskin utaongezeka na si kupungua!

Nadhani maskini zaidi Kenya wako kule kaskazini ambako wanakula udongo na mizizi na mara nyingine kufa kwa njaa....Hao wa Mombasa sijawahi kusikia wakiombaomba maana wanabiashara zao za utalii ambao inachangia sehemu kubwa ya uchumi wa Kenya.:A S-coffee:
 
Ukiona mtu anakimbilia matusi ujue Hana hoja za msingi ... Aina Yao nadhani mnafahamu, walalamishi wa kutaka mikate wakati halimi ngano anacheza draft na karata huku akicheza taarabu.... Hoja si umaskini Ila Wana ajenda nyingine.... Pande za pwani zimevamiwa na kautundu ka kufadhiliwa na watu flani kutoka (...?..) , wakorofi sana hao ingawa panapowaka moto wao wanamwaga vifaa Vya maangamizi tu.. Mf. Mabomu as To SOMALIA
 
hawana tofauti na wazenji hawa.
watu wa pwani wamefundishwa tabia mbaya ya kudeka deka na waarabu zaidi hata ya watoto.
kwa serikali ya kenya naamini itawa-pin down mmoja mmoja

Chochote cha kujaribu kuwadhulumu wa Zanzibari wa bara wengi sana hatuafikiani nacho. Nna uhakika, na hapa hata mniite mdini mpaka mfyatuke, wanaounga dhulma kwa wazanzibari ni watu ambao si waislaam, sijakutana na Muislaam ambae anataka Wazanzibar wadhulumiwe.

Hali kadhalika wa Mombasa, zote hizi ni mbinu aina moja tu, kwani hiyo Mombasa yenyewe ilkuwa Zanzibar.
 
Nadhani maskini zaidi Kenya wako kule kaskazini ambako wanakula udongo na mizizi na mara nyingine kufa kwa njaa....Hao wa Mombasa sijawahi kusikia wakiombaomba maana wanabiashara zao za utalii ambao inachangia sehemu kubwa ya uchumi wa Kenya.:A S-coffee:

kaka?
Tunaposema mkoa wa Pwani kwa Kenya sio mwambao tu, ule mkoa unaextend mpaka Taveta na Voi ambako ni kwenye slopes za Mt. Kilimanjaro, kwa kule juu unaenda mpaka Garsen na kwenye mpaka wa Pwani na Nort East kwenye mji unaitwa Garissa, ambako ni karibu jangwa.
Madai yao ni kuwa kuna umasikini licha ya kuwepo kwa rasilimali nyingi, bahari na kadhalika.
Pia wanadai kuwa jamii za Pwani, kama Wamijikenda, Waamu na wengine wametengwa katika keki ya taifa, wametumia msamiati wa 'marginalization',
na nafasi zengine (same as madai ya kina Sheikh Issa Ponda kwa huku kwetu).
 
Back
Top Bottom