Moja ya Kauli za Kukatisha Tamaa za JK

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
"Sina namna ya kugeuka kuwa wingu la mvua nikaenda kugeuka wingu kubwa la mvua pale Mtera." Alisema Rais Kikwete alipoulizwa maswali na Waandishi wa Habari wakati anatembelea maonesho ya Sabasaba majuzi!

Source: Tanzania Daima.

My take:
Kwa kauli hii Kikwete ataondoka madarakani akiwa hajatatua tatizo la umeme! Kauli nyingine aliyowahi kutoa ni pale alipodai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni maskini!
 
Wewe ulitegemea kauli gani kutoka kwa huyu mlugaluga? Kama hana uwezo wa kutatua matatizo yanayoikabili nchi kwanini asiachie ngazi waje wale ambao wana ubunifu wa kumaliza matatizo yetu? Yeye alipokuwa anagombea urais alifikiri ikulu anakwenda kucheza ngoma?
 
Galileo aligundua na kusema dunia inalizunguka jua ..... watu wakamwona mwehu ..... je sisi watanzania tunaosema kuhusu matatizo yanayoikabili nchi yetu ni wehu...?
 
Kuna kitu jeshini wanaita maintenance of Morale...yaani hata mkipigwa kamanda wenu anasema hawa tumeshawashinda na sasa hizo wanazopiga ni za mwisho wameishiwa kabisa...kumbe anatafuta plan B...sasa huyu Rais wetu nasikia alikua jeshini lakini sidhani kama huyu jamaa anaweza kuongoza nchi ikashinda vita yeyote achilia mbali hii ya umeme,njaa,umasikini,wizi,,uporaji wa mali za umama!!! ikija vita kabisa hapa ya mtutu atakimbia kabisa..
 
mmhh natamani kama jk angesema leo anajiuzulu ingekuwaje na nani angeendesha hili gurudumu?..
 
Hiyo lugha yake imenikera sana, hata hivyo sio mara yake ya kwanza kusema vineno butu kama hivyo: check" wanaopata mimba shuleni wana vihele hele, wapinzani ni fotokopi, sijui chanzo cha umaskini tz, n.k"
Lugha za taarabu na mipasho ndio tamati ya kuwaza kwake!
 
"Sina namna ya kugeuka kuwa wingu la mvua nikaenda kugeuzawingu kubwa la mvua pale Mtera." Alisema Rais Kikwete alipoulizwa maswali na Waandishi wa Habari wakati anatembelea maonesho ya Sabasaba majuzi! Source: Tanzania Daima. My take: Kwa kauli hii Kikwete ataondoka madarakani akiwa hajatatua tatizo la umeme! Kauli nyingine aliyowahi kutoa ni pale alipodai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni maskini!

mkuu yaani hizi tu ndo unaona ni za ajabu? tafadhali sana embu jaribu kuzifuatilia zote, unaweza ukashangaa kila kauli moja inazidi uzito nyingine, yaani ukiambiwa uchanganue kauli yenye utata zaidi utachanganikiwa.
 
kazi tunayo kama ni hivi

mkuu yaani hizi tu ndo unaona ni za ajabu? tafadhali sana embu jaribu kuzifuatilia zote, unaweza ukashangaa kila kauli moja inazidi uzito nyingine, yaani ukiambiwa uchanganue kauli yenye utata zaidi utachanganikiwa.
 
Buchanan, Habari ya siku? Ulikuwa Sabatical nini umekuwa kimya muda mrefu?

Tukirudi kwenye mada, jana nimeangalia taarifa ya habari saa mbili usiku,hakuna kipya na cha maana alichosema lakini watu wazima na akili zao wanakimbilia kutaka kugonga naye wakati wakirudi nyumbani Umeme hakuna na yeye kishasema hawezi kuwa wingu, nyama kilo 5000, kilo ya mchele 1600, unga 400, nauli 400 one trip. Hakuna hata mmoja kati ya wale waliokuwa wanakenua aliyeuliza mzigo huu mgongoni kwetu watanzania utaisha lini. Hakuna aliyeuliza maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi.

Hakuna aliyeuliza kasi zaidi ilikuwa ya kwenda wapi, nguvu zaidi zilikuwa za kufanyia nini na ari zaidi ilikuwa ya kufikia wapi? Na jee mpaka sasa tumekaribia huko tulikokuwa tunaenda kwa kasi na kwa nguvu?
 
Amwachie Dr Slaa, hao mafisadi anaowafuga watakimbia nchi na "kufariki" kama Dr Ballali!

Balali yupo mkuu, walizika sanamu lake. Bado mgao anapata wa Rada, meremeta, EPA, na wa Madini yetu, anaishi ulya km vile yuko peponi wakati cc tunaishi kwenye giza. naamini siku viboko vitakapo lipuka, wahuni wote watakoma wanao jiita magamba
 
Ndio yale yale kama ya Hawa Ghasia jana asubuhi alishindwa kujitambua na kuongea pumba ati unajua tunategema mvua khaaa ivi huyu Ghasia hajijui yeye ni waziri anaongea kwenye TV ya Taifa na nchi nzima, twamsikiliza kauli zake mbuge wa CUF Tabora akamwambia huwezi uka kaaa kufikilia au kutegemea mvua ni ufilisikaji wa fikra na kutokuwa creative kweli ni twenty yrs mnashinwa tambua nini cha kufanya?

Hawa sio viongozi wamekuja kututawala jamani khaa.

Serikali imejua imechemka na wananchi wameisha jua na serikali inalitambua hilo sasa hawana hoja kabisa bali ni kutapatapa kwa maneno ya gazeti na karatasi na midomo ilihali utendaji ni zero
 
Back
Top Bottom